Baada ya kufika Moscow leo nimeamua kufuatilia saga la Dr. Shika, kumbe anasema ukweli

Baada ya kufika Moscow leo nimeamua kufuatilia saga la Dr. Shika, kumbe anasema ukweli

Huyu bwana ana akili timamu, hajarukwa akili kama wengi tulivyoamini.
Huyu jamaa ana akili timamu ila kwa maelezo yote hayo. Hana hiyo kampuni ni kiini macho cha kazi aliyokuwa anafanya
 
Aisee, maneno mengi yanaungana na ukweli, ila in reality unawezaje kuwatoroka KGB kindezi ndezi kama alivyosema yeye?
Inavyosemekana Dr shika alikua trained na hata katika mateso hayo nahs they got nothing... na inaonekana wali mu underestimate thus why.., na kumbuka kuna wenzake waliuliwa ... na pia cdhan kama alikuja dar directly kuhofia kua tracked yupo vizur ukilinganisha na msaada uliopo nyuma ya pazia
 
Kwa jinsi jamaa anavyoongea systematically, inaonesha ana akili zake timamu kabisa. Ila kuna masahibu makubwa amepitia ndo maana yuko hivyo.
 
Lancefort Ltd ni kampuni iliyosajiliwa nchini Russia miaka kadhaa iliyopita, na kwasasa haifanyi kazi kwa kipindi kirefu baada ya watendaji wake kupotea gafla kwa mazingira ya kutatanisha.

Kutoka mjini Rostov on don napokaa mpaka Moscow ni mwendo mrefu kidogo ambao ni km 1200 na zaidi, kwa mwendo wa trein ni 5hrs,
nimefika mjini moscow na kuanza kuuliza hasa legality ya kampuni hiyo ndani ya moscow na Urusi kwa ujumla, nimefanikiwa kupata maelekezo ya kukutana na Mtanzania mmoja anaisha mtaa wa Tverskaya Street, ambaye kanikaribisha na kuanza kufanya uchunguzi wangu, nikaamua kwanza nipate hifadhi ndani ya hotel ya Sputnik.

Baada ya kwenda kwa watanzania wanaoishi huku nimegundua huyu mzee alipata matatizo kwa kuhisiwa ni spy wa Marekani, ambaye kapandikizwa kutokea Afrika, na amekuwa akitafutwa na kufuatiliwa nyendo zake zote kuanzia kwenye kampuni yake na nyumbani alipokuwa anaishi.
Mke wake bi Luisa Kvonkov ndo alibanwa na kueleza kwao ni Tanzania Magu, Lakini inasemekana kwamba kuna kampuni kubwa la kimarekani aidha shirika la upelelezi ambalo liko nyuma ya kampuni ya Lancefort, ndio chanzo cha kutiwa msuko suko uko alikokuwa anamiliki kampuni hiyo.

Shirika la Lancerfort limekuwa likimiliki asset kubwa nchini urusi na kwingineko duniani wakati chanzo cha hela yao hakijulikani, hivyo moja kwa moja kuhisiwa ni miongoni mwa mashirika ma spy ambao wafadhili wake ni wamarekani ambao wana uhasama wa mda mrefu na Urusi.

Wametelekeza mali nyingi kukiwemo na private jets na magari ya thamani.

Kupitia wapelelezi wa ndani ya urusi ambao walilichunguza shirika ambalo inasemekana rais wake ni Dr Luis Shika kwa kipindi kile, waligundua mawasiliano ya karibu na baadhi ya mashirika yafuatayo AMNESTY INTERNATIONAL, CIA, FBI , HGRE, OKLE, ambayo mara nyingi huwa ni waanzilishi wa upelelezi katiKa nchi nyingi,

Baada ya kugundua hayo walitekwa na kuwekwa mateka na wawili kuuwawa, mmoja wapo akiwa mkenya Edward Koinange na mwingine wa Siera Leone Yunusu AKhbu, Na wawili kukimbilia Tanzania lakini Rais wao akapelekwa hospitali baada ya kuwatoroka akiwa ameumizwa vibaya, hakutibiwa Urusi alitoroshwa kinyemela mpaka mjini Dnipro Ukraine, na kutoroshewa Tanzania,
Baada ya kufika Tanzania hakuenda moja kwa moja kwao akajificha mjini Dar es salaam, (Haya ni maelezo kwa mujibu wa mtu wake wa karibu)
Baadae kutorokea Uhispania Mjini Malaga , amekaa malaga miez 8 Na kurudi Tanzania,

Mwaka 2012 wakaidhinisha malipo kutoka marekani ambayo bado yapo kwenye mlolongo wa
kukamilisha mchakato,

WITO KWA BALOZI ZETU TUNAOMBA MUWASAIDIE HAWA WATANZANIA WANAOKUWA NA MATATIZO MUWASAIDIE

Tukiachana na Shika wapo watanzania wengi wanaokosa msaada wa karibu sana kutoka Kwa balozi zetu hizi ,

Ukisoma ukatafakari haitadhuru

Tufanye nimemaliza

KUNA MENGI SITAYAANDIKA HAPA KUTOKANA NA KUJUA KWAMBA KUMBE HII ISHU NI CRUCIAL , NA KULINDA USALAMA WA DR,

PIA YATAENDELEA KUWA KUMBUKUMBU ZANGU NA KUZIPELEKA MAALI ZITAITAJIKA KWA KUMSAIDIA DR,

USIKURUPUKE KUKOPI HABARI HII, MAANA CODES ZOTE NINAZO MIMI UTASHINDWA KUITETEA,MTU PEKEE MWENYE UWEZO WA KUWEKA EVIDENCE NI MIMI, IKITOKEA UKAKOPI SEMA UMEITOA WAPI,

Britanicca

fac4c12cdf742cab874da9e575e22549.jpg
A cock and bull tale not worthy of anybody who claims to be a scholar in a foreign country on Tanzania government sponsorship. You deserve to be starved to death in Russia, Ukraine or wherever it is your bogus claim to academia got you there.
 
Na kirusi.mzee.anakigonga vema
Nadhani habari zake kirefu tunaweza kuzipata ktk makala za kirusi. Wengi wetu hatuna uwezo wa kuelewa kirusi tunaishia kutengeneza stori.
Katika hayohayo machache yaliyopatikana, ni kwamba Jasusi ana namna nyingi ya ku fake life style..msimchukulie poa tu.
Watengeneza filamu na waandishi wa vitabu vya kipelelezi kaeni naye huyu mzee atawapa stori itawaingizia pesa nyingi.
 
Pia hana meno ya mbele.
Halafu sijui mawazo yamemfanya aonekane ndivyo sivyo.
This time tungefanya Hata harambee huku akisubiri mpunga wake.
Mana Hata ndugu walimtenga japo nao wamekiri jamaa yupo njema.Na Hata gazeti la mwananchi walipotembelea Nyumbani kwao.Dr.Shika.Sio watu wa kawaida.
Wana mahekalu
Kina nani wana mahekalu?
 
Back
Top Bottom