Baada ya kufukuzwa Mbeya, Dr. Bingwa feki wa magonjwa ya moyo aendeleza libeneke Moro

Whisper

JF-Expert Member
Joined
Jun 2, 2009
Posts
502
Reaction score
207
Yule daktari aliyehatarisha maisha ya wananchi wa Mbeya kwa kujiita Dr. bingwa wa magonjwa ya moyo, ambaye aliondolewa kwa nguvu ya kalamu ya mwandishi, sasa ameibukia Morogoro.

Dr. huyo anayefahamika kwa jina la Nyagori, ambaye hajawahi kusomee degree yoyote ya udaktari, ameibuliwa kwa mara nyingine na kalamu ya Raia Mwema. Hivi ndivyo Raia Mwema ilivyoripoti kwa ufupi:

DAKTARI bingwa mshauri wa magonjwa ya moyo (consultant cardiologist), Harun Elmada Nyagori wa Hospitali ya Mkoa wa Morogoro, anadaiwa kupachikwa udaktari huo bingwa bila kuwa na sifa zinazostahili, vyanzo kadhaa vya habari vimefichua taarifa hizo.

Vyanzo hivyo vya habari vinadai ya kwamba, hata taarifa zilizopo kwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Morogoro zinathibitisha utata katika wasifu wa kitaaluma wa mtaalamu huyo.

Inadaiwa kwamba kumebainika utata wa taarifa za wasifu wake (CV), kwa mfano, tarehe yake ya kuzaliwa, elimu yake ya sekondari hadi taaluma yake.

Wakati taarifa zake za kiofisi zikidaiwa kuonesha kuwa alisoma elimu ya sekondari kuanzia mwaka 1993 na kuhitimu mwaka 1998, cheti chake cha kidato cha nne kinaonesha kuwa alihitimu elimu ya sekondari mwaka 1996 akiwa amepewa cheti cha daraja la nne (division IV) baada ya kufaulu masomo manne alama D, moja alama C na manne yaliyosalia akipata F.

Taarifa zake hazioneshi amepitia mafunzo yoyote ya afya hapa nchini bali zinaonesha amefanya masomo yake ya awali ya utabibu (preparatory foundation course in medicine) kati ya mwaka 1998 na 1999, huko Ukraine katika Chuo Kikuu cha Lugansk State Medical.
 
Duh! Hawa ndo madaktari wanaotoka nje na wizara inawalea. Amehamishwa kutoka mbeya na kuhamishiwa moro. Huyo hata co haitwi sasa kafikaje hospitali ya rufaa? Then ya mkoa? Mbona hata hospitali za wilaya ma co tunawapunguza taratibu? Hii nchi ni ya ajabu sana.
 
Dr Nyagori Bingwa wa Magonjwa ya moyo !.
 
Tunapojadili mambo muhimu yenye mustakabali wa nchi tusiache na hawa watu wanaobebwa na watu walioko wizarani. Huyu 'dr' aliwahi kuwa mganga mfawidhi wa hospitali ya mkoa Mbeya madudu yake yakafichuliwa na kuondolewa. Cha ajabu akahamishiwa hospitali ya mkoa morogoro huku elimu yake ikiwa haieleweki! Aliwahi kuandikwa na raia mwema kuhusu utata wa elimu yake lakini hakuwahi kuchukua hatua zozote za kisheria kwa kuchafuliwa au kujitokeza na kusema ukweli. Sasa hivi ni intern coordinator wa hospitali ya Morogoro. Tunavyokamata madaktari feki na hawa waliowekwa na watu wasio waaminifu ni lazima wachunguzwe kama kweli wanastahili kile wanacholipwa? Kuna mwaka pia kuna mtu ambaye alikuwa na connection na kiongozi wa wizara ya afya alifoji vyeti kuwa amemaliza Bsc pharmacy na kula posho ya mwaka mzima, waliporudi kufanya mtihani wa usajili ndipo alipokamatwa kwani alifeli vibaya sana. Walipoitisha vyeti vyake ikagundulika ni fake.
 
Huyu jamaa sijui kwanini haguswi. Ni aibu aisee. Mwache ale vichwa. Kwa watanzania si muhimu. Mtu aliyeanzisha thread nzuri imechangiwa na watu watano. Ikija suala la Zito, Slaa, Ridhiwani watu wanafurika... Watanzania twafa kwa uzembe wetu.
 
PIA anamiliki hospitali yake binafsi pale mjini morogoro inaitwa "afya medicare specialized clinic" anakula vichwa vya wamasai kama hana akili nzuri.
 
Huyu jamaa sijui kwanini haguswi. Ni aibu aisee. Mwache ale vichwa. Kwa watanzania si muhimu. Mtu aliyeanzisha thread nzuri imechangiwa na watu watano. Ikija suala la Zito, Slaa, Ridhiwani watu wanafurika... Watanzania twafa kwa uzembe wetu.

Watanzania tunapenda kujadili vitu vyepesi na vya umbea. Ndo maana ccm wakiona kuna jambo linawaelemea wanatafuta mtu aanzishe kitu kipya ili kitutoe kwenye mstari. Mfano kina Kigwangala kuja na hoja ya kumng'oa speaker ni kutaka tuwashabikie bila matokeo yoyote yanayotarajiwa.
 
Jamani mimi nilienda kwenye zahanati yake mbeya enzi hizo ilikuwa Makunguru kwa kazi fulani jamani kweli nchi ina makanjanja kila kona, yaani ana laptop apple ambayo hata kufungua na kulink na mashine ya cadiograph alishindwa alichonizuga akasema kuna program wamarekani wameondoka nayo hivyo anaomba nije wiki tatu zijazo. Chanzo ni pale alipofungua mashine hiyo na kunieleza kuwa taarifa za mgonjwa zinasomwa na kutafsiriwa marekani nikamwambia hebu twende hatuakwa hatua na kwakuwa kulikuwa tayari na taarifa za mgonjwa zinazohitaji uchambuzi huo ! Nikaona ghafla anatoa jasho na maelezo yakawa mengi akiwa ameshika mouse kama ujuavyo kampuni ya apple na bidhaa zake mac zina application tofauti kidogo na windows kubrows mtandao akanuliza hivi tunaconnect kwenye ipi hapa? Nadhani hakujua ile alama ya safari haijui hadi mwisho alifunika komputa na akaniomba tutoke Kwani katibu tawala mkoa amemwita ikawa ndo kukimbia!
 
Hii wizara ya afya imejaa makanjanja wengi sana na wizara ipo kimya. Mtu akijiita tu mi dr bila hata kuthibitisha vyeti vyake wanampa ajira. Mfano mzuri ni wakati wa kupanga intern drs, unaambiwa tu uende na barua ya chuo na copy za vyeti vya form four na six. Hivyo vyote unaweza kuvitengeneza mtaani na ukapangiwa kituo. Nashauri wawe wanakuwa na list kutoka chuoni(vyuo vya ndani) ya wahitimu wa mwaka husika!
 
Lakini mimi na hoja nzito kuhusu huyu mjamaa,tunajua udaktari sio kuuza nyanya sokoni,atakuwa miaka hiyo ana practice ameshafanya malpractice ajauwa?mimi nahisi watu wana bifu na huyu mtu au sometimes he is good performa,tuchunguze kwa nini watuwanamuonea wivu.maana watz nao bwana hatupendi maendeleo ya watu hasa akiwa challenged.
 
Mkuu inaelekea jamaa mnagombania madaraka,au unamwonea wivu.Taarifa yako ni ya majungu japo sikufaha wewe wala huyo dokta wako.Ina maana wewe umejuaje maisha yake ya ndani mpaka ujue anaendekeza 'LIBENEKE' Morogoro?? Je,amewahi kukugegeda wewe na wengine wengi unaowafahamu hapo?? Wewe uko Mbeya uko Morogoro ulienda kufanya nini mpaka yeye tu ndio ujue maisha yake ya ndani pamoja kwamba Moro kuna watu wengi?? Acha wivu na kashfa za kishoga wewe,shindana kimaendeleo na si ki majungu na uongo wa kipumbavu.
 
Hata specialist wa moyo marehemu DR Masau (RIP) madaktari wa wizara ya Afya wakishirikiana na wale wa Muhimbili walimpiga vita eti hana cheti cha F.6 ili wahalalishe ufisadi wao wa kupeleka wagonjwa India kutibiwa kwa gharama kubwa ambapo zingepungua kama wagonjwa wangetibiwa kwa Dr Masau na pengine hata uchakachuaji usingekuwepo.

Sent from my BlackBerry 9220 using JamiiForums
 

Mkuu nakuunga mkono.huyu itakuwa kaachwa kimapenzi na ndio maana analalamika 'jamaa anaendeleza libeneke' anaingiza umalaya wake kwenye kazi ya mtu.
 

Kamdanganye mumeo acheni wivu wa kishoga nendeni shule
 
Hatari sana , serikali legelege huwa na misingi dhaifu katika usimamizi wa rasilimali zake . Haiwezekani serikali makini ikafanya madudu kama haya ,suluhisho ni kumwondoa kabisa ama ni kumuhamisha !!!!
 
Hatari sana , serikali legelege huwa na misingi dhaifu katika usimamizi wa rasilimali zake . Haiwezekani serikali makini ikafanya madudu kama haya ,suluhisho ni kumwondoa kabisa ama ni kumuhamisha !!!!

Acheni wivu wa kishoga nyie.ukabila umewajaa.mambo yenu ya kuachwa kimapenzi msiingize na kazi za watu.
 
Hatari sana , serikali legelege huwa na misingi dhaifu katika usimamizi wa rasilimali zake . Haiwezekani serikali makini ikafanya madudu kama haya ,suluhisho ni kumwondoa kabisa ama ni kumuhamisha !!!!

Jamani mimi huyo Dr namfahamu akiwa Mbeya pale Makunguru kwenya clinic yake,

Amenitibu na namshukuru sana! sana! maana naamini Mungu alipitia kwake ili niweze kupona na nilipona, aliweza kugundua tatizo ambalo hata referral walishindwa. Ni kwel ana vi element vya ubabaishaji katika kutibu,, kuna dawa alinichomekea weeeee,,,ilikuwa balaaaa,,

But all in all thanks Mr Nyagori,,,,, nitakukumbuka daima.
 

Mshukuru Mungu, ndiye aliyekuponya.
I know the guy, he is a pompous quack!

Sasa ana clinic yake ya Moyo Morogoro mjini, aendelee kuua. Cha kushangaza ni kwanini wamempa leseni ya kufungua hiyo clinic.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…