Yule daktari aliyehatarisha maisha ya wananchi wa Mbeya kwa kujiita Dr. bingwa wa magonjwa ya moyo, ambaye aliondolewa kwa nguvu ya kalamu ya mwandishi, sasa ameibukia Morogoro.
Dr. huyo anayefahamika kwa jina la Nyagori, ambaye hajawahi kusomee degree yoyote ya udaktari, ameibuliwa kwa mara nyingine na kalamu ya Raia Mwema. Hivi ndivyo Raia Mwema ilivyoripoti kwa ufupi:
DAKTARI bingwa mshauri wa magonjwa ya moyo (consultant cardiologist), Harun Elmada Nyagori wa Hospitali ya Mkoa wa Morogoro, anadaiwa kupachikwa udaktari huo bingwa bila kuwa na sifa zinazostahili, vyanzo kadhaa vya habari vimefichua taarifa hizo.
Vyanzo hivyo vya habari vinadai ya kwamba, hata taarifa zilizopo kwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Morogoro zinathibitisha utata katika wasifu wa kitaaluma wa mtaalamu huyo.
Inadaiwa kwamba kumebainika utata wa taarifa za wasifu wake (CV), kwa mfano, tarehe yake ya kuzaliwa, elimu yake ya sekondari hadi taaluma yake.
Wakati taarifa zake za kiofisi zikidaiwa kuonesha kuwa alisoma elimu ya sekondari kuanzia mwaka 1993 na kuhitimu mwaka 1998, cheti chake cha kidato cha nne kinaonesha kuwa alihitimu elimu ya sekondari mwaka 1996 akiwa amepewa cheti cha daraja la nne (division IV) baada ya kufaulu masomo manne alama D, moja alama C na manne yaliyosalia akipata F.
Taarifa zake hazioneshi amepitia mafunzo yoyote ya afya hapa nchini bali zinaonesha amefanya masomo yake ya awali ya utabibu (preparatory foundation course in medicine) kati ya mwaka 1998 na 1999, huko Ukraine katika Chuo Kikuu cha Lugansk State Medical.