Jamani mimi huyo Dr namfahamu akiwa Mbeya pale Makunguru kwenya clinic yake,
Amenitibu na namshukuru sana! sana! maana naamini Mungu alipitia kwake ili niweze kupona na nilipona, aliweza kugundua tatizo ambalo hata referral walishindwa. Ni kwel ana vi element vya ubabaishaji katika kutibu,, kuna dawa alinichomekea weeeee,,,ilikuwa balaaaa,,
But all in all thanks Mr Nyagori,,,,, nitakukumbuka daima.
clinic yake ya mbeya ilikuwa inaitwaje? na je bado ipo? pia naomba unijuze hapo alikuwa anatumia jina gani?
Yule daktari aliyehatarisha maisha ya wananchi wa Mbeya kwa kujiita Dr. bingwa wa magonjwa ya moyo, ambaye aliondolewa kwa nguvu ya kalamu ya mwandishi, sasa ameibukia Morogoro.
Dr. huyo anayefahamika kwa jina la Nyagori, ambaye hajawahi kusomee degree yoyote ya udaktari, ameibuliwa kwa mara nyingine na kalamu ya Raia Mwema. Hivi ndivyo Raia Mwema ilivyoripoti kwa ufupi:
DAKTARI bingwa mshauri wa magonjwa ya moyo (consultant cardiologist), Harun Elmada Nyagori wa Hospitali ya Mkoa wa Morogoro, anadaiwa kupachikwa udaktari huo bingwa bila kuwa na sifa zinazostahili, vyanzo kadhaa vya habari vimefichua taarifa hizo.
Vyanzo hivyo vya habari vinadai ya kwamba, hata taarifa zilizopo kwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Morogoro zinathibitisha utata katika wasifu wa kitaaluma wa mtaalamu huyo.
Inadaiwa kwamba kumebainika utata wa taarifa za wasifu wake (CV), kwa mfano, tarehe yake ya kuzaliwa, elimu yake ya sekondari hadi taaluma yake.
Wakati taarifa zake za kiofisi zikidaiwa kuonesha kuwa alisoma elimu ya sekondari kuanzia mwaka 1993 na kuhitimu mwaka 1998, cheti chake cha kidato cha nne kinaonesha kuwa alihitimu elimu ya sekondari mwaka 1996 akiwa amepewa cheti cha daraja la nne (division IV) baada ya kufaulu masomo manne alama D, moja alama C na manne yaliyosalia akipata F.
Taarifa zake hazioneshi amepitia mafunzo yoyote ya afya hapa nchini bali zinaonesha amefanya masomo yake ya awali ya utabibu (preparatory foundation course in medicine) kati ya mwaka 1998 na 1999, huko Ukraine katika Chuo Kikuu cha Lugansk State Medical.
Hata mimi amewahi nitibu na nina ndugu alikua na shida ya figo alimsaidiabsanasana hapo morogoro ana miliki hospitali na inatambulika kisheria inapokea hadi bima .Sipendi kuwa mnafiki binafsi alinisaidia sana.
Inawezekana kweli ni mbabaishaji lakini jamaa kama ni kusomea medicine kasomea na ni cardiologist,... Udaktari mtu kama hujui kutu huwezi hata kukaa ukamsikiliza mgonjwa sio mchezomchezo. Huyu ni dr kweli licha ya ubabaishaji unaoonekana, ana vyeti na wizara inamtambua.Afya Medics Center kama sijakosea kwa sasa haipo tangu amehama Mbeya alifunga akafungua Moro
Kuongelea taaluma ya mtu fulani, bora hata uwe una taaluma hata kidogo inayo lingana na ya huyo unaemwongelea, au hata uwe nauelewa kiasi tu juu ya taaluma yake, na ikiwzekana umahamu mtu na taaluma yake kwa kina pia.Jamani mimi nilienda kwenye zahanati yake mbeya enzi hizo ilikuwa Makunguru kwa kazi fulani jamani kweli nchi ina makanjanja kila kona, yaani ana laptop apple ambayo hata kufungua na kulink na mashine ya cadiograph alishindwa alichonizuga akasema kuna program wamarekani wameondoka nayo hivyo anaomba nije wiki tatu zijazo. Chanzo ni pale alipofungua mashine hiyo na kunieleza kuwa taarifa za mgonjwa zinasomwa na kutafsiriwa marekani nikamwambia hebu twende hatuakwa hatua na kwakuwa kulikuwa tayari na taarifa za mgonjwa zinazohitaji uchambuzi huo ! Nikaona ghafla anatoa jasho na maelezo yakawa mengi akiwa ameshika mouse kama ujuavyo kampuni ya apple na bidhaa zake mac zina application tofauti kidogo na windows kubrows mtandao akanuliza hivi tunaconnect kwenye ipi hapa? Nadhani hakujua ile alama ya safari haijui hadi mwisho alifunika komputa na akaniomba tutoke Kwani katibu tawala mkoa amemwita ikawa ndo kukimbia!
Hata mimi amewahi nitibu na nina ndugu alikua na shida ya figo alimsaidiabsanasana hapo morogoro ana miliki hospitali na inatambulika kisheria inapokea hadi bima .