Baada ya kufukuzwa Mbeya, Dr. Bingwa feki wa magonjwa ya moyo aendeleza libeneke Moro

Baada ya kufukuzwa Mbeya, Dr. Bingwa feki wa magonjwa ya moyo aendeleza libeneke Moro

huyu mtu amepewa tuzo na ''wazungu'' juu ya tafiti flani hivi alizofanya kuhusu mambo haya ya utabibu...sijui hata inakuaje mambo haya
 
Jamani mimi huyo Dr namfahamu akiwa Mbeya pale Makunguru kwenya clinic yake,

Amenitibu na namshukuru sana! sana! maana naamini Mungu alipitia kwake ili niweze kupona na nilipona, aliweza kugundua tatizo ambalo hata referral walishindwa. Ni kwel ana vi element vya ubabaishaji katika kutibu,, kuna dawa alinichomekea weeeee,,,ilikuwa balaaaa,,

But all in all thanks Mr Nyagori,,,,, nitakukumbuka daima.

clinic yake ya mbeya ilikuwa inaitwaje? na je bado ipo? pia naomba unijuze hapo alikuwa anatumia jina gani?
 
clinic yake ya mbeya ilikuwa inaitwaje? na je bado ipo? pia naomba unijuze hapo alikuwa anatumia jina gani?

Afya Medics Center kama sijakosea kwa sasa haipo tangu amehama Mbeya alifunga akafungua Moro
 
Kuna jamaa alikuwa anamsimulia huyu Nyagori, ikabidi nitafute posti yake humu. Anasema Haruni Nyagori kafanya internship isiyoeleweka huko Mbeya Rufaa miaka ya 2007/2008. Ati kila alipokuwa zamu alikuwa akiwalipa posho interns wenzake ili wamshikie zamu. Yeye alikuwa hawezi. Nasikia baada ya hapo 2009 hadi 2011 alikuwa Medical Officer Incharge wa Mbeya Regional Hospital.

Lakini ajabu ukiangalia Mtandao wa Medical Council of Tanganyika, jamaa inaonekana kamaliza Internal Medicine 2008 na Cardiology 2011. Sasa wajiuliza mbona qualifications zake zinatatiza? Ilikuwaje mwaka 2008 na 2011 amalize Internal Medicine na Cardiology huko Urusi wakati alikuwa Mbeya?

Huyu jamaa analindwa na nani? Mwangalie kwenye namba 94!!!
image.png
 
MMED in internal medicine at lugansk state university ni 2 years only....so, inawezekana kwa mtaala wa ukrein
Ko, kama kamaliza MD 2005, ITS VERY POSSIBLE KUMALIZA MMED 2008 na CARDIOLOGY 2011 at lungansk
 
Yule daktari aliyehatarisha maisha ya wananchi wa Mbeya kwa kujiita Dr. bingwa wa magonjwa ya moyo, ambaye aliondolewa kwa nguvu ya kalamu ya mwandishi, sasa ameibukia Morogoro.

Dr. huyo anayefahamika kwa jina la Nyagori, ambaye hajawahi kusomee degree yoyote ya udaktari, ameibuliwa kwa mara nyingine na kalamu ya Raia Mwema. Hivi ndivyo Raia Mwema ilivyoripoti kwa ufupi:

DAKTARI bingwa mshauri wa magonjwa ya moyo (consultant cardiologist), Harun Elmada Nyagori wa Hospitali ya Mkoa wa Morogoro, anadaiwa kupachikwa udaktari huo bingwa bila kuwa na sifa zinazostahili, vyanzo kadhaa vya habari vimefichua taarifa hizo.

Vyanzo hivyo vya habari vinadai ya kwamba, hata taarifa zilizopo kwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Morogoro zinathibitisha utata katika wasifu wa kitaaluma wa mtaalamu huyo.

Inadaiwa kwamba kumebainika utata wa taarifa za wasifu wake (CV), kwa mfano, tarehe yake ya kuzaliwa, elimu yake ya sekondari hadi taaluma yake.

Wakati taarifa zake za kiofisi zikidaiwa kuonesha kuwa alisoma elimu ya sekondari kuanzia mwaka 1993 na kuhitimu mwaka 1998, cheti chake cha kidato cha nne kinaonesha kuwa alihitimu elimu ya sekondari mwaka 1996 akiwa amepewa cheti cha daraja la nne (division IV) baada ya kufaulu masomo manne alama D, moja alama C na manne yaliyosalia akipata F.

Taarifa zake hazioneshi amepitia mafunzo yoyote ya afya hapa nchini bali zinaonesha amefanya masomo yake ya awali ya utabibu (preparatory foundation course in medicine) kati ya mwaka 1998 na 1999, huko Ukraine katika Chuo Kikuu cha Lugansk State Medical.

Wahusika Morogoro wakimuachia huyu jamaa, hasa sasa katika kutafuta wafanyakazi wasio na sifa; basi watakuwa majibu yanayopaswa kutumbuliwa.
 
Mjini shule 1 yr in (preparatory foundation course in medicine) unakuwa MD,hii ni zaidi ya hatari,Mungu atuongoze kwenye hili giza.
 
dr..jpg

Daktari mshauri mwandamizi wa magonjwa ya Moyo kutoka Hospitali ya Rufaa mkoani Morogoro, nchini Tanzania amepewa tuzo na Chuo Kikuu cha Magonjwa ya Moyo Marekani (American college of Cardiology).

Dkt Harun Emalda Nyagori ambaye pia ni Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Mtakatifu Francis, amepewa tuzo ya kutambuliwa kwa utafiti na uzoefu wake katika ushauri kuhusu magonjwa ya moyo barani Afrika.

Baadhi ya utafiti uliofanywa na Dkt Nyagori ni pamoja na kushindwa kufanya kazi kwa dawa za maradhi ya moyo nchini Tanzania na changamoto za magonjwa ya moyo nchini humo.
Tuzo nyingine alizopata ni kutoka kwa Jumuiya ya madaktari bingwa wa maradhi ya moyo barani Ulaya na Jumuiya ya Umoja wa Madaktari bingwa wa maradhi ta moyo nchini Mexico.

Dkt Nyagori ni kati ya madaktari bingwa wachache nchini Tanzania wanaoshauri na kutibu maradhi ya moyo yasiyohusiana na upasuaji
Amekuwa akifanya kazi hiyo kwa miaka saba sasa akiwasaidia wangonjwa katika mkoa wa Morogoro na mikoa jirani inayopakana na Morogoro.

Dkt. Nyagori pia aliwahi kupokea tuzo nyingine. Septemba 2015 alipokea tuzo kutoka Jumuiya ya Madaktari Bingwa wa Maradhi ya Moyo Barani Ulaya, London.

Tuzo nyingine ni kutoka Jumuiya ya Umoja wa madaktari bingwa wa maradhi ya Moyo nchini Mexico mwaka 2016.

Kwa kushirikiana na madaktari wengine, Dkt Nyagori amekuwa akiwatibu kwa wastani wagonjwa 40 hadi 60 kwa siku.

Idadi inayofikia wastani wa wagonjwa 160 - 200 kwa wiki.
 
Sipendi kuwa mnafiki binafsi alinisaidia sana.
Hata mimi amewahi nitibu na nina ndugu alikua na shida ya figo alimsaidiabsanasana hapo morogoro ana miliki hospitali na inatambulika kisheria inapokea hadi bima .
 
Afya Medics Center kama sijakosea kwa sasa haipo tangu amehama Mbeya alifunga akafungua Moro
Inawezekana kweli ni mbabaishaji lakini jamaa kama ni kusomea medicine kasomea na ni cardiologist,... Udaktari mtu kama hujui kutu huwezi hata kukaa ukamsikiliza mgonjwa sio mchezomchezo. Huyu ni dr kweli licha ya ubabaishaji unaoonekana, ana vyeti na wizara inamtambua.
 
Jamani mimi nilienda kwenye zahanati yake mbeya enzi hizo ilikuwa Makunguru kwa kazi fulani jamani kweli nchi ina makanjanja kila kona, yaani ana laptop apple ambayo hata kufungua na kulink na mashine ya cadiograph alishindwa alichonizuga akasema kuna program wamarekani wameondoka nayo hivyo anaomba nije wiki tatu zijazo. Chanzo ni pale alipofungua mashine hiyo na kunieleza kuwa taarifa za mgonjwa zinasomwa na kutafsiriwa marekani nikamwambia hebu twende hatuakwa hatua na kwakuwa kulikuwa tayari na taarifa za mgonjwa zinazohitaji uchambuzi huo ! Nikaona ghafla anatoa jasho na maelezo yakawa mengi akiwa ameshika mouse kama ujuavyo kampuni ya apple na bidhaa zake mac zina application tofauti kidogo na windows kubrows mtandao akanuliza hivi tunaconnect kwenye ipi hapa? Nadhani hakujua ile alama ya safari haijui hadi mwisho alifunika komputa na akaniomba tutoke Kwani katibu tawala mkoa amemwita ikawa ndo kukimbia!
Kuongelea taaluma ya mtu fulani, bora hata uwe una taaluma hata kidogo inayo lingana na ya huyo unaemwongelea, au hata uwe nauelewa kiasi tu juu ya taaluma yake, na ikiwzekana umahamu mtu na taaluma yake kwa kina pia.
Kama huna hata moja miongoni mwa hayo si busara kuongea uongo na kufurahisha vijiwe, na kumchafua mtu, kama ulijua sio Dr ulifuata nn kwake, Kumbuka hiyo ni taaluma, unapo mchafua huyo, ni sawa na kuchafua wengine pia na kuchafua taaluma za watu.
Nenda shule kasome, nenda kasome hata level ya clinical assistance, yaani cheti tu thn urudi uongee humu vzr!
Usipoheshimu taaluma za wenzako huwez kuendelea hata kidogo kwenye maisha yako,
Nimekwambia ivo sababu namfahumu huyo Dr, nimefanya nae kazi ya utabibu, amefanya/anafanya kazi ya utabibu na wengine wengi tu, na watu wengi hasa medical students wanaowaza maisha wanapitia mikononi mwake!
Kasome bro!
 
Back
Top Bottom