Jumanne Mwita
JF-Expert Member
- Nov 18, 2014
- 530
- 1,446
Leo nataka niwape stori ya kweli najua kila mmoja wetu anamambo yake kutokea huko nyuma katika maisha yake watayatoa kwa wakati wao ila mimi nimona muda huu unanifaa kushare haka kastori kafupi tu.
Bhana ngoja nitoe stori yangu moja hivi.
Mwaka 2018 nilikuwa Bukoba najishughulisha katika harakati zangu za hapa na pale. Nikapata chumba mtaa wa matopeni bwana ile nyumba inamlango mmoja sasa ukiingia unapishana na sebure ya mwenye nyumba.
Siku zikaenda akaja binti mmoja hivi ikasemekana ni mdogo wake na mwenye nyumba anamuita kaka.
Mimi yangu macho niko kivyangu vyangu ila nilikuwa sina muda na yule demu, demu nae kumbe alikuwa anapima upepo baada ya muda kwenda ilipita kama miezi 6 kwenda na wiki kadhaa hivi.
Demu uvumilivu ukamshinda ikabidi anifate geto humo humo kwao akagonga mlango kufungua namkuta yeye tukasaliminiana baadae akasema anaomba nimnunulie kifurushi simu yake inadaiwa kanipa vocha na namba yake ya simu ili nikiingiza vocha nimrushie kifurushi chake cha dakika.
Nikafanya kama alivyotaka kwa sababu mimi sikuwa na lengo baya kwake na wala sikuwa namfikiria kwa lolote lile isipokuwa niliona kama natoa msaada sababu alikuwa anadaiwa kwenye laini yake.
Kesho yake akaruka na mimi kama kawaida "Mambo" muda huo namba nilisha futa sina namba naona kama namba mpya sielewi kuendelea ndio najua niyeye.
Baada ya miezi minne hivi mawasiliano yalikuwepo ila siyo ya kumtaka nilimchukulia kama mtu baki tu au ni mtu naemjua basi nikienda job tunaenda nae maana muda huo nilikuwa na usafiri wa pikipiki CC250 cruise nikawa naona kama ni dada angu au mdogo wangu tu kama tunavyoishi nyumba moja kumbe mwenzangu anamawazo yake anayajua mwenyewe.
Sikumoja niko geto ni usiku huo kagonga mlango kufungua yuko kwenye kanga moja, yaani moja kwa moja ndani anafunga na mlango kabisa nikamwambia toka nje au nimpigie kaka ako kuwa upo ndani kwangu kasema piga tu hamna shida.
Bwana ikabidi nifanye kweli nikaifinya ile sijamaliza viziri mlango unagongwa nasikia sauti ya kaka ake anasema najua uko na flani humo mwambie atoke mwenyewe kusikia hivyo nikajua huu mtego sasa mbuzi kafia kwa muuza bucha.
Nikafungua mlango nikamwambia toka nenda unaitwa, hapo nipo kwenye fumanizi sasa kaka mtu na mkewe wakaja juu nikawaambia mlichokiona hapa hata mimi mwenyewe nashangaa kimetokeaje labda tumuulize mtuhumiwa mimi sihusiki kwakweli nikafunga mlango nikabakia ndani.
Nikawa nasikia sauti tu uko nje wanasema wewe Jumanne utamuoa huyu maana haiwezekani mshiriki kama mke na mme alafu umuache nikikumbuka walikuwa niwatu wa maombi hatari kwanza usiku ule kabla ya kwenda kulala walipiga maombi yale ya kumuvurumusha shetani hata kama yuko nyuma ya mtungi lazima asepe hilo sikujali mtoto kaja mwenyewe nikampa haki yake na maombi ya baraka juu yangu.
Sikuile ikapita nikaja kuhama pale baada ya siku kama 3 hivi nikahama ule mtaa sababu ya ile inshu. Maana mimi mwenyewe kibinafsi sikuona kama ilikuwa sahihi ilikupisha mkasa ule nikahamia mtaa mmoja unaitwa zamzam karibu na sanamu la mashujaa la Mayunga.
Baada ya kuhama pale mtaa wa matopeni nikaenda mtaa wa Mayunga mtaa mmoja unaitwa Uswahilini, nimekaa pale kwa muda kidogo sakata lingine likaja niliyempa mimba Misungwi, anataka mahitaji ili muda wa kujifungua ukifika awe na mahitaji yake muhimu kama mzazi nikipiga hesabu hapo hata hela ya kula mimi mwenyewe sijui naitoa wapi biashara imebuma kila nachoona hakikamatiki, nikapata wazo nikamwambia mjomba kijijini aniuzie mbuzi zangu niweze kusave hii inshu ajifungue salama baada ya hapo ndio ntaangalia utaratibu mwingine.
mbuzi zikakosa soko mpaka anajifungua hakuna hela nimetuma ikafikia hatua nikawa namwambia mama mkwe ninaumwa hivyo nimelazwa hii nikukwepa majukumu ya mke na kiumbe kilichokuja duniani ila sikuwa na namna sema ilinibidi nifanye hivyo maana message nilizokuwa napokea kwa siku na kila saa ni siri yangu mke anatuma message kama anatoa hosia wa mwisho kwamba muda wowote hatunae ikabidi nitumie njia hii kupona kwanza kwa muda ili baadae tuendelee na mengine sikufanya haya kwa kutaka bali biashara yangu haikuwa sawa mimi mwenyewe hata kula yangu shida muda mwingine nalala njaa mpaka nikavimba mashavu miguu kisa nilitumia mlo mmoja yaani dagaa nilizila karibu mwaka hii ni kwa sababu niliamua nisave bajeti ili nisitumie hela ya mtaji ila nilichovuna baadae ni kuugua tena.
tuachane na hilo baadae nikapata mteja wa mbuzi nikauza nikamtumia maana hii inshu nilitaka nisimwambie yeyote kuwa ninamtu nimezaanae iwe siri yangu siku mtoto akikua ndio nimtambulishe nyumbani wamjue ikawa imeshindikana hilo wazo langu nikaumbuka.
baadavya kufika nyumbani huyo binti amekaa pale home mwaka mzima sina mpango nae nayeye kakomaa tu yaani hana hata mpango wakusema hapa nimepata nafuu ngoja nirudi kwetu hamna mama nae anasema huyu ndio wakuoa sasa nimempima katika vipimo vyangu kila kipima kwa huyu binti naona anakufaa usije ukamuacha hapo sasa najisemea hapa sasa nimepeleka mtego home moja kwa moja nimelipukiwa sina bahati sasa ngoja nisikilizie itakuwaje.
mwaka ukaisha miezi sita ikapita hajaondoka tu duuh ikabidi nimuite sasa aje Bukoba tuishi sina namna mama nae anasema nilikuwa naangalia utachukua maamuzi gani ndio maana nimekaa kimya ili nione unafanya maamuzi yapi hatimae umefanya maamuzi sahihi.
Tumeishi Bukoba muda huo nilikuwa na yule mwingine wa kufumaniwa na kaka yake ikabidi huyu wa kufumaniwa nimuache niendelee na mke sasa ambae nimeona bora nifanye maamuzi ndio nikafanya maamuzi na niliezaa nae.
Wakufunaniwa akawa anataka kuja nilipohamia, sikuwahi mwambia naishi wapi toka nimetoka pele kwao na nilipokuwa kazini alikuwa kweli anapajua ila kumleta nilipoiwa nikiishi ilikuwa haiwezekani bora nimpeleke Gesti kuliko geto nilifanya hivyo muda wote.
siku moja bwana mke akadaka message sijui nilipitiwaje bila kufuta na kublok namba maana nilikuwa na mtindo nikifika home nablok namba yake natulia kama siyo mimi siku moja nimekaa zangu nimetoka kazini nimejichokea nakutana na ugeni umekaa ndani kuchungulia ni yule demu wa kufumaniwa wamekaa na mke wanapiga stori nilitaka kurudi nilikotoka ila nikajikaza kiume nikazama ndani daah hii ilikuwa soo na nusu ila nilikaza kama mwaname nikalimaliza hilo hapo ndani palipo sasa stori naijua ilikuwaje.
Muda huo demu wa fumanizi anamimba yangu huyu kamuita kuthibitisha maana waliongea yote kwenye simu akamwambia namimba ya Jumanne huyu ili athibitishe akamuita wajuane.
Baada ya hili soo nikajua bwana watagombana au wataniacha wote na chakushangaza wote wawili waliendelea kunijali kama mwanzo mpaka nikawa nasema hapa huenda nategwa nikawa sitabiliki nikiona ukalimu imezidi nabadilika kama tumegimbana.
Nifupishe stori yule demu wa fumanizi alijifungua hospital ya Kagera Sugar ila bahati haikuwa kwetu mtoto alifariki baada tu y kujifungua kilichopelekea mtoto kufariki ni madokta walikuwa wanafunzi hivyo baada ya kuona njia ni mdogo wao wakalazimisha asukume hivyo hivyo matokeo yake mtoto katoka amechoka hakumaliza masaa akafariki hivyo tukawa nikawa nimepoteza mtoto kwa njia hiyo siyo kwamba nilikuwa sihudumii hapana nilikuwa nahudumia ila baada ya kukosa mtoto nikakata mawasiliano.
2023 kaka yake akamuita mdogo wake wakumfumania akamwambia mwambie Jumanne anisamehe huenda mimi ndio nilichangia yeye kufanya maamuzi mengine mpaka sasa hujaolewa hivyo kama unanamba yake nipe nimpigie, kaka yake alikuwa anaumwa hivyo katika kauli za mwisho alisema mwambie Jumanne nimemsamehe na yeye kama kunasehemu nilimkosea anisamehe.
hazikupita siku baada ya kusema hayo mwezi wa 9/2023 alifariki kaka yake mfumaniwaji natumia hilo neno siyo kwamba ni zuri hapana naweka ili kuweka stori uelewe anayezungumziwa ni nani kati ya hao wawili.
Mpaka leo hii yule demu wa kufumaniwa ananioenda ila mimi simkubali hata ila ndio hivyo, hata muda huu nikimwambia njoo anakuja chap na haraka.
ukiachilia mbali mke nae niko nae mpaka sasa tuko na watoto 3 na tumejenga, huu mkasa nikaona nisiishi nao labda nanyie mmepitia zaidi yangu ila stori ndio hiyo