MINOCYCLINE
JF-Expert Member
- Apr 2, 2015
- 8,018
- 16,802
1. Bado Simba SC yetu haichezi Mpira wa Kuvutia na pia watuambie kwanini Kipa mzuri, mzoefu na makini namba Mbili Beno Kakolanya haonekani na badala yake mbadala wake anakuwa Kipa Kinda ambaye Mightier simkubali na simuamini pia Ally Salim?
2. Simba SC yetu upande wa Stamina hatuko 100% Fit.
3. Tatizo la Mabeki Kutegeana hasa katika Kukaba bado ni tatizo.
4. Mipira ya Juu ( hasa Cross ) bado Mabeki wetu hawaichezi vizuri ingawaje kidogo tatizo linaanza Kupungua.
5. Lile tatizo la Wachezaji wa Simba SC kuanza Kubweteka hasa Timu ikiwa inaongoza bado halijafanyiwa Kazi.
6. Washambuliaji wa Simba SC waache Uchoyo na waambiwe kuwa Muhimu Kwanza ni Ushindi na siyo nani amefunga.
7. Baada ya kuwaona Asec Mimosa FC tuliowafunga Goli 3 kwa 1 ( ambazo Mightier nilizitabiri mapema tu hapa JamiiForums ) na Kuiona Mechi ya Gendamarie FC na Berkane FC ambapo Berkane FC alishinda Goli 5 kwa 3 nashauri kwa Mechi zote za Ugenini ( away ) Mkakati wetu Mkuu uwe ni Kucheza pure Defensive na kufanya Interval Counter Attacks, ila kwa Mechi za hapa Nyumbani Mkakati uwe ni 100% Kushambulia.
8. Kwa Mechi tunazohitaji Ushindi ( hasa za Nyumbani ) Kiungo Saido Kanoute awe anacheza na Mkude na Wachezaji Pape Ousmane Sakho na Bernard Morrison wawe Wanaanza ili tupate Ushindi wa haraka ila kwa Mechi za Ugenini ( away ) nashauri Thadeo Lwanga na Muzamiru Yasin wawe Wanaanza wakisaidiwa na Mkude Dimba la Chini.
9. Tunaomba Mshambuliaji Kibu Denis atibiwe haraka kwani kama akiwa Fit ndiyo Turufu yetu Kubwa hasa hasa katika Mechi za Ugenini ( Away ) kwani ana Uwezo mkubwa wa Kupambana, Kusumbua Mabeki na hata kuwafanya Wasipande Kushambulia kwa Kumuogopa kitu ambacho kitakuwa ni Faida Kwetu Kimchezo.
10. Beki Mkongo Henock Inonga aambiwe Ukweli kuwa japo ni mzuri Kiuchezaji, ana Kipaji Kikubwa na ni Msaada mkubwa katika Kuzuia na Kuanzisha Mashambulizi ila apunguze Sifa za Majukwaa, Kudekadeka, kutaka attention kila mara na Kujiamini kulikopitiliza kwani anatugharimu na atatugharimu zaidi huko mbeleni asipojirekebisha.
11. Wachezaji wa Simba SC waambiwe Ukweli kuwa Mashindano haya ni Magumu, yana Ushindani mkubwa, bado Safari ni ndefu tena kuliko wanavyofikiria, waache Utoto na ule Ushindi wa Juzi dhidi ya Asec Mimosa FC uwaimarishe tu lakini usiwafanye waone kuwa ndiyo wamemaliza au wanajua sana kuliko Wenzao walionao katika Kundi lao.
Yangu ni haya tu na mengineyo naomba niwaachie na wana Simba SC Wenzangu hapa JamiiForums wayaseme ( wachangie ) kwa Maslahi mapana ya Timu yetu na ningetamani sana hata Viongozi wa Simba SC ( hadi wale wa Bodi akina CEO Barbara Gonzalez, Mangungu na Magori ) wausome huu Uzi pamoja na Msemaji Wetu Ahmed Ally na Benchi la Ufundi ili yale tuyasemayo hapa wayapokee na wakiona yanawafaa wayafanyie Kazi.