Baada ya kugundua ana mimba isiyo yangu, nipo katika wakati mgumu sana. Nishaurini

Baada ya kugundua ana mimba isiyo yangu, nipo katika wakati mgumu sana. Nishaurini

Wanaume wenzangu tujifunze njia za kidiplomasia kuwaacha hawa wanawake pasipo kuwaumizi kimwili maaana kumkatili kiasi hicho utakuja kupambana na mkono wa sheria. Unamwacha tuuu dhambi yake imtafune...
sure
 
Habari zenu wakuu, Jf ni sehem nayoiheshimu na imejaa watu wazima wenye hekima na wanaojitambua natumaini mtanipa ushauri mzuri na wenye hekima.

Nipo kwenye mahusiano na binti 24 years old, Tumekuwa na mahusiano kwa mda wa miaka miwili na mda wote nilikuwa nikijitahidi sana kumlinda na mimba sababu yupo kwao mipango yetu ilikuwa ni kuzalia kwenye ndoa hivyo mda wote tuliokuwa tunakutana nilizingatia sana kinga ili kumlinda na mimba.

Sasa shida imekuja tokea miezi miwili iliyopita alikuwa kabadilika sana yani hata kukutana na mimi ni hadi aamue kwa kujiskia yeye tofauti na zamani, akija kwangu simu ataiacha kwao sababu hatuishi mbali na simu nilimnunulia mimi, hadi nikajiuliza simu imeficha nini lakini niliendelea kuwa mvumilivu.

Mara ya mwisho nikakutana nae kimwili siku moja baada ya kumaliza period na siku ya 27 ya mzunguko wa hedhi ndio ikawa mara ya mwisho kusex nae na mara zote nilitumia condom kwa usahihi na wala haikupasuka wala kupata damage yoyote,na hata mda wa kusex alikuwa yupo yupo tu yani najihisi nipo peke yangu kitandani.

Sasa baada ya kupita siku karibia 36 bila kuona siku zake, ikabidi nimuulize vipi kuna tatizo, akawa kakaa kimya tu anasema hajielewi labda ni mabadiliko tu, kwa vile nilishaona ile sio hali ya kawaida na haijawahi kutokea ikanibidi niende pharmacy nikanunua Baby check, kwa ajili ya kupima mkojo wake ili nijue kama ana ujauzito

Jioni nikampa nikamuekekeza acheki mkojo wa asubuhi akiamka, ilpofika asubuhi akachek na matokeo yakawa ni haya [emoji116], akanitumia hiyo picha whatsap

View attachment 1500024

Alama mbili zikatiki kuwa ni mjamzito, ikanibidi nionane nae jioni ile tujadiliane na maswali nliyokuwa nayo kichwani inawezekana vipi mtu usex kwa kutumia condom kwa usahihi na tena kwenye siku ambazo sio za kushika mimba na mtu apate mimba?

Nilivyoonana nae ikanibidi nimbane kisawa sawa kwa tecknic nazozijua mimi ili aseme ukweli kama aliteleza, baada ya kumbana huku akilia kuwa mimba ni yangu nikamwambia pia kama bado utaniaminisha mimba ni yangu mimi sina tatizo mtoto akizaliwa tutaenda kucheki DNA, kuthibitisha kuwa ni wangu ili nilee damu yangu, Akasema hataki kuzaa hivyo tuitoe, mimi nikasimamia msimamo wangu kuwa damu yetu haipotei kama mimba ni yangu ajiamini kwanini aogope hadi atake kuitoa na uwezo wa kulea upo.

Ikabidi aongee ukweli kuwa alinisaliti na mtu mwenyewe aliyechepuka nae haijui hata background yake hata kazi anazofanya hazijui, niliishiwa nguvu pale nilipo mwambia alete simu yake ampigie huyo jamaa kuwa ana mimba yake

Baada ya kumpigia jamaa akakubali na kusema hana tatizo , nilibaki na mshangao na machozi yalinitoka, na kama isingekuwa kutumia condom basi ile mimba ilikuwa niikubali kwa mikono miwili na ukiangalia kwetu kutoa mimba ni haram na kosa kubwa wakati uwezo wa kulea upo

Pale ndipo nilipoamini kuwa wanawake ni watu wakuishi nao kwa akili sana, kukuletea mtoto asie wako hawaoni kazi, naamini kuna watu wengi mnalea watoto ambao sio wenu, mimi nimeponyea kwenye tundu la sindano

nichukue fursa hii kuwashauri vijana ambao hamko kwenye ndoa acheni kuruka na wanawake kavu kavu, hasa hawa mabinti under 28, hawafai hata kidogo ni wachache sana wametulia ila wengi ni mafia, kukuleta mimba isiyo yako huwa hawaoni tabu

Ni heri mtumie condom tu ili kuepukana na huu mchezo tunaochezewa wanaume, ifike mahali tuseme basi kulea watoto ambao sio wetu tumechoka

Vile vile tokea hili tukio litokee nipo katika wakati mgumu sana, mawazo hayaniishi sababu kutendewa unyama kama huu na mtu niliyempenda inaumiza sana, na huyu mwanamke kila kukicha ananiomba msamaha akilia, hivi nawezaje kusamehe usaliti kama huu? ndio maana kwenye heding nikaomba ushauri wenu namna ya kuanza maisha mapya yenye amani nimechanganyikiwa kwa kweli
Pole kiongozi,,

Ibada hapo ndo suluhisho,,
 
Pole sana Mkuu kama si kutumia kinga ungebambikiwa mimba labda ungegundua kwenye DNA au ungelea kama wako.
 
Muage mwambie maisha mema wanataka wapo wengi japo wiki za kwanza utaumia ila baada ya mwezi utakuwa sawa na maisha yatasonga
 
Mshukuru Mungu umejua ukweli ila ni kitu ambacho unaweza recover na kuendelea na maisha. Imagine ingekuwa kakupa gonjwa lenyewe, ni irreversible!
huyo achana nae, ila pia umejifunza kitu! Cheza kwa akili na tafuta mke kwa akili zaidi...
 
Kaka nimechoka, anayenicheka aje anicheke lakini yanaweza yakamkuta hata walio kwenye ndoa kuweni makini na wake zenu

Sio "yanaweza kuwakuta" yamewakuta wengi sana, wengi hawajui kuwa wanalea watoto wa wanaume wenzao.

Mbaya zaidi wake wao wanajua ila wanawacheck tu kwa dharau huku wakiwakamua kwa kuwalea watoto wa vidume wengine
 
Mkuu bado unamwita mpenzi!? Aisee.
Nikihisi tu umeacheat, huwa sisubiri maelezo, tunaachana hewani.
Cheating is a choice, not a mistake
sure kaka nimeumia sana
 
Muage mwambie maisha mema wanataka wapo wengi japo wiki za kwanza utaumia ila baada ya mwezi utakuwa sawa na maisha yatasonga
Asante sana kaka chozi linafutika familia yangu ya jf, mungu awalinde
 
Pole sana mkuu, yalishanikuta nikalea kwa taabu sana hali haikuwa nzuri kipindi hicho, mtoto mpaka kafika miaka minne nkagundua si wangu kutokana na mambo fulani niliyohisi na binti akakubali kweli mtoto si wangu.

Niliumia sana lakini hakukuwa na jinsi, muhimu endelea na maisha yako muhimu umejifunza. Wanawake muda fulani si wa kuwaamini sana 100% .
Mkuu huo msala uliumalizaje?
 
Back
Top Bottom