Baada ya kuhutubia Bunge la Angola, Rais Samia atatembelea kiwanda kikubwa cha mafuta nchini humo

Mindyou

JF-Expert Member
Joined
Sep 2, 2024
Posts
2,536
Reaction score
7,194
Rais Samia leo Aprili 9, 2025, anatarajiwa kutembelea kiwanda kikubwa cha kusafisha mafuta cha Luanda Oil Refinery ikiwa ni siku ya tatu na ya mwisho ya ziara yake ya kikazi nchini Angola.

Ziara hiyo inaweka alama muhimu ya kihistoria, kwani ni mara ya kwanza kwa Rais wa Tanzania kutembelea rasmi Angola tangu mwaka 2006. Kabla ya hapo, Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere, ndiye aliyekuwa kiongozi wa kwanza wa Tanzania kufanya ziara ya Kiserikali nchini humo.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais – Ikulu, Sharifa Nyanga, lengo la kutembelea kiwanda hicho ni kujifunza na kubadilishana uzoefu kuhusu usimamizi na maendeleo ya sekta ya mafuta na gesi, hasa kwa kuzingatia kuwa Tanzania ina hifadhi kubwa ya gesi, huku Angola ikiwa ya pili barani Afrika kwa hifadhi ya mafuta.

"Akiwa kiwandani, Mheshimiwa Rais Samia atapokelewa na Waziri wa Madini wa Angola, Mhe. Diamantino Pedro Azevedo, ambapo watajadili fursa za ushirikiano katika sekta ya mafuta na gesi, pamoja na namna ya kukuza uwezo wa kitaalamu katika nyanja hizo," alisema Nyanga.

Rais Samia yuko Angola kwa mwaliko wa Spika wa Bunge la Angola, Carolina Cerqueira, ambaye pia ni mwanamke, na jana alimpokea kwa heshima kubwa Bungeni. Samia ameweka historia kwa kuwa Rais wa kwanza Mwanamke kutoka Afrika kulihutubia Bunge hilo.

samia angola.png

Ziara hii inaleta kumbukumbu ya mahusiano ya muda mrefu kati ya Tanzania na Angola na inaonesha dhamira ya serikali ya awamu ya sita kuimarisha diplomasia ya kiuchumi kupitia ushirikiano wa kimataifa, hasa katika sekta muhimu kama mafuta na gesi.

Source: Nipashe
 
Wanatembelea Angola kuona refinery wakati hapa nyumbani mradi wetu wa kiwanda cha LNG umekwama mwaka wa 10+ saivi eti wanafanya majadiliano.

Wenzenu wanasema na kufanya nyie mmekalia maneno na siasa tu. Alafu eti mnaenda kutembelea nchi nyingine muone wanavyofanya!! Matumizi mabaya tu ya kodi za Wananchi.

CCM ni laana kwa Taifa hili.
 
Huyu mzanzibari mwanamke katumia lugha gani kuhutubia huko nchi za watu?
 
Rais Samia leo Aprili 9, 2025, anatarajiwa kutembelea kiwanda kikubwa cha kusafisha mafuta cha Luanda Oil Refinery ikiwa ni siku ya tatu na ya mwisho ya ziara yake ya kikazi nchini Angola.

Ziara hiyo inaweka alama muhimu ya kihistoria, kwani ni mara ya kwanza kwa Rais wa Tanzania kutembelea rasmi Angola tangu mwaka 2006. Kabla ya hapo, Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere, ndiye aliyekuwa kiongozi wa kwanza wa Tanzania kufanya ziara ya Kiserikali nchini humo.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais – Ikulu, Sharifa Nyanga, lengo la kutembelea kiwanda hicho ni kujifunza na kubadilishana uzoefu kuhusu usimamizi na maendeleo ya sekta ya mafuta na gesi, hasa kwa kuzingatia kuwa Tanzania ina hifadhi kubwa ya gesi, huku Angola ikiwa ya pili barani Afrika kwa hifadhi ya mafuta.

"Akiwa kiwandani, Mheshimiwa Rais Samia atapokelewa na Waziri wa Madini wa Angola, Mhe. Diamantino Pedro Azevedo, ambapo watajadili fursa za ushirikiano katika sekta ya mafuta na gesi, pamoja na namna ya kukuza uwezo wa kitaalamu katika nyanja hizo," alisema Nyanga.

Rais Samia yuko Angola kwa mwaliko wa Spika wa Bunge la Angola, Carolina Cerqueira, ambaye pia ni mwanamke, na jana alimpokea kwa heshima kubwa Bungeni. Samia ameweka historia kwa kuwa Rais wa kwanza Mwanamke kutoka Afrika kulihutubia Bunge hilo.

Ziara hii inaleta kumbukumbu ya mahusiano ya muda mrefu kati ya Tanzania na Angola na inaonesha dhamira ya serikali ya awamu ya sita kuimarisha diplomasia ya kiuchumi kupitia ushirikiano wa kimataifa, hasa katika sekta muhimu kama mafuta na gesi.

Source: Nipashe
Rais wa mchongo hatumtaki
 
Back
Top Bottom