baada ya kujifungua

aisherjs

Member
Joined
Aug 19, 2013
Posts
28
Reaction score
7
Swali langu ni kwamba baada ya mama kujifungua hutokwa na damu ya uzazi kwa muda wa siku ngapi?

Na je anapomaliza damu ya uzazi anaanza mzunguko wake wa hedhi ama hukaa muda gan kabla mzunguko wa hedhi haujaanza
 
Ngoja waje wataalamu. Ila ntakujibu kwa experience tu. Kuna wengine baada ya kujifungua huona siku zao kwa siku 7 hadi mwezi ila hutoka kidogo kidogo sana. For my case mzunguko mwingine huja baada ya miezi 10. Note maumbile na mazingira yako tofauti.
 
Binafsi ilikaa almost wiki tatu hivi.na baada ya hapo mzunguko ulianza baada ya miez minne
 
Ni kweli tunatofautiana binadam, mamaangu ye alisema hukaa miaka miwili ndo huanza kupata hedhi tena baada ya kujifungua. But mi hubleeb kidogokidogo kwa wiki tano au sita then baada ya miezi sita huanza mzunguko. Nafkiri wataalam wapo watufafanulie hili
 
Swali langu ni kwamba baada ya mama kujifungua hutokwa na damu ya uzazi kwa muda wa siku ngapi? Na je anapomaliza damu ya uzazi anaanza mzunguko wake wa hedhi ama hukaa muda gan kabla mzunguko wa hedhi haujaanza

inategemea na mtu,mfano mimi baada ya kujifungua nilitokwa na damu something like one week or more ila haikuzidi siku kumi na damu yenyewe haikua nyiiiingi sana,na mwezi uliofuata nilianza mzunguko tena katika tarehe zilezile ambazo nilikua napata mzunguko kabla ya kupata ujauzito na mpaka sasa naendelea na mzunguko kawaida
 
Hii nadhani haina formula na pia nad
hani kutoka nyingi au kidogo huchangiwa na vitu gani unakula baada ya kujifungua. Mm mama yangu pia alishangazwa na mm mana yy ilikuwa ikitoka kama mwezi tangu akijifungua na hukaa miaka miwili na kitu ndo circle ya kawaida hurudi tena. Ila kwangu ilikuwa napata ile damu ua kujifungua wiki mbili na mwezi unaofuata ratiba ya hedhi ule mzunguko wa kawaida unaanza. Nadhani maumbile ya mtu na mtu
yanahusika. Biology sijui inatakaje hapo...
 
wiki mbili mpaka mwezi kulinga na mambo ya "nature & nurture" kwa sana .
 
Kwa hiyo huo muda ambao mzunguko wa hedhi unakua haujaanza inamaanisha kuna kuwa hakuna yai linalokua limepevuka na kushuka ktk nyumba ya uzazi dat means hakuna uwezekano wa mama kushika mimba tena katika kipindi hicho?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…