Baada ya kukataliwa na wananchi, CHADEMA wanajigeuza mgambo

Baada ya kukataliwa na wananchi, CHADEMA wanajigeuza mgambo

Wakudadavuwa

JF-Expert Member
Joined
Feb 17, 2016
Posts
17,506
Reaction score
16,003
Ndugu zangu,

Ni dhahiri sasa Chadema wamefikia hatua ya kujigeuza migambo. Wanataka kila wasemalo au watakalo lifanyike.

Wanajiona wao ndio wanastahili "attention" ya wananchi. Rais Samia anajitahidi kukutana na makundi muhimu katika jamii kama vile wazee, wakinamama, vijana, viongozi wa dini nk. Chadena wanataka wasikilizwe wao.

Kwenye baadhi ya nchi hapa barani Afrika kama vile Uganda, Somalia na Nigeria kuna vikundi vya migambo mwanzo vilijidai vyama vya siasa lakini baadae wakafikia malengo yao ya siasa za uasi.

Yaani Rais aache kufanya vipaumbele vyake ajikite kusikiliza kikundi chenye maslahi binafsi. Kwa kauli wanazotoa na vitisho mitandaoni na mikutanoni ni dhahiri sasa wamulikwe, wadhibitiwe mapema kabla hawajakomaa.

Siasa safi ni muhimu kwa mustakabali wa Taifa letu.
 
Wananchi hawakupiga KURA ndio Maana Muda wote SPIKA anawaambia Wabunge Wamshukuru MAGUFULI kuwachangua Acha kupotosha UMMA Mwaka 2020 HAKUKUWA NA UCHAGUZI Bali Kulikuwa na UTEUZI
 
CHADEMA inazungumzwa kuliko chama kingine chote, kina trend kwa kasi kubwa
 
Ndugu,
Siasa safi haziwezi kuletwa kupitia Katiba ya 1977 inayotoa mianya ya ukandamizaji wa haki
 
Waa tuuu kwasababu siku unajiunga hukutuambia mkuuu.
Ulijiunga kimyakimya saa ya kutoka unataka kututangazia.
Pili hilo unalifanya kwenye nafsi yakoo .
And fanya kile kinachokupa Amani mkuu Moyoni mwako.

Sisi CCM huwa tunawaangalia tuuu
 
Back
Top Bottom