Akizungumza nami muda mfupi uliopita Waziri Ngeleja amesema kuwa matatizo kama haya huwa yanaweza kutokea na kwa vile ni ya kiufundi zaidi basi yanahitaji umakini wa hali ya juu kuyatatua na amewahakikishia wananchi kuwa juhudi zote zinafanywa ili kurejesha hali katika hali ya kawaida.
Siasa mara nyingine kweli inachekesha,nina mfano,yani say unampa mtoto kitu flani,halafu baadaye anadai kipya,ukamnyang'anya ulichompa hapo awali,halafu ukamrudishia na kumwaminisha kwamba ni kipya,na mtoto huyo kuruka ruka kwa furaha kama vile kweli ni kipya,kufurahia ama kutokufurahia kwa mtoto huyo kunategemea na umri halisi na level ya uelewa wake. Pia kwa mtoto huyo,jingine ni inategemea na matumizi na umuhimu wa alichonyang'anywa mtoto huyo bila kujali umri na uelewa wake,matumizi ya alichorudishiwa yanaweza kumsahaulisha kudai kile kipya,anaweza kujiridhisha kwamba ni kipya huku akifahamu kabisa kwamba sivyo....Furaha ya kurudishiwa kile alichonyang'anywa ni sawa na furaha ya kupata kipya.
Mfano huo hapo juu ni sawa kabisa na situation iliyotokea,say ccm wanataka kutumia hilo kama karata ya kwamba wana fix matatizo ya wananchi,wale wananchi wenye umeme hawawezi kujua hilo kama wasipokatiwa umeme...Wote tunajuwa adha ya kukosa umeme bongo,umeme ukirudi kusema kweli mnashangilia,halafu ukiwasha tv unasikia waziri anasema tumejitahidi na tatizo lilikuwa hili nk,hapo kimantiki unajikuta umeishangilia serikali kama vile mtoto aliyepata cha zamani na kudhani ni kipya simply kwasababu furaha ya kukipata kile alichonyang'anywa mwanzoni ni sawa na furaha ya madai mapya ya mwananchi,ie kuhusu gharama za umeme nk.
Inategemea na level ya uelewa wa wabongo,wanaweza wakaichagua ccm tena kwa furaha za kurudishiwa umeme ambao walikuwa nao hapo awali lakini wakanyang'anywa kwasababu tu walikuwa na madai mapya ie gharama za umeme,na kwamba serikali ya ccm haifanyi kazi zaidi ya ufisadi.
Kwa kifupi wadanganyika mnabipiwa,mtakoma kuringa,si mnadai wengine wanakimbia nchi,ooh wanabeba mabox,kwanini msifix hayo matatizo?Kama mnaamini mtayafix kwa stlye ya uongozi tulio nao basi mtakaa maana mnapiga debe ooh ccm nambari wani blah blah.