Bado naukumbuka usiku ule vizuri, nilikuwa nimekaa nikifunikwa na giza nene wakati mshumaa mwembamba ukimulika mwanga mdogo. Muda huo nilijaribu kumaliza chakula kilichopo kwenye sahani yangu nikiomba kimoyomoyo umeme urudi. Akili yangu ikachangamka na nikawatazama baba na mama waliopo mbele yangu. Kwa kuwa ilikuwa giza, sikuweza ona nyusa zao vizuri hivyo nikapata ujasiri wa kuwauliza swali lililonisumbua kwa muda mrefu.
‘Mama, Baba, naomba mninunulie simu’
Kimya kikatawala, wadogo zangu walinipiga jicho wakishangaa ushujaa wangu. Kicheko cha mama cha ghafla kikafunika ukimya ule na kisha akajibu, ‘Mmh, we bado mdogo’. Hapo ndipo nilipoanzisha mdahalo juu ya mimi kupata simu na kwa mara ya kwanza wazazi wangu walishuhudia nikiongea kwa ujasiri. Niliamini ya kuwa ninayo haki kuwa na simu kama rafiki zangu wa kidato cha pili.
Nilijua kwamba bila simu, ninapitwa sana katika kuchangia mada pamoja na wenzangu wenye simu. Kutokuwa na simu ni kama kuishi kwenye puto au kidunia changu mwenyewe. Lakini wenye hela wakakataa, wazazi wakaamua kuwa mimi bado ni mdogo kutumia simu. Kiukweli hawakukosea.
Miaka miwili baada ya kulilia simu, nikiwa nimehitimu kidato cha nne, wazazi wakaninunulia simu aina ya TECNO F1. Nilifurahi sana kwa kuwa sasa ninauwezo wa kujiunga na makundi ya WhatsApp, kuperuzi Instagram, na kuangalia video za Youtube. Pia nilifurahi kwa kuwa nitatumia simu kadri ya mapenzi yangu bila kutegea simu za wazazi kama zamani. Wahenga wanasema ukipenda boga, penda na ua lake lakini ahh wapi! Nilipenda kuwa na simu lakini sikupenda changamoto zilizombatana na simu.
Kwa mfano kununua vifurushi mara kwa mara hususani nikiwa sina pesa. Tatizo lingine ni pale mama anapokasirika akigundua natumia Tiktok au naperuzi mtandaoni siku nzima bila kujishughulisha na kazi za nyumbani. Na hata macho yalipoanza kuuma na nikawa nachelewa kulala, nilijikuta siachi kutumia simu.
Lakini changamoto kubwa zaidi ilikuwa pale niliposhuhudia kwa macho yangu picha za utupu za wasichana ninaowajua na wengine wa rika yangu. Picha hizi zilisambazwa kwenye makundi ya WhatsApp kisa wasichana hao wameachana wachumba wao vibaya. Nilisononeka sana kwasababu aibu hii kwa wasichana hao itadumu mtandaoni milele.
Pia, nilishuhudia uonevu wa kimtandao (au cyber bullying) pale baadhi ya wenzangu walitukanwa, kusemwa au kuonewa mitandaoni hususani wakituma picha zao Instagram. Juu ya yote, maendeleo katika simu yamewawezesha watu wenye nia mbaya kuiba pesa kwa kuwadanganya watu. Loh! Hakika simu ni chombo chenye nguvu.
Kiukweli sikutarajia kushuhudia uovu wote huu baada ya kutumia simu. Nikajiuliza, je, ninasimama wapi katika matumizi ya simu na mitandao ya kijamii kiujumla? Vilevile, jamii na serikali inasimama wapi katika maendeleo haya ya sayansi na teknolojia kupitia simu na mitandao ya kijamii?
Kwa kujibu swali langu la kwanza, niliamini kuwa mbegu ya mabadiliko hupandwa na kukua moyoni mwa mtu kwanza. Kwahiyo mabadiliko ya jinsi na kiasi cha muda wa matumizi ya simu yangu yalianza na mimi. Ndipo nilitumia Youtube kujifunza jinsi ya kutengeneza kacha na mikufu ya shanga. Licha ya ugumu wa kujifunza, nilijikuta nikijawa na furaha pale, kwa mara ya kwanza, nilimtengenezea mama kacha nyeupe na akaipenda sana. Nikabana matumizi na kukusanya elfu kumi kama mtaji wa kununua shanga na uzi ili nitengeneze kacha.
Nilitumia ubunifu huu wa kutengeneza kacha za aina mbalimbali ili kuziuza kwa wanafunzi wenzangu. Ilinilazimu kutuma picha za kacha nilizotengeneza kwenye WhatsApp ili niweze kuwaonyesha na kuwafikia watu wengi zaidi. Nilitumia faida niliyopata kuendeleza biashara yangu ya kacha na kuokoa uchumi wangu kwa kukidhi baadhi ya mahitaji yangu ya muhimu.
Pia, nilipokuwa na kifurushi cha kutosha nilitafuta video za kujifunza kusuka nywele za mabutu au njia tatu za knotless. Baada ya kujifunza, nikaweza kujisuka mwenyewe na Bibi yangu hapa nyumbani. Mungu akiniwezesha nitaanza kuwasuka watu wengine na hatimaye kuanzisha saluni ndogo. Niligundua kwamba uamuzi wa kutazama video Youtube waweza kuwa daraja la kubadilisha hali ya uchumi ya mtu hata kwa kiasi kidogo ili kuleta maendeleo.
Kwa kujibu swali langu la pili juu ya nafasi ya jamii katika maendeleo ya sayansi na teknolojia hususani kupitia simu na mitandao ya kijamii, ni kweli kwamba maamuzi ya matumizi ya simu ni juu ya mwenye simu ila hatuna budi kuwa wasamaria wema hata mitandaoni. Tunaweza kutumia simu zetu kukemea na hata kuwachukulia hatua za kisheria wanaofanya uovu kama wizi na uonevu wa kimtandao. Kwa kuwa leo uovu huu waweza kumtokea mtu usiyemjua lakini kesho ukamkuta mtu unayemjua na kumjali.
Vilevile, serikali inayo nafasi ya muhimu katika maendeleo haya. Ilikuwa ni wiki mbili zilizopita, ndani ya joto kali la Dar es Salaam, nilipokuwa katika foleni ndefu sana kwenye mstari wa uhamiaji nikisubiri kuhudumiwa ili niende kwenye dirisha la nida kwa ajili ya kusajiliwa namba ya nida.
Namshukuru Mungu niliweza kuhudumiwa siku hiyo licha ya kukuta foleni ndefu. Ila baadhi ya wenzangu hawakubahatika kirahisi kwani mara nyingine walikuta ofisi za nida zimekosa umeme au pakiwa na umeme waliambiwa waende ofisi za eneo lengine ili wahudumiwe. Changamoto hii ilikula nauli na muda wao.
Ili kuweza kukabiriana na changamoto hii, serikali yaweza kuanzisha tovuti ya usajili wa nida. Hivyo basi, watu wataweza kuambatanisha nakala muhimu za kushughulikia nida kama vile vyeti vya kuzaliwa, picha maalumu na vitambulisho husika kwenye tovuti hiyo. Mfumo huu wa usajili wa nida mtandaoni utapunguza foleni katika ofisi za nida na vilevile kuwasaidia watu kupata huduma ya nida pale ambapo ofisi za nida zinakosa umeme au zikiwa mbali sana. Tovuti itawezesha kipaumbele kutolewa kwa wale watakaofika katika ofisi za nida kwani foleni imeshapunguzwa mtandaoni. Pia, huduma hii itafungua milango ya ajira kwa watengenezaji tovuti yaani web designers.
Changamoto inakuja wakati watu watahitaji kutia saini na kuweka alama za vidole. Hivyo basi, serikali inaweza kuwekeza katika tovuti inayoweza kusoma alama za vidole au serikali inaweza kuwekeza katika wakala mbalimbali kama wale wa kusajili laini za simu kwenye serikali za mitaa ili watu waende kutia saini na kuweka alama za vidole baada ya kujaza fomu za nida mtandaoni.
Kisha watu watahitajika kwenda kwenye ofisi husika za nida ili kuchukua kadi za nida kirahisi baada ya muda husika. Nimetambua kuwa maendeleo haya ya sayansi na teknolojia kupitia simu yameweka nguvu na dunia nzima katika viganja vyetu, na hivyo tunauwezo wa kujenga jamii na hata uchumi lakini je, maendeleo haya yamekusaidiaje wewe?

Upvote
3