Baada ya kuliona jengo la Yanga FC, nimeanza kuamini uchawi upo

FRANCIS DA DON

JF-Expert Member
Joined
Sep 4, 2013
Posts
38,920
Reaction score
44,970
Kama si uchawi sijui itakuwa nini, ukiambiwa lile jengo lililojaa ukungu mweusi wa fungus kama kuta za choo cha Tandale kwa mfuga mbwa ni jengo la klabu kubwa zaidi barani Afrika na Tanzania unaweza usiamini.
Sasa mimi nitoe way forward badala ya kuishia kulalamika tu. Wafanye fascadal upgrading kwa kutumia material mbadala kama 'alluminum-plastic composite boards' na 'glass glazing sheets', hizi hata miaka mia hazina kuchakaa, kazi yako ni kung'arisha tu kama kioo cha gari, nitawaandalia '3D computer rendered model' ya jinsi jengo litavyoonekana baada ya hio upgrade bure kabisa. Vitu vingine vinatia aibu sana. Yaani hata simple landscaping/ gardening imewashinda kabisa, mazingira ya nje ni matope na uchafu uchafu.
________________________________
IG: @marble_na_granite
 
Umetumia vigezo gani hapo kwenye Bold... Pia ukubwa wa Klabu ni kiwanjani, mambo mengine baadae
 
Tuwekee picha za hilo jengo la Yanga
 
Duh, acha masihara mkuu

"Eti klabu kubwa zaidi africa"

You are joking right?
 
Ushauri mzuri sana, ingawa viongozi wa hizi Club zetu malengo yao ni kujinufaisha zaidi hivyo watakupuuuza ili kila mwaka wapate bajeti ya Kupaka rangi jengo.
 
Mkuu huu uzi ungeuleta kule jukwaa la Sports tuushambulie kama viwavi kwenye shamba la mahindi.
Lile sio jengo ni pango la Popo....
 
Watakwambia katiba hairuhusu rangi tofauti ya njao na kijani hakikisha hata vioo vinakuwa vya kijani.
Hahaha uzuri Aluco bond boards huja katika rangi mbali mbali zikiwemo njano na kijani, hali kadhalika vioo.
 
Hakuna hata lenye ahueni tena bora la yanga ila la simba ukipita hata nje kama jengo la kale bagamoyo lililonyewa na kunguru
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…