Magical power
JF-Expert Member
- Sep 27, 2022
- 2,158
- 5,626
"Baada ya kumaliza chuo 2019 nakusota bila ajira mwaka huu nikaona nitumie cheti cha JKT kuomba ajira ya ulinzi Suma JKT nikalinda sehemu ya kwanza ilikua Golden Tulip ambako security officer alinitaka niingie kila siku kwa mshahara wa laki mbili.
Ilikua changamoto kutoka kigamboni paka masaki
Ilinibidi kuomba nihamishiwe Uhuru height iliyopo posta pale napo nilifanya kazi mwanzoni, mambo yalikua sawa kwa kiasi japo tatizo ni lile lile hakuna mapumziko ni masaa ishirini na nne tukiwa mlinzi wa kampuni mmoja na baunsa mmoja baada ya kuzoeleka na maboss wapale tukawa tunapewa tips tugawane na wale mabaunsa kitu ambacho mabaunsa hawakukipenda.
Ikafikia hatua tukawekeana chuki mpaka tukawa hatueleweni.
Wakati huo nilipata msiba wa baba yangu, nilipoenda nikarudi nikabadilishiwa kituo na kuamia maeneo ya karibu na ocean road hapo napo tatizo nilile lile tulikua wachache na hakuna mapumziko wala maslahi (walinzi mnafahamu).
Nikajaribu kuongea na kijana anaye uza maji nje ya geti la ocean road ili anipeleke anapochukulia maji kwa malikauli na mimi yale masaa ninayopumzika niuze maji akaniambia kwa muonekano sitaiweza ile kazi(akanikazia).
Nikamfuata mzee fulani anatembeza viatu vya mtumba kusudi nilile lile wakati wa mapumziko niende kupoint mali nitembeze mtaani (akanikazia).
Wakati naendelea na kazi nilikua nikiwekeza elfu hamsini katika kila mshahara kama akiba. Nilipo toka msibani nilipokea rambi rambi kama laki nne nikazijumlisha jumla ikawa milioni moja na laki tatu nikatafuta piki piki used nikanunua.
Kila kijiwe nilipo enda jamaa walinifukuza nilifika pale ferry tena wale jamaa waliifunga mpaka mnyororo pikipiki.
Dah ikabidi nirudi nyumbani huku nikiendelea na kazi kwa manyanyaso juzi niliacha kazi baada ya kuongezewa masaa ya kazi bila kuongezewa mshahara.
Nikaitoa pikipiki kwa dereva aniletee hesabu na mimi niendelee kutafuta kazi ya professional niliyosomea kama mwalimu wa history na kiswahili.
Hivi sasa nasubiri majibu ya usahili niliofanya kwenye vituo mbali mbali kikiwemo kimoja maeneo ya magole.
Bado napambana sijatoboa" Bahati, Dar.
#WatuNiStory