John Heche: Magufuli ameondoa bandari ya Kwala imerudi mjini na kufanya Mji wote kuwa sehemu ya kuweka Makontena

John Heche: Magufuli ameondoa bandari ya Kwala imerudi mjini na kufanya Mji wote kuwa sehemu ya kuweka Makontena

Mkalukungone Mwamba

JF-Expert Member
Joined
Aug 29, 2022
Posts
3,141
Reaction score
7,205
"Kuku mmoja anayetaga mayai ya dhahabu ni bandari ya Dar Es Salaam. Unachotakiwa kufanya ni kuhakikisha hakuna usumbufu kwenye mizigo, kwanza unawatengenezea watu barabara za uhakika kutoka Bandarini. Magufuli alianza kujenga bandari ya Nchi kavu Kwala kwamba mizigo yote itoke bandarini iende Kwala na pale Kwala Magufuli aliweka eneo la Zambia, Congo, Burundi na nchi zote zinazotutegemea."

Soma Pia: Suluhisho la foleni Dar, ni kuondoa malori bandari kavu katikati ya Jiji kuyapeleka Bandari kavu ya kwala

"Ameondoka Magufuli, Bandari ile imerudi Mjini, Dar Es Salam Mji wote imekuwa sehemu ya kuweka Makontena, wanafanya usumbufu mkubwa sana kwa Wafanyabiashara, Kontena za mtu mmoja zinagawanywa Posta, lingine Mbagala, lingine Vingunguti, unapata usumbufu mkubwa sana wa kutafuta kontena. Bandari hii tusipochukua hatua inaenda kufa." John Heche, Makamu Mwenyekiti wa Chadema akizungumza na Vijana wa Chadema leo Jumatano.

 
huo ni ushahidi tosha na uliowazi kwamba hawa wanaoitwa "wafanyabiashara wakubwa" tanzagiza wote ni matapeli na wanaishi kwa wizi na udanganyifu tu, kama tukiikomboa nchi yetu na kuanza kujenga real economy based on planning and real skills kama engineering, it, biotech, mathematics etc hakuna hata mmoja wao atakuwa bilionea hapa tanzagiza amini hilo, wanaweza tu kuwa bilionea kwa wizi na unfair treatment of others kwa kuitumia serikali walioshika kufanya uchuuzi kuleta imports ktk china na kusambaza kwenye mafremu nchi nzima au utapeli na money laundering kwenye mipira lkn kwenye real economy hawana hiyo intelligence, tukijenga real economy uchumi na kazi zote zitashikwa na black people kwa maana ndiyo wasomi wakubwa hapa nchini ...
 
NYOOSHA MAMBO,FOLENI ZIONDOKE MIJINI, INSHALLAH...
-Shughuli zote za uhifadhi wa makasha ya mizigo au dry port ni vyema zote zikaamia kwala,ili jiji lipumue!...
 
Unadhani swala mabasi kwenda stend ya maghufur litafanikiwa .?mi nadhani Kuna ualakini ni big ishu
 
Back
Top Bottom