Naomba niseme haya sio maono ni hisia tuu kama za mwanamke mwenye mimba kwa mumewe.
Sakata la Feisal sio kubwa kama linavyopambwa, mi naamini Injinia hana tatizo na mchezaji kiasi hicho na hata hivyo yupo karibu sana na wachezaji wetu.
Feisal anatumika kuihujumu club ya Yanga kwa kujua ama kutokujua na wale ambao wamejaribu wakati wa ligi ikashindikana.
Club pinzani ya Simba ilihitaji point sita tuu ili aweze kuwa sambamba na Yanga ambaye alikuwa anaongoza ligi.
Mechi na azam ilikuwa kubwa sana, kijana Feisal alikuwa tegemeo kwenye kikosi sasa akatumika kuihujumu Yanga ili apoteze hiyo mechi , ikumbukwe alitoka kupoteza mechi na IHefu hivyo kwa vyovyote vile fitina za mpira zilitumika.
Yanga ilisimama imara, angalia hata bao alilofunga Mayele dhidi ya Azam alivyolishangalia. Kwa sasa tukimaliza michezo yetu yote tukawa kama Simba ambao wanazurura tuu kwa sasa tutaanza kufuatilia hizi kesi.
Kuhusu kutoka hadharani kwa viongozi wa Yanga ili kujibu tuhuma, mi nadhani kukaa kimya kwa sasa ndio jibu zuri zaidi kwa sababu neno lolote atakalotoa Garib au Hersy ni dhahabu kwa wanahabari uchwara. [emoji123][emoji123]