Baada ya kumsikiliza mama wa Feitoto, ni dhahiri Fei na familia nzima wamerubuniwa

Machafu huonekana Masafi Yakiwepo! Leo Hela imeonekana ndogo Kwa sababu Master Key na Screen Protector wanachukua Mkwanja Mrefu!

Iko hivi, Hata leo waamue kumlipa Fei toto mil 30 kwa Mwezi mathalani, wakaja wachezaji wengine wakawa wanalipwa labda 50mil kwa mwezi, Fei atasusa tena atasema anaonewa, anadhulumiwa!

Huyo aliyempa zile milion 100+ za kuilipa Yanga, Amlipe sasa Milion 20 kila mwezi awe anampigia danadana kwenye bustani yake pale nyumbani kwake pale Msasani Peninsula.
 
Unatakiwa ujibu ulichoulizwa, kuita mtu mjuaji na kumpuuza ni dalili ya muoga, aliyeamua kujificha kwenye kivuli cha ujinga.

Mchezaji kusaini mwenyewe mkataba, hakuwezi kuwa sababu ya kumzuia kuuvunja ikiwa kuna kipengele husika kinachomruhusu kufanya hivyo kwenye mkataba wake, na ndicho Fei alichofanya, hili ni simple kabisa kueleweka ukiweka pembeni ushabiki na mahaba yako kwa timu.

Ajabu utopolo kwa upande wao, mpaka leo bado hawajatuwekea kipengele chochote kinachoonesha Fei kavunja makubaliano, wako kimya, na ajabu zaidi wanaendelea kumlipa Fei mshahara, kama sio kumtongoza arudi kwenye timu huko ni kufanyaje?

TFF nao kwa upande wao, wanaendelea kuwabeba kwenye maamuzi yao, sio sababu kwanini hutoa maamuzi nusu nusu na kusema mengine watayatoa siku za mbele, hizi haraka za TFF kwenye hili suala ni za nini? hawa wanatumiwa na wanasiasa.

Kama wewe hauna mahaba ya ajabu kwa timu yako, jiulize hayo maswali, usimkasirikie anayekuamsha usingizini ili utoke kwenye lindi la ujinga ulilopo.
 
Wewe ndio haupo serious, hiyo milioni 4 kama unaiona nyingi ni kwako kutokana na hali uliyonayo kimaisha, sio kwa Fei na mama yake, njaa zako usizihamishie kwa wengine, wao wame set standard yao ni above 4 milion, hilo sio kosa kwao.
 
- Yanga hawawezi kukuwekea wewe vipengele vya mkataba kwa sababu wewe sio muhusika wa huo mkataba. Mkataba ni siri baina ya wahusika.

- Yanga wanaendelea kumlipa Feisal kwa sababu Feisal bado ni mchezaji wao. Analipwa kwa muujibu wa mkataba wake aliosaini na Yanga.

- TFF kuna wanasheria, Yanga wana wanasheria, na Feisal pia anao wanasheria. Wote wamehusika na hilo shauri, hatujasikia upande wowote ukilalamika kua maamuzi hayakua ya haki.
 
- Yanga hawawezi kuniwekea mimi kwasababu hawana, ndio maana wanabebwa na TFF kwa kutoa maamuzi nusu nusu bila kuwepo taarifa kamili iliyojitosheleza, tuone vipengele gani Fei kavunja kwenye mkataba wake.

- Feisal hatakiwi kulipwa mshahara bila kuutumikia, unaposema tu wanamlipa mshahara kwasababu ni mchezaji wao, hakusajiliwa ili akachezee nyumbani, fungua ubongo huo, wanachofanya Yanga kumlipa Fei mshahara wakati hachezi, ni sawa na kumrubuni kwasababu wamegundua ujinga wao.

- Hujasikia upande ukilalamika au hutaki kusikia? kama pasingekuwepo na malalamiko hilo suala lisingerudishwa TFF kwa ajili ya review.
 
Kama kuna msanii aliniuma kwa sbb ya life style aliyochagua kuishi basi alikua Banza Stone (rip), mwengine anaefatia nadhan ni huyu dogo Fei. Unapokua mtu maarufu kwny nchi yako basi maisha unayoishi hayapaswi kua yako peke yako lazima ujue kuna jamii ya kina sisi na watoto wetu tunakuangalia kama kioo so you have to balance. Fei asipostuka mapema anaenda kupotea, mchezaji anahitajika kucheza mechi nyingi Fei kakosa mechi nyingi tena muhimu mbaya zaidi Yanga kama wameziba pengo lake. Ningekua Fei ningenyoosha moja kwa moja kwa Injinia kuomba msamaha na kuyajenga sbb hana nafasi yyt ile ya kushinda hii kesi.
 
- Hauwezi kuthibitisha kwamba yanga hawana makubaliano na Feisal.

- Hauwezi kuthibitisha kwamba TFF wanaibeba Yanga.

- Hauwezi kunakili au kuonyesha kanuni yoyote inayowataka TFF wakuonyeshe wewe yaliyomo kwenye mkataba ya Feisal na Yanga.

- Hauna uelewa wa masuala ya kisheria, ndio maana haujui kama hukumu hutolewa kwanza, kisha proceedings zinafuata baadae. Badala yake, unalalamika eti maamuzi yanatolewa nusu nusu!

- Upo utaratibu wa kufuatwa kama Feisal anadhani ameonewa. Aende CAS.

- Hautaonyeshwa yaliyomo kwenye mkataba wa Feisal kwa sababu hayakuhusu, wewe sio muhusika wa huo mkataba. Na hakuna kitu utafanya, zaidi ya kulialia huku mitandaoni.
 
Wewe ndio haupo serious, hiyo milioni 4 kama unaiona nyingi ni kwako kutokana na hali uliyonayo kimaisha, sio kwa Fei na mama yake, njaa zako usizihamishie kwa wengine, wao wame set standard yao ni above 4 milion, hilo sio kosa kwao.
Kuna watu duniani hapa mmekuja kimakosa sana. Halafu sijui ni kwa nini Jamii Forums watu wengi mnapenda kujitutumua mkiwa nyuma ya keyboard, na wakati wengi wenu ni wachovu tu!

Hivi usikute kipato chako wewe kama wewe kwa mwezi ni tia maji tia maji tu! Ila unamsemea huyo mtoto huku ukiwa umebana kabisa na pua eti "hiyo milioni 4 unaiona nyingi kwako kutokana na hali uliyo nayo kimaisha"! Kwani wewe hapo ulipo una hali gani ya kushangaza kimaisha?

Halafu huyo Fei Toto wenu kabla ya kuja Yanga alikuwa analipwa milioni ngapi kule JKU alikokuwa akicheza? Nyinyi ndiyo maana mnaitwa mbumbumbu! Maana uwezo wenu wa kufikiri uko chini sana.
 
Unapoteza tu muda wako kuielewesha hiyo mbumbumbu ya Mh. Ismail Aden Rage. Kamwe haitakuelewa.
 
Umeandika mashudu tu hapa. Najuta kwa nini nimepoteza muda wangu kusoma. 🚮
 
Kwa Fei hiyo pesa ni ndogo dada, kumbuka huyu ni mchezaji, jinsi miaka inaenda ndvyo nguvu na uwezo hata kiwango kinapungua, imagine 36 yrs anaacha soka afu hana cha maana alichopataa, ataishije kuelekea uzee wake?

Kwan mie nlijuaga wachezaji wazawa wanaolipwa pesa ndefu Bongo, Fei yumo, eti 4m?? Jaman kujitoa kote kuleeee???

[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] lazima akimbieeee
 
Hakikaaaa.
 
Nyingi kwako mkuu,kuna waziri mmoja alisema mil 10 ni pesa ya mboga tu...maisha hubadilika kulingana na hadhi,mazingira na majukumu, kwa mfano wewe hapo unaweza kuiona nyingi kutegemeana na mazimgira yako,majukumu yako na hadhi yako....

Tafuta Hela.
Kwa mtu yeyote mtafutaji, ukimuambia hii hela ni ndogo; anaweza kukuchapa hata kibao. Kwangu mimi hata shilingi 100 ni kubwa. Maana ukiitoa katika fedha yoyote ile, utakapoitoa hiyo shilingi 100 na thamani ya hiyo pesa itabadilika.

Sasa nyinyi mnaojifanya ni matajiri humu Jamii Forums, daima nitaendelea kuwashangaa. Mnaidharau milioni 4 anayolipwa Yanga, huku wachezaji wenu wenhi wakilipwa mishahara chini ya hapo!


Na kama mimi ni muongo, niwekee mkeka wa wachezaji wenu wa simba hapa! Halafu tuone mishahara ya akina Izrael Mwenda, Nasoro Kapama, na ile ya akina Nelson Okwa, Augustine Okrah, Clotus Chama, nk.
 
Ukweli mtupuuuu huuu. Umeamaliza kila kitu.
 
Nikiacha ushabiki nakiri kweli hapa mchezaji na mama yake wamemkosea muajiri wao
 
Jaman mie nilijua Fei anapata zaidi ya 10m, khaaah eti 4m [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Ahsanteeeeee na mie nataka kujua hili suala LA team kuvunja mkataba wa mchezaji.

Swali zuri sanaaa, tuone majibu.
 
Sasa km mchezaji hataki kutokaaaa,???
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…