denooJ
JF-Expert Member
- Mar 31, 2020
- 18,509
- 68,228
- Yanga na Feisal walikuwa na makubaliano kimkataba ndio maana suala lao lilikuwepo TFF kwa ajili ya maamuzi.- Hauwezi kuthibitisha kwamba yanga hawana makubaliano na Feisal.
- Hauwezi kuthibitisha kwamba TFF wanaibeba Yanga.
- Hauwezi kunakili au kuonyesha kanuni yoyote inayowataka TFF wakuonyeshe wewe yaliyomo kwenye mkataba ya Feisal na Yanga.
- Hauna uelewa wa masuala ya kisheria, ndio maana haujui kama hukumu hutolewa kwanza, kisha proceedings zinafuata baadae. Badala yake, unalalamika eti maamuzi yanatolewa nusu nusu!
- Upo utaratibu wa kufuatwa kama Feisal anadhani ameonewa. Aende CAS.
- Hautaonyeshwa yaliyomo kwenye mkataba wa Feisal kwa sababu hayakuhusu, wewe sio muhusika wa huo mkataba. Na hakuna kitu utafanya, zaidi ya kulialia huku mitandaoni.
- Naweza kuthibitisha TFF wanaibeba Yanga kwasababu wamekuwa na maamuzi yenye mashaka kwenye hili suala, na walishawabeba tena kabla kwenye kesi ya Hersi na Manara, ambayo mpaka leo bado haijatolewa maamuzi [precedence].
- Hata kama siwezi kunakili, TFF kimsingi wanatakiwa kwenye maamuzi yao waoneshe kipengele cha mkataba ambacho Fei alikivunja mpaka waseme ni mchezaji halali wa Yanga, lakini hawajawahi kufanya hivyo zaidi ya maneno matupu, suala la kisheria lazima lije na majibu ya kisheria, sio porojo kama zako, sijui unanielewa?!
- Usiseme sina uelewa wakisheria wakati hao TFF wenyewe hawafuati sheria na taratibu, najua nisemacho; hili shauri la Fei mwanzo TFF walikuja na taarifa nusu nusu kama ya jana, wakadai wangekuja na taarifa kamili, lakini hawakuwahi kufanya hivyo, zaidi ya danadana zao za kila siku, proceedings za TFF ni za hovyo zilizojaa ubabaishaji wa hali ya juu.
- Naamini huko CAS ndipo anapoelekea, TFF hawana weledi wa kuamua mashauri kama haya, dawa yao mpaka iwe suala linalohusu Yanga vs Simba, lakini kwa individual players TFF wanatumika kukandamiza haki za mchezaji.
- Hakuna popote nimetaka kuoneshwa mkataba, nachotaka TFF waseme, wanapodai Fei ni mchezaji halali wa Yanga watuambie wamefanya hivyo kwa kunukuu vipengele gani alivyovunja kwenye mkataba husika, hili tumeona likifanyika sehemu nyingi, hata kule mahakamani unapojitutumua unazijua taratibu zao, wacha usshabiki maandazi.