Nikianza kueleza sababu ya hiyo hali naweza sema ni 'Desire'au kwa kiswahili ni Hamu au Tamaa zao ndizo zinawapelekea kuwa hivyo.
Kiasili Tamaa au 'Desire' hutukumba wanaadamu wote, kama mtaalam mmoja alivyowahi sema; Tamaa namna ilivyo huchochewa na mambo makuu mawili...
a) Tamaa huchochewa na Uigaji (imitation)
Hapa wanaadamu hupenda au hutaka vitu kwa sababu tu tunaona watu wengine wanavitaka. Mathalani waweza kwenda mahali kupata chakula ukakuta migahawa miwili, Mmoja una watu wengi wanapata chakula ndani na mwingine hauna watu... Kikawaida akili hutuamuru kwenda kwenye ule wenye watu. Hii inatokana na imani yetu kuwa kwakuwa watu wengine wameupenda basi lazima utakua mzuri na huduma zitakuwa nzuri tu, nasi hujikuta tunatamani kuingia kupata huduma na kuukwepa ule mgahawa mtupu hata Kama wakati mwingine huu mtupu huwa na chakula bora zaidi.
b) Tamaa huchochewa na Ushindani.
Maisha ya mwanadamu yamejaa Ushindani kila mahali, toka kwenye familia watoto hushindana kupata makini au 'atensheni' ya wazazi, wafanyakazi hutafuta 'atensheni' ya mabosi maofisini n.k.
Asili yetu hii ya Ushindani ya KUTAKA KUCHUKUA VITU AMBAVYO WENGINE WANAVYO hutupa furaha na kutufanya kujisikia ufakhari pale tunapofanikiwa.
Hivyo, ktk kisa chako ni dhahiri hao akina dada wanakutaka kwa sababu wameona kuna mtu kakubali kuolewa nawe nao vichwani mwao wanaamini kuwa 'ni lazima huyu mtu atakua na kitu cha ziada mpk fulani kakubali kuolewa nae'
Na pia ktk fikra zao watakuwa wanaendeshwa na tamaa ya kumpokonya mwanamke mwenzao kitu alichonacho (mume) na kuchukua wao ili tu kujifakharisha.
Ndio asili yetu wanaadamu.
CHA KUFANYA:
Hii ni juu yako sasa, kwa maana ushajua wanachokitafuta na kinachowasukuma kukufuata...
Namna bora ya kuamua ni kuchanganua faida na hasara za maamuzi utakayoyachukua.
Kama utaamua kuwala au kulinda ndoa yako kikamilifu.
Kama unaithamini ndoa zaidi basi ni muhimu kuwaacha ila kama una shauku ya kujaribu vitu vipya basi hii ndio fursa adhim kabisa...ila jua huyu mwanamke uliyemuoa ndio karata yako ya dhahabu pindi utakapomuacha huo mvuto kwa hao WENGINE taratibu utapungua.
Kila la kheri.