JituMirabaMinne
JF-Expert Member
- May 4, 2020
- 3,381
- 9,744
Kwanza nilikua nishapanga kuwa gari yangu ya pili kumiliki lazima itakua Toyota Premio New model. Naipenda sana hii gari, it is my dream car.
Hii gari ni nzuri sana ila ukipata yenye 1nz.
Hayo matoleo yaliyobaki yenye engine za ZR ni kisanga.
Kwenye hizo engine za ZR (2ZR FE na 3ZR FAE) matatizo ambayo engine za series ya NZ, AZ, ZZ n.k. huwa zinahimili, kwenye hizi engine mpya kama ZR gari inakuzimia.
Matatizo kama "System is too lean" kwenye engine kama 1nz unaweza usisense kama kuna shida na gari inaendesheka vizuri kabisa japo engine inakuwa inazalisha joto jingi, in a long run inaweza damage engine.
The same problem kwenye engine kama 3ZR FAE gari inakuwa inazimazima, unawasha unaenda kidogo inazima. The worst ni kwamba hilo ni moja ya matatizo ambayo hayapo direct. Hivyo gari unaweza ukasumbuka nayo sana.