Mystery
JF-Expert Member
- Mar 8, 2012
- 15,843
- 31,057
Ni dhahiri kuwa Kwa Kila mpenda Demokrasia hapa nchini, anapaswa ampongeze Kwa dhati, Rais Samia Kwa hatua alizochukua za kishujaa za kufutilia Kwa mbali zuio haramu, lililokuwa limewekwa na mtangulizi wake, mtawala wa awamu ya 5. Mwendazake Magufuli, za kupiga marufuku mikutano ya kisiasa ya vyama vya kisiasa nchini
Kama mnakumbuka vizuri Kuna Sheria nyingi zilizokuwa zikipelekwa bungeni, katika kile kilichokuwa kikiitwa miswada ya dharura na kupitishwa "fasta fasta" na waheshimiwa wabunge wetu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Kwa kweli, Kwa mwendo tuliokuwa, tukienda nao, nchi hii ni dhahiri, ingerejeshwa Kwa "mabavu" katika mfumo wa chama kimoja!
Kama nchi naamini tulikuwa tukienda vizuri katika mfumo wa kisiasa wa vyama vingi, hadi mwaka 2015, alipoingia madarakani, Mwendazake Magufuli, ambaye utawala wake, uliamua Kwa makusudi kupiga U turn na kuirejesha nyuma nchi yetu katika kuijenga Demokrasia nchini.
Tukumbuke pia mtawala wa awamu ya 5, alidiriki kutamka hadharani kwenye sherehe za chama Chao Cha CCM, mwaka 2016, zilizofanyika mjini Singida, dhamira yake ya kutaka kuviua Kwa "mabavu" vyama vyote vya upinzani nchini, kuwa ifikapo mwaka 2020!
Vitendo vilivyofuata baada ya kauli yake hiyo, kama vile kumiminiwa risasi 16 mfululizo Kwa kiongozi wa Chadema, Tundu Lissu mwaka 2017, kubambikiziwa kesi mbalimbali Kwa viongozi wengi wa Chadema, vinadhihirisha kuwa kweli mtawala huyo alidhamiria kuviua Kwa "mabavu" vyama vyote vya upinzani, hususani Chadema, ifikapo mwaka aliotabiri yeye wa 2020!
Kwake yeye aliona ni kosa linalofanana na uhaini, Kwa kiongozi yeyote wa chama Cha upinzani, kukosoa sera zake "binafsi" na za chama chake Chake Cha CCM!
Hata hivyo Rais Samia "ametengua" fikra na matendo ya mtangulizi wake, Kwa kutamka kuwa Serikali yake ipo tayari kukosolewa, kwani anaamini kuwa hiyo ndiyo njia pekee ya kuweza wao watawala kuweza kujirekebisha na kuwaletea maendeleo endelevu watanzania.