Baada ya kushindia maji na matunda kwa siku 30 nimeweza kupungua uzito wa kilo 8 tu!

Baada ya kushindia maji na matunda kwa siku 30 nimeweza kupungua uzito wa kilo 8 tu!

Covax

JF-Expert Member
Joined
Feb 15, 2021
Posts
10,198
Reaction score
35,323
Kama nilivyosema kwenye huo uzi wangu na kupewa ushauri mbali mbali, niliufanyia kazi, siku 30 bila chakula cha wanga nashindia matunda na maji tu usiku kipande cha gimbi na mboga mboga nimeweza kupunguza uzito kwa 8kg tu.

Lengo ni kupungua mpaka 85kg, bado kg 11 niendelee au ntaugua vidonda vya tumbo?

Hongera...

Kula kidogo, usiache kabisa...

Utaumwa...
 
Ila kilo 8 nyingi aisee. Hongera.

Maana ukienda bucha, ile kilo 2 tu ni pande la mnofu.
[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]acha hizo mtu anaangaila na 105kg loh kuweka mwili ni rahisi ila kuuondoa sio mchezo.
 
[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]acha hizo mtu anaangaila na 105kg loh kuweka mwili ni rahisi ila kuuondoa sio mchezo.
Asiache kula. Kabisa. Awe anakula mdogo mdogo. Anachofanya ni suicide. 😁😁
 
Hongera sana mkuu....

8kg ni 17pounds wewe unaona mchezo ila ni hatua kubwa sana.....

Hata muonekano wako utakuwa umebadilika

Sasa pambana huo uzito usirudi, hapa ndo kazi ilipo
 
Bila picha ni umbea kama umbea mwingine tuu
 
Usiache kula kabisa mchana...
Kuna MTU alikuwa bonge alipungua hadi kushangaza, hakuwahi kwenda Gym ila misosi yake ilikuwa ni mboga za majani, mtindi na matunda matunda...

So mkuu kula hayo madude ushibe kabisa halafu masoda na vitu vitamu acha... utapungua kwa kasi.
 
Ahsante ila mimi mtindi naweka asali tu.
 
Ufanye na mazoezi sasa. Maana wakati mwingine kuridhika katika maisha kuna changamoto zake. Mimi nina mwaka wa 10 huu sasa, nacheza kati ya 75kg - 80kg.
 
Ufanye na mazoezi sasa. Maana wakati mwingine kuridhika katika maisha kuna changamoto zake. Mimi nina mwaka wa 10 huu sasa, nacheza kati ya 75kg - 80kg.
Hongera hiyo sio mbaya kwa mwanaume
 
Back
Top Bottom