Lord denning
JF-Expert Member
- Jun 3, 2015
- 15,819
- 33,255
Baada ya kuona Wananchi wengi wanaielewa hoja ya Lissu na Chadema kuwa bila kufanya Marekebisho ya Katiba na Sheria za Uchaguzi hakutakuwa na Uchaguzi Mkuu mwaka huu, CCM wamechanganyikiwa kiasi cha kuanza kutengeneza propaganda mfu wakidhani wataweza kuendelea kuwarubuni Watanzania kukubali udhalimu wao na utapeli wao.
Kuanza kutumia vyombo vya habari kuanza kurusha mahojiano ya kutengeneza ya watu wanaowatengeneza kujifanya wananchi eti wanapinga hoja zilizoenda shule za Chadema ni ushahidi tosha kuwa CCM wana hali mbaya sana na sasa wamehamia kufanya propaganda wakidhani wataendelea kuwarubuni Watanzania.
Siku ya jana wakati Lissu yuko njiani kwenda Singida walikomuandalia mapokezi kabambe, CCM na wajinga wao walitengeneza mahojiano feki ya watu waliowatengeneza eti kuwa Wananchi wa Ikungi ili kutengeneza Propaganda kuwa Wananchi wa Ikungi anakotoka Lissu hawaungi mkono Kaulimbiu ya Chadema kuwa No Reform No Election.
Kilichonifurahisha, baada ya clip hizo kurushwa kwenye vyombo mbalimbali vya habari, nimefurahi kuona reactions za watanzania zikionesha wazi wameshagundua kuwa hiyo ni michezo ya CCM kueneza propaganda mfu na kuwatisha ili wasifanye mabadiliko ya kweli kwa faida la Taifa lao.
Nimependa pia namna Watanzania walivyogundua kuwa hizo ni propaganda za CCM kwa sababu wameonesha wazi kushangazwa na vyombo vyote vya habari kurusha taarifa hiyo moja yenye maudhui yanayofanana wakati habari ya msingi iliyopaswa kurushwa ni safari ya Tundu Lissu kuelekea Singida.
Nawaonea huruma sana CCM. Wanajaribu sana kupingana na wakati ila wasichokifahamu ni kwamba hakuna ambaye amefanikiwa katika kupambana na wakati.
CCM imeshachokwa kweli na Watanzania na uzuri ni kwamba, watanzania wameshagundua kuwa CCM ni chanzo kikuu cha umaskini wao na wao kuwa na maisha duni.
Ushauri wangu wa CCM. Kubalini yaishe. Muda hauko upande wenu.
Ushauri wangu kwa Media zinazokubali kutumika na CCM kuendesha hizi propaganda mfu kuanzia Global Publishers, Jambo TV, Mwananchi Digital, ITV na nyinginezo. Jitokezeni Muhesabiwe.
Wakati ni huu na msije mkasema hamkuambiwa mambo yatakavyowarudia maana naelewa mnasoma comments za wananchi wanavyokataa hizo propaganda mfu mnazotumiwa kizieneza.