Erythrocyte
JF-Expert Member
- Nov 6, 2012
- 128,308
- 245,426
Ni wazi TAKUKURU baada ya kushindwa kubaini makosa kwenye michango ya wabunge wa Chadema , kutokana na kudanganywa na Peter Lijuakali, Mbunge aliyeanza vituko Chadema kutokana na chuki ya kukataliwa kwenye kinyang'anyiro cha uongozi wa Chadema Mkoani Morogoro, ikaanza njama zingine nje ya tuhuma za awali.
Kwa vile TAKUKURU imeamua kutumika kuishambulia Chadema kwa maelekezo ya mwanaccm Lijuakali na kuacha kufuata weledi kama ilivyoainishwa kwenye Katiba ya nchi, na kwa ushahidi mwanana alioweka Katibu Mkuu wa Chadema Mh Mnyika, ambao umeivua nguo Takukuru bila shaka yoyote ni vema basi MKURUGENZI WA TAKUKURU akajiuzulu ili kulinda heshima ya Taasisi ya umma ambayo si mali ya CCM.
Wala asione aibu , atoke tu kama wengine walivyotoka, hakuna atakayemshangaa bali atapongezwa na kujilindia heshima yake .
"Nitasema kweli daima , fitna kwangu mwiko"