Nyote mnaosema GENTAMYCINE mzushi na mwongo naomba anzeni kwanza na wale ambao jana walikuja humu na threads nyingi wakisema kuwa Ruge Mutahaba alikamatwa na akaenda Central Police na bahati nzuri Ruge Mutahaba muda huu huu amepinga na kasema kuwa hakuenda Central Police na aliishia tu Oysterbay kutoa maelezo. Hivyo kabla ya kukurupuka na GENTAMYCINE basi anzeni kwanza na WAZUSHI wa threads za jana ambazo hata sasa hivi bado zipo na zina trend. Nimefurahi mno Ruge Mutahaba kuweza kufunguka na sasa lengo langu kuu la kutaka kujua ukweli juu ya hili limetimia na sasa sina tena Ugomvi na Mtani wangu Ruge kwani angeenda kinyume nilikuwa tayari nina Makombora yangu ya IBM ( Intercontinental Ballistic Missals ) nimeyaandaa dhidi yake. Ana bahati mno Mtani wangu!
Nimwombe tu Makonda kuwa atoke sasa Kwake Masaki na aende IKULU kwa Rais amwambie kuwa IMETOSHA na atuachie Mkoa wetu kwani kwa maelezo KUNTU ya Ruge ni dhahiri kuwa Paul Christian Makonda HATOSHEI na AMETOKOTA.
Rais JPM fukuza Kazi upesi Makonda.