Wakuu hbri za humu. Kuna mtumishi alienda masomoni bila utaratibu wote kukamilika. Cha ajabu mtumishi akawapeleka CMA, kuwashitaki kwa nini hapewi mshahara. Hana barua ya kufukuzwa kazi wala onyo na mishahara check inakuja lkni hapati mshahara. Afisa utumishi mahakamani walimuuliza, je huyu ni mtumishi au siyo mtumishi? Akasema mpaka sasa ni mtumishi. Je wewe kama mwanasheria hiyo kesi utaamuaje? Afisa utumishi aliruka taratibu zote za utumishi. Je, jamaa atarudi kazini? Na wkti huo huo walimweka mtumishi hewa.