GENTAMYCINE
JF-Expert Member
- Jul 13, 2013
- 60,660
- 121,325
Katika kuonyesha kuwa hakufurahishwa ' totally ' na ' kufurumushwa ' Kwake katika Cheo chake alichojitungia mwenyewe cha Ukurugenzi wa Habari na Mawasiliano ( ambacho hata katika Katiba ya Yanga hakipo ) na ambacho sasa amepewa Ndugu Dismas Ten atayakekuwa akisaidiwa na Godlisten Anderson ' Chicharito ' aliyekuwa mpayukaji maarufu wa Klabu ya Yanga Ndugu Jerry Muro wakati akihojiwa na Waandishi wa Habari ambapo sehemu ndogo ya hayo mahojiano yake yanapatikana katika Mtandao wa Azam Media aliweza kuyasema haya yafuatayo ambayo sitayaongeza wala kuyapunguza...
Je wana Yanga wenzangu sisi leo ni wa kuitwa ' Wapuuzi ' na aliyekuwa Msemaji wetu Kipenzi na ambaye kila Uchao tulikuwa ' tunamtukuza ' na ' kumpamba ' Jerry C. Muro? Ni matumaini yangu makubwa Uongozi wetu chini ya Kaimu Rais wetu wa Yanga Bwana Clement Sanga na Katibu Mkuu wa Yanga Mwalimu Charles Boniface Mkwasa hawatalinyamazia hili kwani kiukweli Jerry Muro ' ametutukana ' na ' ametudhalilisha ' sana Sisi wana Yanga.
Wenu Mwanachama Mtiifu wa Yanga FC GENTAMYCINE na nitoe tu pongezi zangu kwa Uongozi wa Yanga kwa kuamua kumsajili Mchezaji Ibrahim Ajib na kuamua Kambi ya Timu yetu iwe kati ya Kigurunyembe Mkoani Morogoro au Kyela Mkoani Mbeya na tusiwaige wale ambao walipanda Ndege na sasa wapo zao kwa Madiba wanafanya mazoezi yao.
Hakika hakuna kama Yanga FC Afrika na duniani!
Nawasilisha.
- " Yanga ndiyo ilinihitaji na sikuihitaji Yanga "
- " Nimeenda Yanga nikiwa Tajiri tayari hivyo sikuenda pale kwa ajili ya Njaa "
- " Yanga inaongozwa na Viongozi Wezi na ina mashabiki Wapuuzi na Wanafiki sana "
- " Nimeibadilisha Yanga kutoka kuwa Timu ya Kishamba na kuwa Timu ya Kisasa "
- " Yanga inaibiwa na Manji alikuwa anaogopa kuwakemea kwakuwa alikuwa anajua wanakula nae wote na kwamba angewakemea basi hao hao Wezi wasingemrudisha tena Madarakani "
- " Mimi nimesoma na nina Elimu kubwa hivyo kuendelea kubaki katika Timu ya Wapuuzi ni kujivunjia tu Heshima yangu hasa kwa wale wanaojua uwezo wangu uliotukuka "
- " Hata huyo aliyenirithi asitegemee kulipwa Mshahara kwa wakati na najua atakimbia mwenyewe kwani Mimi nilikuwa sipati taabu ya Mshahara kwakuwa nimesoma sana halafu nje ya Yanga nilikuwa nafanya Kazi zangu binafsi ambapo nina Mabasi na Madaladala lakini pia nina Mke mzuri na Familia nzuri hivyo walichokifanya Yanga Kwangu ni kama tu kumpiga teke Chura "