Baada ya kutoswa kama Msemaji wa Yanga FC hatimaye Jerry Muro kauwasha moto na kuikashifu mno Yanga

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Joined
Jul 13, 2013
Posts
60,660
Reaction score
121,325
Katika kuonyesha kuwa hakufurahishwa ' totally ' na ' kufurumushwa ' Kwake katika Cheo chake alichojitungia mwenyewe cha Ukurugenzi wa Habari na Mawasiliano ( ambacho hata katika Katiba ya Yanga hakipo ) na ambacho sasa amepewa Ndugu Dismas Ten atayakekuwa akisaidiwa na Godlisten Anderson ' Chicharito ' aliyekuwa mpayukaji maarufu wa Klabu ya Yanga Ndugu Jerry Muro wakati akihojiwa na Waandishi wa Habari ambapo sehemu ndogo ya hayo mahojiano yake yanapatikana katika Mtandao wa Azam Media aliweza kuyasema haya yafuatayo ambayo sitayaongeza wala kuyapunguza...
  1. " Yanga ndiyo ilinihitaji na sikuihitaji Yanga "
  2. " Nimeenda Yanga nikiwa Tajiri tayari hivyo sikuenda pale kwa ajili ya Njaa "
  3. " Yanga inaongozwa na Viongozi Wezi na ina mashabiki Wapuuzi na Wanafiki sana "
  4. " Nimeibadilisha Yanga kutoka kuwa Timu ya Kishamba na kuwa Timu ya Kisasa "
  5. " Yanga inaibiwa na Manji alikuwa anaogopa kuwakemea kwakuwa alikuwa anajua wanakula nae wote na kwamba angewakemea basi hao hao Wezi wasingemrudisha tena Madarakani "
  6. " Mimi nimesoma na nina Elimu kubwa hivyo kuendelea kubaki katika Timu ya Wapuuzi ni kujivunjia tu Heshima yangu hasa kwa wale wanaojua uwezo wangu uliotukuka "
  7. " Hata huyo aliyenirithi asitegemee kulipwa Mshahara kwa wakati na najua atakimbia mwenyewe kwani Mimi nilikuwa sipati taabu ya Mshahara kwakuwa nimesoma sana halafu nje ya Yanga nilikuwa nafanya Kazi zangu binafsi ambapo nina Mabasi na Madaladala lakini pia nina Mke mzuri na Familia nzuri hivyo walichokifanya Yanga Kwangu ni kama tu kumpiga teke Chura "
Haya wana Yanga FC ' wenzangu ' tuliomo humu JF aliyekuwa Msemaji wetu Jerry Cornelius Muro ndiyo katuwashia hivyo moto na hizo Kashfa je hayo aliyotuambia ni ya kweli au kuna kitu ambacho anatutafuta ubaya sisi Wana Yanga hasa katika Kipindi hiki Kigumu na cha Shida hadi bado tunahangaika Kusajili Wachezaji wa Kuwakopa na kwa Mali Kauli?

Je wana Yanga wenzangu sisi leo ni wa kuitwa ' Wapuuzi ' na aliyekuwa Msemaji wetu Kipenzi na ambaye kila Uchao tulikuwa ' tunamtukuza ' na ' kumpamba ' Jerry C. Muro? Ni matumaini yangu makubwa Uongozi wetu chini ya Kaimu Rais wetu wa Yanga Bwana Clement Sanga na Katibu Mkuu wa Yanga Mwalimu Charles Boniface Mkwasa hawatalinyamazia hili kwani kiukweli Jerry Muro ' ametutukana ' na ' ametudhalilisha ' sana Sisi wana Yanga.

Wenu Mwanachama Mtiifu wa Yanga FC GENTAMYCINE na nitoe tu pongezi zangu kwa Uongozi wa Yanga kwa kuamua kumsajili Mchezaji Ibrahim Ajib na kuamua Kambi ya Timu yetu iwe kati ya Kigurunyembe Mkoani Morogoro au Kyela Mkoani Mbeya na tusiwaige wale ambao walipanda Ndege na sasa wapo zao kwa Madiba wanafanya mazoezi yao.

Hakika hakuna kama Yanga FC Afrika na duniani!

Nawasilisha.
 
Ok ahsante,jee hii hadithi yako inatufundisha nini 'babu'?
 
Uzaliwe milimani ujifanye Yanga kwani huko alikotoka hakuna timu!Yanga ni timu ya wazawa wa Dar es salaam kama ilivyo Mbeya city kwa wazawa wa Mbeya
 
Na haya yooooooooote kayaongea baada ya kutemwa,sasa watakaokuwa wanayashabikia zaidi maneno yake ni wale wanaosubiria kuliiba kombe,maana kiwanjani awatakuja kulipata kamwe.
 
Mimi mwenyewe nimeduwaa, jamaa alivyokuwa analipuka kipindi kile cha kudai point za mezani halafu eti leo hii amekuwa shabiki nguli wa Yanga[emoji15].... Interesting!

Wakuu, Gentamicin amechokoza masa tu yeye sio mshabiki wa Yanga ndio maana ameweka ". " kwenye neno wenzangu sababu anajua kuwa sio mwenzetu.
 
Hivi Simba SC tutawahi tena kuja kuwa na Kikosi imara na cha kukumbukwa kama hiki?

MAISHA YANAENDA KASI KWELI..JUZI ULIKUWA UNAISIFIA SANA SIMBA....Leo ghafla kwa unafiki uliotukuka unasema wewe ni Shabiki nguli wa Yanga..Interesting

Nilishawahi labda hata kukuonyesha Kadi yangu ya Uanachama ya Simba SC Mkuu? Na unathibitisha vipi kuwa Mimi GENTAMYCINE ni mwana Simba na siyo mwana Yanga? Hivi kumbe Mtu akisema au akijinasibu tu humu Mitandaoni kwamba Yeye ni Simba au Yanga tayari ndiyo kinakuwa uthibitisho na ushahidi wake tosha / kamili?

Mkuu unanipa sana machungu kwani hivi sasa wenzako Sisi wana Yanga sasa tunahangaika ' Kukopeshana ' huku na kule ili tusajili Kikosi kizuri cha kuweza kuepuka Kipigo cha ' Mbwa mwizi ' na ' Shalubela ' kutoka kwa Simba SC hapo August 23 katika Community Shield halafu Wewe unaleta tena habari zako zingine?

Vipi huna Ndugu labda huko Nanyumbu ili tuipeleke Klabu yetu ya Yanga ikafanye mazoezi kwani huku Kigurunyembe na kule Kyela wametukatalia hadi tuwape Kwanza ' advance ' na sisi hali yetu Kifedha unaijua ni ' tia maji tia maji ' hivyo tumechanganyikiwa na siku ndiyo zinazidi kukaribia hivyo tunaogopa Simba SC safari hii wasije kutupiga ' Week ' pale Taifa ikawa balaa tukatafutana na kuchapana Viboko.

Yanga Daima na Wenu Mwanachama Mtiifu GENTAMYCINE.
 
Reactions: 7ve
Hata aseme neno gani sisi wapenzi na washabiki wa Yanga tumetulia tu nasubiria ubingwa wa 4 nyie mlioenda FIFA subirini mletewe kombe msimbazi. Nashangaa hiyo trh 23 mtacheza na nani wakati bingwa ni nyie wenyewe mnaosubiria ushindi wa Fifa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Duuh kwa hiyo kiuhalisia wewe ni shabiki kindakindaki wa Yanga au Simba?? Maana naona kwenye ile thread ya kuisifia simba umefunguka kweli
 
Wakuu, Gentamicin amechokoza masa tu yeye sio mshabiki wa Yanga ndio maana ameweka ". " kwenye neno wenzangu sababu anajua kuwa sio mwenzetu.

Acha kuwadanganya Watu Mkuu Mimi ni mwana Yanga FC na wengi sana humu wanalitambua hilo. Hakuna Timu nisiyoipenda kama Simba SC. Mkuu vipi huko unapoishi hakuna uwanja angalau na sisi Timu yetu ya Yanga ije ifanye mazoezi ya Kujiandaa kwa ' mtanange ' dhidi ya Simba na Ligi Kuu? Safari tumeshindwa kwenda kuweka Kambi nchini Uturuki kwakuwa hali yetu ya Kiuchumi / Kifedha ni mbaya sana hadi unaona akina Msuva, Kaseke, Munishi, Mustapha na Niyonzima wametukimbia.

Sisi wana Yanga FC tunaumia na tunaona sana Wivu Simba SC kwenda kuweka Kambi nchini Afrika ya Kusini na hata usajili wao ni wa hatari mno kiasi kwamba kama Sisi wana Yanga FC tusiposhikamana nina wasiwasi mechi ya Ngao ya Jamii pale Taifa tunaweza kupata kipigo cha ' Shalubela ' na hata tukafungwa Week au ile ya Six O'clock kujirudia tena.
 
Duuh kwa hiyo kiuhalisia wewe ni shabiki kindakindaki wa Yanga au Simba?? Maana naona kwenye ile thread ya kuisifia simba umefunguka kweli

Fanya tu ana ana ana dooo....kisha Timu utakayoishia ndiyo naishabikia hiyo Mkuu.
 
Ndugu GENTAMYCINE ulipo kuwa shule uliwahi kukutana na maswali ya ku- summarize?

Na Wewe ulipokuwa Shule ulilielewa vizuri sana somo la Mwandiko? Hivi Mwalimu wako aliyekufundisha Mwandiko alikuambia kuwa neno ' ulipokuwa ' likiandikwa linaandikwa kama ulivyoandika Wewe ' ulipo kuwa ' kwa kuachanisha maneno? Usiwe mwepesi Kushabikia Choo cha jirani yako kimejaa wakati chako kipo hadi pomoni na Mifunza juu inatambaa huku wengine ukiwatumia kama Kitoweo katika Chakula chako unachokula.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…