Baada ya kutumia P-2 sasa anashindwa kubeba ujauzito, je afanye nini aweze kukaa sawa


Aende hospitali akaonwe na daktari bingwa wa kina mama na uzazi (obstetrician and gynecologist) ili afanyiwe uchunguzi na vipimo ili apatiwe matibabu sahihi.

Kila la kheri.
 
Mkuu umefanya utafiti gani kujua kuwa chanzo ni P-2? Wewe ni mchunguzi wa masuala ya uzazi?
 
Habari

P2 ni njia ya uzazi wa mpango ya dharula, haitakiwi kutumiwa kama njia ya uzazi wa mpango ya muda mrefu (ilipaswa atumie njia nyingine baada ya kushauriwa na wataalamu katika kliniki za uzazi wa mpango, hospitalini)

P2 ina changamoto ya kubadilisha mzunguko wa hedhi kwa muda mfupi, si zaidi ya miezi mitatu kawaida, isipokuwa kama imetumika mara nyingi mfululizo.

Dalili unazotaja, haziendani na madhara ya P2 peke yake, Kuna uwezekano mkubwa ana matatizo mengine yanayochangia.

Ushauri:
  • Aache kutumia P2 kwa sasa
  • Aonane na Bingwa wa magonjwa ya kinamama (Obstetrician & Gynecologist)
  • Ikiwa si rahisi kumpata huyo,afike tu hospitali iliyopo karibu kwa vipimo na ushauri wa kitaalamu
 
Apambane na hali yake
 
Atumie MP4 avuruge na siku zake za mwaka kabisa..
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…