Habari!
Binafsi Mimi ni Mkristo, charismatic christian, situmbishwi na ninachokiamini kwakuwa nimekithibitisha.
Kwasababu ya ukosefu wa ajira, kufukuzwa kazi, uvuvi , tamaa ya pesa na sifa basi watu wengi wamefungua huduma au wameingia kwenye huduma za Kichungaji, kinabii, kitume, kiinjilisti na ualimu.
Lakini mioyo yao Iko mbali na Mungu.
Ni wazinzi wa kutupwa, hutumia sadaka kwa anasa na wengine ni walevi.
Sasa hawa tumewasema vya kutosha na tutaendelea kuwasema na kuwakemea bila hofu. Maana waumini wao wakisia unawasema wanakwambia utapata laana kwa kumsema mpakwa mafuta.
Mpakwa mafuta ya nguruwe?
Sasa zamu yenu masheikh
Kuna masheikh na maustadhi wakisoma kidogo tu hugeuka kuwa wavivu na kuanza kujigeuza waganga wa kienyeji. Ni wazinzi, wachawi, waongo na wahuni waliojificha kwenye mgongo wa dini. Acheni tabia hiyo.
Wengine mnajuficha kwenye mgongo wa Dua. Acheni uhuni tafuteni kazi halali. Kwani ni nani aliyewaambia kuwa Quran inafundisha uvivu?
Wilaya niliyotoka kila kijana aliyesoma Quran akirudi nyumbani hugeuka mganga. Tumieni hiyo ELIMU ya Quran kuelimisha jamii na kuwa kielelezo cha tabia njema.
Acheni uhuni.