Juzi wazee wetu wameitisha Press na wameongea sana, kwa watu wasiojua ball ambapo wamekuja mjini miaka ya hivi karibuni akina Eddo Kumwembe na wachambuzi wenzako wajinga wajinga ambapo elimu zao ni za kuunga kuunga wanachukulia poa kauli za wazee wetu na kuona hazina mashiko.
Ukweli ni kuwa hadi mnaona Injinia Hesi anashiriki vikao vya CAF huku Yanga Jana kacheza na JKT Tanzania na kushinda mjue kuwa Ligi ya Tanzania wameshamaliza, mikakati na mbinu zao dhidi ya Simba ni mizito sana, mikakati yao ya kuiua SImba Iko kwenye bodi ya Ligi, Iko kwenye chama cha soka, Iko kwa waamuzi, Iko kwa makocha wa vilabu ambapo wamewahi kuchezea Yanga, Iko kwa wanachama wao wanaoiongoza Yanga kwenye vilabu vingine ambako wanavidhamini na Iko pia kwenye timuy yetu wenyewe ya Simba.
Tutapata sana taabu kuwafunga au kuwashusha hawa jamaa, hakyamungu nawaambia, hebu fikiria kipa wao kaingia nchini siku ya mechi na bado kacheza vizuri nyie hamuoni kuwa haya sio ya kawaida?
Wazee wangu wana hoja za msingi kabisa, kwa mfano Baraka Kizuguto Yuko TFF, Aron Nyanda Yuko TFF, Abeid Mziba Yuko TFF, hao wote wameshachezea Yanga na huyo Baraka aliwahi kuwa afisa pale jangwani wakati sie pale yupo Clifford Ndimbo TU ambaye hana ubavu wa kucheza na hao wote.
Kule bodi ndio usiseme, kwa hiyo hawa jamaa hatutaweza kuwafunga Wala kuwanyang'anya ubingwa na ndio maana zungu pori alisema watabeba ubingwa mara 30, hakusema kwa kubahatisha, alikuwa anamaanisha kwa sababu ya mikakati waliyokuwa nayo.
Njia pekee iliyobakia ni Moja tu kudadadeki, hakuna kulalamika Wala Nini, maana unaweza kwenda kulalamika serikalini kumbe unayemlalamikia ni Yanga Lia Lia, ushauri wangu wazee njia pekee iliyobakia Sasa hivi ni Moja tu, dondosheni KURUJUANI MOJA TU KUANZIA VIONGOZI WA jangwani, CHAMA CHA SOKA, CHAMA CHA WAAMUZI, BODI NA WALE WOTE WANAOTUSABABISHIA MARADHI YA MOYO HADI KUSABABISHA MWANACHAMA MWENZETU KUPOTEZA MAISHA PALE KIWALANI.PERIOD.