kifupi kirefu
JF-Expert Member
- Oct 29, 2018
- 539
- 3,507
Tulimzuia Dangote kutoa makaa ya mawe kutoka S.Afrika, je migodi yetu ya makaa ya mawe ipo hali gani leo? Kutoka kwenye lesson leant tunaamni mawazo yetu yalikua sahihi?
Tulidhibiti usafirishaji wa mazao ya chakula nje hasa Kenya ambayo inategemea chakula kutoka kwetu, je Hali ya soko la ndani ipo vipi? Kenya bado wanatutegemea au wametafuta soko la vyakula Mataifa mengine? Je, mkakati wakudhibiti mahindi na mazao mengine kwenda Kenya vina tija?
Tulidhibiti uuzaji wa korosho serikali ikaanza kununua yenyewe huku wakulima wakilazimishwa kusubiri mnada hata kama wanataka kuuza japo kilo kumi walipe ada za watoto. Mfumo huu baada yamajaribio bado una tija au tunatakiwa kutafuta mfumo mbadala?
Tumepandisha Kodi kubwa kwa bidhaa zinazotoka nje vikiwemo vitenge na kana ili kuvisaidia viwanda vya Mo na vingine vya ndani viweze kukua na kupata soko. Je bado tunaamini viwanda vyetu vinauwezo wakuzalisha quality product au ushindani kutoka nje unahitajika? Kwanini wafanyabiashara wanazidi kuagiza mzigo kutoka nje pamoja na bei kuwa juu? Mkakati huu bado unatija au Waziri wa viwanda anatakiwa kutafiti upya na kuja na suluhu?
Elimu ni bidhaa na pia ni huduma, tumewabana shule binafsi wasitoe huduma hii kwa Watanzania kwa lengo lakukuza shule za serikali lakini watoto wote wa vigogo na wafanyabiashara au watu wanaojiweza wanasoma private school, je lengo la serikali kamaalikueleweka na watumishi wa Umma watunga sera litaeleweka kweli kwa wananchi wakawaida? Kwanini tusiacha huduma na bidhaa hii ya elimu iwe yaushindani huru?
Tumeanza kudhibiti uingizaji magari kwa lengo lakutafuta pesa ya ukaguzi iliyokuwa inakwenda kwa makampuni ya nje, je Intelligence inasemaje kuhusu mwitokio wa wanannchi? Kwanini tangazo lile limeleta mshtuko mkubwa? Je bandarini Kuna garage na rasilimali watu kutoka serikalini wenye uwezo wa kukagua na kutengeneza hayo magari? Je mipaka mingine haitaruhusiwa kuingiza magari yaliyoshuka nchi jirani?.
Tuwe na tabia yakibiashara, ukijaribu mkakati huu ukashindwa usiwe mgumu kukubali mapungufu nakuja na mkakati mpya, tujifunze kujifunza kutoka field tutoke maofisini.