Baada ya Lundenga kukemea Matusi ya Mange, Wizara ya mambo ya ndani na Jeshi la Polisi latoa onyo

Baada ya Lundenga kukemea Matusi ya Mange, Wizara ya mambo ya ndani na Jeshi la Polisi latoa onyo

SANGAPIPI

JF-Expert Member
Joined
Jun 25, 2013
Posts
206
Reaction score
301
Wiki iliyopita kupitia mtandao wa Instagram,Blogger Mange Kimambi alimshambulia kwa matusi Aliyekuwa Miss Tanzania Hoyce Temu kwa kisa ambacho hata hakihusiani nae.Vilevile katika kashfa na tuhuma hizo walihusishwa hata watu wasiohusika katika ugomvi wa Mange na Ndugu yake Hoyce kinyume na sheria.

Hoyce Temu alieleza kusikitishwa kwake na maneno ya kashfa yasiyokuwa na chembe ya ukweli yaliyoelekezwa kwake na blogger huyo

Wadau mbalimbali walitoa maoni yao akiwepo Mratibu wa Miss Tanzania Hashim Lundenga aliyelaani vikali tabia hiyo iliyofanywa na Blogger huyo kuchafua majina ya watu kwa kashfa na tuhuma za uongo kwa malengo yasiyoeleweka.

Alisema inasikitisha kuona mtu ambaye anaisaidia jamii kwa hali na mali akitungiwa kashfa za uongo na kuchafuliwa jina pasipo sababu yoyote ya msingi.

Vilevile waziri wa mambo ya ndani ameonya kuwa Jeshi la polisi litachukua hatua kali bila huruma na bila kujali mhusika alipo kwa wale wote wanaotumia mitandao ya kijamii vibaya huku msemaji wa jeshi hilo akitoa msimamo mkali dhidi ya wale wote wanaotumia mitandao vibaya.

Amewataka wote ambao wanachafuliwa kwa njia ya mitandao waripoti TCRA au jeshi la polisi kwa hatua kali bila kujali jiografia ya makazi ya wahusika au mipaka.
 
!
!
Hivi mtanzania ukifanya kosa ukiwa nje ya nchi, sheria zikoje? Kama hivi je huyu dada anaweza kushtakiwa.
 
Hivi huyu mdada/mmama yuko juu ya sheria? Maana siyo mara ya kwanza kumsikia akitukana watu mitandaoni wakati sheria za makosa ya mitandao zipo wazi! Au hii sheria ya mtandao ni kwa watu gani??
 
Ya nini kumshitaki?

Tatizo siku hizi hii mitandao imejaa ma-pussy kibao.

Huyo wala hakuna haja ya kumshitaki.

Ni kumuwinda na ukimkamata sehemu unampa kichapo na kumwachia kovu la maisha.

Na anajua anao mess nao ni ma-pussy ndo maana hakomi.

La sivyo watu wangekuwa washamzimisha zamani sana.

Halafu anapewa kichwa sychophants wenzake.

Halafu unaweza ukakuta anafikiri kuwa US basi ana immune ya kisheria.Ignorance ni mbaya sana
 
Huyu dada mshamba mshamba tu. Anawaharibia watu pose sana huyu, iko siku atayakanyaga watu watamfanyia Noma watu walie oh kaonewa.
 
Halafu eti alidiriki kutangaza nia ya kugombea ubunge kupitia CCM!

Duh taifa liliepuka fedheha nyingine.

Nadhani alipoona hadi waganga wa kienyeji wapo bungeni akapata inspiration.

Ndio maana wengine tulisema sifa za ubunge ziwe zaidi kusoma na kuandika.

Kipimo cha akili timamu pia kiongezewe vigezo vya "Utimamu"
 
Zinaweza kuwepo. Kumbuka yule dogo aliye publish kwamba Jenerali Mwamunyange sijui kafanywaje fanywaje na amepelekwa nje ya nchi, alidakwa na anaendelea na kesi pale Kisutu. Sheria zipo na zinafanya kazi kama kawaida.

!
!
Tofauti ya huyu dada na yule wa Mwamunyange ni kwamba huyu wa Mwamunyange alifanya kosa akiwa hapa nchini wakati huyu dada yuko mamtoni. Je mipaka ya sheria ikoje? Je yule mtanzania aliyeamua kuolewa kule uingereza akirudi naye atashtakiwa?
 
!
!
Anko unaonekana una hasira nae aisee, duh.

Hapana.

Sina hasira naye kabisa.

Zaidi ya kumsoma kwenye mitandao na kuona vi video vyake kadhaa kwenye YouTube, simjui na hanijui.

Na kwa kadri nijuavyo, hajawahi kunitukana.

Lakini, kwa jinsi ambavyo huwa anawatukana hao anaogombana nao, napata picha flani kuwa ni watu waoga na wadhaifu.

La sivyo, angekuwa keshalipata somo.
 
Hapana.

Sina hasira naye kabisa.

Zaidi ya kumsoma kwenye mitandao na kuona vi video vyake kadhaa kwenye YouTube, simjui na hanijui.

Na kwa kadri nijuavyo, hajawahi kunitukana.

Lakini, kwa jinsi ambavyo huwa anawatukana hao anaogombana nao, napata picha flani kuwa ni watu waoga na wadhaifu.

La sivyo, angekuwa keshalipata somo.

!
!
Huyu huwa anatukana hadi marehemu huyu. Hachagui huwa anatukana mno. Huyu dada ana vidole vichafu mno aisee daaah. Ila huyu Temu Hoyce aisee alimchafua mno.
 
Back
Top Bottom