Watanzania sita, wakiwemo wasanii wawili wa maigizo, wamefungwa Magereza mawili ya Hong Kong nchini China baada ya mahakama kuwakuta na hatia ya kujihusisha na biashara ya ukahaba, Ijumaa linakuwa la kwanza kukujuza.
Kwa mujibu wa chanzo chetu cha uhakika, wabongo hao, wamefungwa kwenye Magereza ya Lai Chi Kok na Tuemun ambayo ni maalum kwa wafungwa wanawake
Watanzania hao, ambao wanatumikia kifungo cha wiki sita gerezani ni Jack aliyewahi kuwa Muigizaji wa Kundi la Sanaa la Kidedea akijulikana kwa jina la Safina, Maua ambaye naye amewahi kuwa msanii wa maigizo (kundi halijajulikana) na Tina Mkongo aliye maarufu kwenye Club za Jolly na Ambiance za jijini Dar.
"Jack ni yule Safina
‘alikuwaga' Kidedea, tena hivi karibuni tu amecheza filamu ya ‘Inye', msanii mwingine anaitwa Maua, huyu sijui alikuwa kundi gani, na hao wengine niliokutajia," kilisema chanzo kimoja.
Wengine waliokamatwa katika awamu ya pili ya msako huo ni Esther Nyonyo, mwingine alitajwa kwa jina moja la Agness wa Mwanza na Diana maarufu kwa jina la ‘Joka Jeusi' wa jijini Dar es Salaam.
Hawa wote, habari zinasema, walidaiwa kufanya vitendo vya ukahaba kwenye klabu maarufu za Jiji la Hong Kong nchini humo, kitu kilichoelezwa kuwa ni kinyume cha sheria za nchi hiyo.
Klabu maarufu zinazofanyiwa operesheni hiyo ni pamoja na Traffic, Fenrick, Escape, Amazon, Bullidog, Club 29 na Zunk.
Hawa wote walikuwa wakifanyia mambo yao klabu zile kubwa kubwa kama nilivyozitaja, si unajua tena China kwa sasa wageni ni wengi tena wana fedha zao," kilisema chanzo.
Hivi karibuni ilidaiwa kuwa, Serikali ya China ilichoshwa na kukithiri kwa biashara ya ukahaba hivyo kukodisha kikosi maalum kutoka nje kwa lengo la kuitokomeza.
Kikosi hicho cha watu hamsini, kimetoka Scotland na Ireland ambapo inasemekana kimekuwa kikitekeleza operesheni yao kwa kujifanya wateja wa biashara hiyo na kuwanunua makahaba na kuwapeleka hotelini kwa lengo la kujiridhisha kwa ushahidi.
Habari zinasema zoezi hilo linaendelea licha ya makahaba wengi kukimbilia nchi jirani za Singapore na Malaysia kwa lengo la kujiokoa na ‘kamata kamata' hiyo.
Baadhi ya wasanii wa Bongo wanadaiwa kwenda China mara kwa mara kwa ajili ya kufanya biashara halali huku kukiwa na madai ya kujihusisha na biashara ya ukahaba pindi wanapokuwa nchini humo.
Jitihada za kuwapata Mawaziri wa Mambo ya Nchi za Nje wa Tanzania, Mhe. Bernard Kamilius Membe (pichani juu) na Yang Jiechi wa China zinaendelea ili kuzungumzia sakata hilo.:frog:
source:gpl