Baada ya Magufuli, 2025 Makonda atatufaa sana kwasababu ana uthubutu kuliko hata JPM!

Nadhani ni vizuri sasa waafrika na sisi tukawa huru kama wenzetu wazungu.
Yani nchi nyingi za kiafrika wananchi wanaishi kama wafungwa gerezani.

Viongozi wamepora haki za wananchi hata zile za kuyafurahia maisha na uhai waliopewa na Mungu.

Waafrika tumekosa kitu kimoja ambacho ni utu.

Viongozi wanapenda kuheshimiwa , kuitwa waheshimiwa , kuombwa kwa unyenyekevu hata pale ambapo wanatakiwa kutekeleza majukumu yao ambayo wameajiriwa na kulipwa kwa ajili hiyo lakini bado wanataka wapigiwe magoti.Hizi ndio nchi za kiafrika watawala ni kama miungu wapo juu ya katiba na kila kiumbe na roho za watu na ardhi .
Yani viongozi wa Afrika wana mamlaka kuliko hata Mungu muumba na cha ajabu tunawashabikia kwa kuona mateso ya watu wengine yanayotokana na maamuzi ya watawala yasiyo sahihi.

Wakati Afrika wananchi wakiwa wanawanyenyekea watawala wao hali ni tofauti kwa viongozi hao hao wanaopenda kuheshimiwa na kutukuzwa. Kwao kila kitu ni ubabe ,kiburi, kutoa amri za kukamata watu, kutosha watu, kufokea watu hadharani , kutoa lugha mbaya kwa watu wengine n.k.

Watawala wao wanatuambia kuwa wanainyoosha nchi lakini wao hawataki kunyooshwa na wananchi ambao ndio waajiri wao.

Yaani watawala wanawanyoosha wananchi kwa gharama za wananchi ili hali wao na familia zao hawataki kunyooshwa hata kwa kukosolewa.
Hawa ndio watawala wa kiafrika .

Utawala wa kimabavu duniani haukubaliki kwa kuwa wanaoumia sio watawala bali watawaliwa pekee.

Kiongozi asiyependa demokrasia hapendezi kabisa katika ulimwengu wa sasa.
Haitapendeza tena kuwarithisha watoto wetu nchi yenye watawala wenye hulka za kikoloni na unyapara. Hatutaki nchi ambayo wale walioko nje ya system wanakua kama watumwa.
Nchi ambayo wakubwa ni mabwana na wadogo ni watwana wanaodhalilishwa na hawana wa kukimbilia kwa kuwa mahakama nazo zinaingiwa na woga.
Nchi ambayo mwanasiasa anaweza kumwambia afisa elimu wafukuze walimu wakuu wote kwa sababu tu ya kushindwa kujibu maswali ya kisiasa.
Nchi ambayo wataalam wanaendeshwa kisiasa kwa manufaa ya wanasiasa.

Makonda namkubali sana lakini sio kwa nafasi ya juu sana.
Uwaziri wa Mambo ya ndani au Tamisemi,au Ujenzi au kilimo au ukuu wa mkoa wowote wenye maendeleo duni mbali utampendeza zaidi!
 
Tutakuwajje na marais wawili katika mtu mmoja: Daud Albert Bashite na Paulo Makonda? Tanzania imekuwa ya kuchezewa kirahisi kiasi hicho? Kulindwa kwake na rais hakuufuti ukweli kuwa ana jinai ya kufoji vyeti!!!!
 
Unasubiri iandikwe wapi? Watangulizi ndio wamelea udini, halafu utegemee waumini wakae kimya zamu yao ikifika?
Na hapo ndipo tutakapo jichanyanganya huyo bashite urais wake ni wa mkoa tu nchi wa nchi atausikia tu kwa wengine
 
Jamani naomba kuuliza "Hivi huyu mayalla aka njaa kwa kisukuma ana akili kweli?au kichwani mwake kuna nzi?"nitafurahi kupata majibu.!
 
Nimeipenda hii na mimi niliitaja hapa.
P
 
Huo ndo ukabila wenyewe
 
Kwanini usiwe wewe paskali, kwani wewe makonda amekuzidi nn, me naona hata wewe utatufaa sn kuliko hata makonda
 
Kassim Majaliwa anaonesha kuwa na COMPOSURE ya kutosha. Uzoefu serikalini, hekima, busara, weledi, hamuonei mtu. Hakurupuki. Mie naona atatufaa sana.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…