Baada ya Magufuli, 2025 Makonda atatufaa sana kwasababu ana uthubutu kuliko hata JPM!

Safari inaendelea Makonda ateuliwa kuwa Waziri wa Habari, Simbachawe atenguliwa Uwaziri wa Mambo ya ndani ya Nchi
P
 
Sawa, ila pasiwepo na utekaji, watu kupotea, na mauaji yanayofanywa na wasiojulikana. Ubabe ruksa kwa mambo ya kujenga nchi ila hayo mengine hayatatakiwa
 
Mwenyezi Mungu akitujalia uzima nitapiga kura yangu kwa mara ya pili baada ya kumchagua Magufuli 2015 na nitamchagua Paul Makonda kuwa Rais wa Tanzania.
 
UKIONA MABADILIKO YANAFANYIKA MARA KWA MARA SABABU NI MAJUNGU NA UMBEA ,KIONGOZI UKIWA UNASIKILIZA MAJUNGU BILA KUANGALIA KPI ZA UNAOWATEUA UTAISHIA KILA MWEZI KUVUNJA NA KUPANGA UPYA
 

Wampe Uwaziri Mkuu
 
Mzee baba, pascal unaonaga mbali! Hii makala ni ya siku nyingi uliandika, mjuba makonda anakikaribia kiti hicho, wamlinde tu na kashfa pamoja na zile ajali za kisiasa kuchafuliwa
 
Mwaka 2030 kuna watu watashangaa sana!
Hivi CCM ninyi matuchukuliaje watanzania.

Hivi mtu anakuwaje Jeuri na anajikuta mkubwa kuliko nchi na hatoki ofisini..
Watu hawafanani,kuna wengine wana Mungu na wengine wana shetani!

Huyu ni mpakwa mafuta ya upako wa Bwana,hivyo kama unasubiria atumbuliwe,utasubiri sana!Wale mnaosubiri kwa hamu Makonda atumbuliwe, mtasubiri sana!. Ukiwa ni mpakwa mafuta, ni mpakwa mafuta!

Muulize Mrisho Gambo kilichomkuta hapa Amini Nawaambieni , Pamoja na Mapungufu Yake Yote ya Kibinadamu, Mtu Huyu Ana Mungu Ndani Yake!, Anaongozwa na Roho wa Mungu!. Mshuhudie Hapa!.

Kwa taarifa yenu, hiki kilichotokea juzi kati hadi jamaa yetu yule tegemeo la 2030 akatema bungo!,ni huyu mwamba ndio aliliamsha akakomaa nae mpaka jamaa akasalimu amri!.

Pokea full dose ya maktaba yangu kumhusu huyu dogo!

Rejea za mtoa mada kuhusu Paul Makonda
  1. Nimemkubali Sana DC Makonda, anafaa kuwa Mkuu wa Mkoa Dar es Salaam
  2. Nikimwangalia Makonda, mambo anayoyafanya namuona kama Magufuli
  3. Bado kuna ubishi kuwa hiki ni chuma? Je, chuma hiki ni chuma kingine ila ni kama kile au chuma hiki ni kile kile kimerejea kivingine?
  4. Mafanikio ya Makonda ni Uthibitisho Wa Jiwe walilolikataa Waashi litafanywa kuwa Jiwe Kuu la Pembeni
  5. Baada ya Magufuli, 2025 Makonda atatufaa sana kwasababu ana uthubutu kuliko hata JPM!
  6. Madawa ya Kulevya: Kumbe Makonda Alizuiwa Kutaja Majina!. Anaamini Uwazi, Atunge By-Law Ataje Majina
  7. Wale mnaosubiri kwa hamu Makonda atumbuliwe, mtasubiri sana!. Ukiwa ni mpakwa mafuta, ni mpakwa mafuta!
  8. Kumbe ni Uongo, Uzushi, Fitna, Majungu, Wivu na Kijicho dhidi ya mafanikio yake! Makonda wapuuze
  9. Pascal Mayalla ampongeza Makonda kuteuliwa mwenezi NEC taifa. Ampigia simu kumpongeza
  10. Ndugu, jamaa na marafiki njooni tumtetee Makonda dhidi ya mapapa wauza unga wanaomzushia
  11. Pongezi Paul Makonda kuifufua CCM kwa amsha amsha. Twende mdogomdogo ngoma ikivuma sana inakaribia kupasuka!
  12. Makonda, only the truth will set you free!
  13. Je, wajua Rais aweza kuteua yeyote hata darasa la saba?. Teuzi hizi hazihojiwi popote na yeyote!
  14. Kutoa siri za Nchi nje ya Nchi ni Uhaini. Maofisa Hawa Wametoa Siri, Wakamatwe, Washitakiwe!
  15. Heko Rais Magufuli kwa msimamo thabiti. Shikilia hapo hapo. Kelele za Mlango Zisikukoseshe Usingizi!
  16. Je, Tanzania tunahitaji viongozi gani?. wajinga wachapakazi, au mangi meza wenye vyeti?.
Mzee Pasco
 
Learned brother unashabikia impunity?
Lawlessness?

Majitu yasiyoheshimu sheria ndio yanapigiwa madebe na maattorney wa kileo!!!!!!

Ukabila?
Mwenzenu?
Au ndo uchawa uliopitiliza?
 
Huyu mzee ni chawa afu kuna Uzi wa week iliyopita anajifanya kushangaa WHY waandish wa habar wako kimya,wakat yeye mwenyewe ni CHAWA PRO MAX ,huyu ni praise team na hana legacy tena,huyu na mzee mwenzie Dkt Ayub Rioba ni chawa na hawa aminiki tena 🗑🗑🗑
 
Pamoja kwamba ni wapoti mwenzangu, nasema. HAPANA!
HAFAI. HANA SIFA HIZO. HANA USTAARABU. HANA WEREVU WALA BUSARA. UWEZO WA KUJADILI AU KUTOA MAAMUZI MUHIMU. HAPANA HAPANA HAPANA!
 
Leo sasa ndo nimethibitisha pasipo na mashaka kua WAHUNI PIA MNAZEEKA NA MAYALA MAANA YAKE NJAA.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…