Baada ya Magufuli, TANESCO wanaanza kata kata ya umeme

Wakati wa magufuli umeme ulikua unakatika kama kawa. DSM walisingizia kunguru. Pale Moro sababu hapajawahi kuwekwa wazi
 
Acha kudanganya watu wewe.Una taarifa za nchi nzima au inaangalia ka eneo kako alafu unakuja na hitimisho.Umeme haujawai kuacha kukatika ovyo nchi hii ata kipindi cha Jpm bado ulikua ukikatika maeneo mbali mbali labda kama ulikua haupati taarifa tofauti na hapo ni majungu tu unataka kutuletea.
 
Hapa utambulia matusi hapa JF wengi wao ni Makamanda kindakindaki wa Mwendakiti Mbowe
 
Acha uongo weye
 
Nipo Mtwara wilaya za Mtwara,Masasi,Tandahimba na Newala tangu mwaka 2017,sioni tofauti ya kiwango cha huduma ya umeme wakati wa hayati na sasahivi.
 
huku arusha na moshi toka mwendazake amesepa mawinguni tumeshasahau mgao wa umeme
 
Acha unafiki wewe, toka mwaka jana wakati Magufuli yupo kuna thread zaidi ya 20 humu tunalalamika kukatika kwa umeme. Usitake kumtetea mtu anaeteketea motoni!
 
Itakuwa ni hujuma maana Mh Rais haja badilisha utawala hapa.
Bado ni Sukuma gang linaongoza hii wizara. Ndio maana tuna taka Mh. Rais abadili wafuasi wa mwenda zake wote.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…