Baada ya malalamiko mengi hatimaye barabara ya Mwanagati imemwagwa vifusi na kusawazishwa

Suley2019

JF-Expert Member
Joined
Oct 7, 2019
Posts
2,203
Reaction score
5,610
Salaam Wakuu,

Kwanza kabisa niwashukuru JamiiForums kwa kupaza sauti yetu ya ubovu wa barabara uliokuwepo kuanzia kipande cha Kwa Mpalange mpaka Mwanagati.

Barabara hii ilikuwa mbaya kupitiliza, ilikuwa ni ngumu sana kwa daladala kufanya kazi bila kuharibikiwa vyombo vyao mpaka walilazimika kupandisha kiwango cha nauli.

Hatimaye baada ya malalamiko yetu Soma: KERO - Barabara za Mwanagati hazipitiki msimu huu wa mvua. Magari yanaharibika. Daladala zinalazimika kupandisha nauli mamlaka husika zimesikia na kuleta kifusi na kusawazisha barabara hiyo. Kwa sasa barabara inapitika vizuri.

Asanteni sana.

PIA SOMA
- Baada ya kelele za Wananchi, barabara ya Mwanagati yaanza kutengenezwa

- Hali ya barabara kwa wakazi wa Mwanagati inasikitisha

Your browser is not able to display this video.




Your browser is not able to display this video.

Your browser is not able to display this video.
 
Barabara zote zimemwagwa lami hata huku chanika ni hivyo ilitengwa mabilioni kurejesha miundombinu kwenye hali nzuri baada ya mvua kubwa
2025-2030 Samia Suluhu Hassan anafaa sana
 
Hii barabara baado sana ikinyesha mvua tu hicho kifusi kwisha habari yake !
Wachimbe mifereji na kushindilia kifusi barabara yote
 
Miaka 60 ya uhuru, uchumi wa Kati bado tunajivunia Barabara ya matope?
Salaam Wakuu,

Kwanza kabisa niwashukuru JamiiForums kwa kupaza sauti yetu ya ubovu wa barabara uliokuwepo kuanzia kipande cha Kwa Mpalange mpaka Mwanagati...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…