Elections 2015 Baada ya Masheikh wa Bagamoyo, Wachungaji wamzamia Edward Lowassa kumuomba kugombea Urais

Elections 2015 Baada ya Masheikh wa Bagamoyo, Wachungaji wamzamia Edward Lowassa kumuomba kugombea Urais

John Okello

JF-Expert Member
Joined
Sep 24, 2014
Posts
459
Reaction score
207
Leo katika Hali isiyo ya kawaida wachungaji wavamia Eneo la Area D ambapo ni Makazi ya viongozi mbali mbali wakimsaka Edward Lowassa. viongozi hao wa dini walikuwa na shauku kubwa na nyuso za furaha wakiimba nyimbo za matumaini Mapya na Edward lowassa.

Aidha misururu hio imesababisaha Ndugu Samwel Sita kusubiri kwa Muda kupisha viongozi hao kwenda kuiona nuru ya MATUMAINI. pia ilimuwia vigumu ndugu Fredric Sumaye kuwahi appointments yake na Spika wa Bunge kupisha msafara takatifu kwenda Jirani yake Edward Lowassa.

Mambo yanazidi kupamba moto kuelekea nuru ya matumaini kwa Watanzania ambao mara zote wamuonapo Edward Lowassa hupata faraja.

Wachungaji hao wametabiri na kuahidi kunena kwa vitendo, na mpaka sasa bado wanaendelea kujieleza ni nini wanacho muahidi bwana Edward Lowassa kama balozi wamuaminiye katika safari ya MATUMAINI,

Nitaendelea kukujuza.

MAAMUZI NA MATUMAINI MAPYA NA EDWARD LOWASSA 2015.
ImageUploadedByJamiiForums1427101586.450986.jpg
ImageUploadedByJamiiForums1427101603.403622.jpg
 
y January Makamba Nafasi ya Urais ni nafasi ya hadhi na heshima kubwa. Unapoiomba hupaswi kufanya michezo ya kuigiza. Huu utaratibu wa kuratibu watu, kuwasafirisha, kuwapa posho na ubwabwa waje kukuomba kugombea ni michezo ya kuigiza ambayo ni aibu kubwa.

Kila mgombea ana uwezo wa kutengeneza WATU wa kumuomba kugombea lakini wengine hatufanyi hivi kwasababu tunaheshimu nafasi tunayoiomba na tunaamini kwamba haipaswi kutafutwa kwa ulaghai na maigizo.

Ni aibu sana kutumia shida na njaa za watu kisiasa. Ni aibu sana kukusanya vijana na wazee wa watu na kuwapangia viti na mahema na kuwapa pesa halafu pesa na kuwapiga picha. Ukiona mtu anatafuta nafasi ya uongozi kwa ujanja na ulaghai ujue atatawala kwa ujanja na ulaghai.

Viongozi wanaokubalika na watu hawangaiki kupanga Viti na mahema na kuwapiga picha watu wanaowakubali.

Mgombea anayehaha na kutumia pesa nyingi kuonyesha anakubalika ukweli ni kwamba hajiamini. Kama unakubalika huwezi kuratibu makundi na kuyalipa na kuwapiga picha na kuita waandishi wa habari waje kushuhudia. Hizo ni mbinu za mfa maji.

Naamini Chama changu hakitatishwa na nguvu za maigizo. Tunataka uongozi safi unaomuogopa mungu. Tunataka uongozi wenye uadilifu na fikra mpya za kuisogeza mbele Tanzania. Tunataka viongozi watakaomaliza shida za Watanzania sio wanaozitumia shida hizo kisiasa.

Hata Mzee Makamba, pamoja na umri wake wa miaka 75, leo akiwa na pesa za kumwaga anaweza kutengeneza makundi yakamuombe kugombea Urais.

Ifike mahali katika nchi yetu tuache hii michezo. Tukiendelea na mambo haya, tunatengeneza taifa linaloendeshwa kwa propaganda tu. Watu wanaotaka kuomba nafasi ya Urais wanapaswa kuwa na ujasiri na wanapaswa kujiamini na kusema wanataka nafasi hiyo na wana fikra gani mpya bila kutumia pesa kuonyesha kwamba wanagombea kwasababu wanahitajika na watu. Uongozi thabiti na shupavu hautokani na michezo ya kuigiza.

January Makamba

 
Sioni wa kumzuia Edo kuwa mgombea kwa ticket ya chama chake!... January, Sumaye, Sitta, Membe et al wajipime kisha wapite kuhesabiwa... Nyota ya Lowassa inang'aa...
 
Yaani mnajitekenya wenyewe na kucheka wenyewe halafu mnasema ni breaking newz wakati ni breaking uwizi wa macho.
 
Masaki

UMEKOSA BUSARA - Wacha watanzania wafanye wanayo yaona ni matumaini kwao�� Wewe kama nani kusema michezo ya kuigiza na una uhakika gani wa kufanya hivyo na kama ww unajua madhubuti siri hiyo ya watanzania kutoka sehemu mbalimbali kuwa wanaigiza basi tunaomba usiongee tu bila vielelezo vya msingi kuthibitisha kauli yako ya kuwapotosha watanzania.

Nilikuwa nikidhani upo vizuri kama kijana na unauwezo mkubwa wa kuchanganyua mambo kumbe bado una siasa kauli which is always detect that, Mr. Politician we don't do drama and listening into it ,but we need and we watch Actions that can run our TZ�� , let Mr. ENL awasikilize Watanzania na afuate nia yawatanzania, sio useme ni mchezo wa kuigiza , if u thnk so then Start your Movie now any am ready to buy each episode wth any currency ��, Thank you wisely am done.
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom