Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Go Lowassa go tukutane October ndio utatujuwa waTZ na Dr Slaa ni nani.
Maccm hayana mgombea zaid ya Lowassa
Makamba kaonge kweli tupu. Kwa hali ilivyo sasa ya watu kuusaka urais kwa njia mbali mbali zikiwa ni pamoja na kuwalipa watu ili waje kujifanya wanakuomba kugombea urais si ajabu tukaanza kuona misafara ya vyangu doa, mateja na mashoga wakilipwa ili kwenda kwa wagombea kuuaminisha umma ili uone kuwa wao wanafaa kuliko wenzao. Naomba siku ifike hao wote wanaowekeza urais kwa pesa na michezo michafu na ya kijinga kama hii waje kushikwa na mshangao kwa kuachwa hewani tuone hayo makundi kama yatawafuata tena. Kweli masikini hawana uhuru! Mimi naona makundi yote yanayokwenda kwa wagombea kwa kuandaliwa na kulipwa ni sawa na mazezeta waliojishushia utu na heshima yao. Walaaniwe wao na wagombea waoy January Makamba Nafasi ya Urais ni nafasi ya hadhi na heshima kubwa. Unapoiomba hupaswi kufanya michezo ya kuigiza. Huu utaratibu wa kuratibu watu, kuwasafirisha, kuwapa posho na ubwabwa waje kukuomba kugombea ni michezo ya kuigiza ambayo ni aibu kubwa.
Kila mgombea ana uwezo wa kutengeneza WATU wa kumuomba kugombea lakini wengine hatufanyi hivi kwasababu tunaheshimu nafasi tunayoiomba na tunaamini kwamba haipaswi kutafutwa kwa ulaghai na maigizo.
Ni aibu sana kutumia shida na njaa za watu kisiasa. Ni aibu sana kukusanya vijana na wazee wa watu na kuwapangia viti na mahema na kuwapa pesa halafu pesa na kuwapiga picha. Ukiona mtu anatafuta nafasi ya uongozi kwa ujanja na ulaghai ujue atatawala kwa ujanja na ulaghai.
Viongozi wanaokubalika na watu hawangaiki kupanga Viti na mahema na kuwapiga picha watu wanaowakubali.
Mgombea anayehaha na kutumia pesa nyingi kuonyesha anakubalika ukweli ni kwamba hajiamini. Kama unakubalika huwezi kuratibu makundi na kuyalipa na kuwapiga picha na kuita waandishi wa habari waje kushuhudia. Hizo ni mbinu za mfa maji.
Naamini Chama changu hakitatishwa na nguvu za maigizo. Tunataka uongozi safi unaomuogopa mungu. Tunataka uongozi wenye uadilifu na fikra mpya za kuisogeza mbele Tanzania. Tunataka viongozi watakaomaliza shida za Watanzania sio wanaozitumia shida hizo kisiasa.
Hata Mzee Makamba, pamoja na umri wake wa miaka 75, leo akiwa na pesa za kumwaga anaweza kutengeneza makundi yakamuombe kugombea Urais.
Ifike mahali katika nchi yetu tuache hii michezo. Tukiendelea na mambo haya, tunatengeneza taifa linaloendeshwa kwa propaganda tu. Watu wanaotaka kuomba nafasi ya Urais wanapaswa kuwa na ujasiri na wanapaswa kujiamini na kusema wanataka nafasi hiyo na wana fikra gani mpya bila kutumia pesa kuonyesha kwamba wanagombea kwasababu wanahitajika na watu. Uongozi thabiti na shupavu hautokani na michezo ya kuigiza.
January Makamba
Poor wachungaji! Wamenena kwa lugha?View attachment 237107
View attachment 237108
Leo katika Hali isiyo ya kawaida wachungaji wavamia Eneo la Area D ambapo ni Makazi ya viongozi mbali mbali wakimsaka Edward Lowassa. viongozi hao wa dini walikuwa na shauku kubwa na nyuso za furaha wakiimba nyimbo za matumaini Mapya na Edward lowassa.
Aidha misururu hio imesababisaha Ndugu Samwel Sita kusubiri kwa Muda kupisha viongozi hao kwenda kuiona nuru ya MATUMAINI. pia ilimuwia vigumu ndugu Fredric Sumaye kuwahi appointments yake na Spika wa Bunge kupisha msafara takatifu kwenda Jirani yake Edward Lowassa.
Mambo yanazidi kupamba moto kuelekea nuru ya matumaini kwa Watanzania ambao mara zote wamuonapo Edward Lowassa hupata faraja.
Wachungaji hao wametabiri na kuahidi kunena kwa vitendo, na mpaka sasa bado wanaendelea kujieleza ni nini wanacho muahidi bwana Edward Lowassa kama balozi wamuaminiye katika safari ya MATUMAINI,
Nitaendelea kukujuza.
MAAMUZI NA MATUMAINI MAPYA NA EDWARD LOWASSA 2015.
Mi nikimwona mchungaji wangu humo kashika bango nahama kanisa
na Mwaka huu atajiuzulu tena. Mimi najua Sana.
View attachment 237107
View attachment 237108
Leo katika Hali isiyo ya kawaida wachungaji wavamia Eneo la Area D ambapo ni Makazi ya viongozi mbali mbali wakimsaka Edward Lowassa. viongozi hao wa dini walikuwa na shauku kubwa na nyuso za furaha wakiimba nyimbo za matumaini Mapya na Edward lowassa.
Aidha misururu hio imesababisaha Ndugu Samwel Sita kusubiri kwa Muda kupisha viongozi hao kwenda kuiona nuru ya MATUMAINI. pia ilimuwia vigumu ndugu Fredric Sumaye kuwahi appointments yake na Spika wa Bunge kupisha msafara takatifu kwenda Jirani yake Edward Lowassa.
Mambo yanazidi kupamba moto kuelekea nuru ya matumaini kwa Watanzania ambao mara zote wamuonapo Edward Lowassa hupata faraja.
Wachungaji hao wametabiri na kuahidi kunena kwa vitendo, na mpaka sasa bado wanaendelea kujieleza ni nini wanacho muahidi bwana Edward Lowassa kama balozi wamuaminiye katika safari ya MATUMAINI,
Nitaendelea kukujuza.
MAAMUZI NA MATUMAINI MAPYA NA EDWARD LOWASSA 2015.
Pesa za ufisadi zinafanya kazi. Waache waigize tu. Rais wa Tanzania hapatikani kwa njia za maigizo
ila mchungaji ndo kiongozi wa kanisawe vipi? Kwani kanisa ni la mchungaji!