Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Kwa hiyo unataka tuwaite 'enemies of simba'!?friends of simba wanaharibu timu
Mkuu grafani11 hapa sibonike kaelezea point ya msingi sana.NA HII NDIO ROOT CAUSE YA HAYA YOTE.
Tukitaka simba iwe timu inayoheshimika na yenye pesa na inayoendeshwa kisomi lazima ifanye kazi "independently".
Tusemezane ukweli......Viongozi wana maslahi yao binafsi.
Timu inahitaji aina mpya ya ufikiriaji...hawa waliopo kina Dewji wa Tangu enzi zile hakuna kipya.................
Mfumo wa uendeshaji inabidi ubadilishwe
TATIZO NI...NANI MWENYE UWEZO WA KUWAWEKA HAWA MATAJIRI PEMBENI?
naomba mungu angalau tumalize nafasi ya kumi na mbili ilimradi tuweke record ambayo haijawahi kuwekwa na SIMBA kwa muda murefu.
Nakubaliana na maoni yako yote isipokua hili la "Wenye Pesa"
Simba iko na hali mbaya kwa sasa kwa sababu ya kuwategemea hawa "Wenye Pesa"
Kuna kipindi hawa wenye pesa hawakuwepo kwenye timu na timu ilifanya vizuri sana....hebu tumuulize Masuke kipindi cha Kaduguda simba ilikuwaje?
Simba inatakiwa ijisimamie kama timu...kwa pesa za timu...isitegemee mtu...hapo tunaweza kwenda proffesionally
Ni wanachama wenyewe. Sisi ndio tunachagua viongozi. Kwa njaa zetu (baadhi) tunachagua baada ya kupewa pipi ! (ndio pipi maana sina namna nyingine ya kueleza).
Angalia mfumo wa Spain (Barcelona na Real Madrid) ni tofauti na Uingereza ambako ni kampuni per se. Kule Spain wanachama (wanajitambua) ndio hupiga kura kupata viongozi - Rais wa Club ambaye huajiri watendaji.
Mfumo huu wa sasa wenye madhara makubwa utaendelea hadi wanachama wa vilabu tujitambue na kuweka viongozi wataosaidia kuleta mfumo bora. Najua tuna safari ndefu. Siku ya uchaguzi ndio matapeli yanawalipia wanachama kadi zao ili waweze kupiga kura ya kuwachagua!
Kila mwana Yanga au simba akichanga fee ya mwaka kwa Tanzania nzima, club inapata kiasi gani? Ongeza udhamini (TBL, Tv nk ) na viingilio. Hapo kuna haja ya kumpigia mtu magoti?
Precise
Lakini pia how if timu ikiuza shares 50% ika raise funds za kutosha .Kwa value ya shares za simba najua IPO yake itatengeneza billions.
Hizo billions zinaweza kutumika kufinance projects nyingi za timu
Hio 50% inaweza kufanya majority shareholder awe na say katika timu.
50% zinazobaki zinaweza kumilikiwa na wanachama.
Issue hapa ni kuifanya timu ijiendesh yenyewe.
Kama ulivyosema michango tu na fedha za wadhamini zinatosha kulipa mishahara yote ya mwaka mzima na kambi ya timu kwa mwaka mzima...sasa iweje waseme timu haina hela?
Kipindi cha Kaduguda mchango mkubwa wa kifedha ulikuwa unatolewa na Dioniz Malinzi, kaka yake Jamal Malinzi. Nadhani kwa sasa ni m/kiti wa BMT. Sina hakika sana kama alikuwa anasaidia tu for good faith au alikuwa mfadhili, sikuwahi kuona jezi imeandikwa Cargo Stars. Na wakati ule kama kumbukumbu zangu ziko sawa kuna ama Simba Cement ama NBC waliinject hela yao pale. Mambo hayakuwa mazuri sana ila tatizo lilikuwa ni hawa jamaa wa FoS na vyombo vya habari, walikuwa hawapatani na Kaduguda.
Ndio maana nikasema ni 'brilliant idea' mkuu. Ni sawa na kumpatia mtu gari katika nchi ambayo magari hayajawahi kuwepo kabisa, hakuna barabara, spare parts, mafundi, petrol stations nk. Kibaya zaidi hii gari uchomoe hata matairi alafu unamwachia mtu kwa ajili ya matumizi katika mazingira hayo hayo. Kuna gap kubwa hapa kati ya gari aliyoachiwa mtu na mtumiaji mtarajiwa. Huo ndio ukubwa wa hizi timu na wanachama wake.
Mfano wa timu hizi ni pale Mengi alipotumia muda mwingi sana sio kama mwanachama bali kama mjuzi wa biashara kuwapiga msasa Yanga ni jinsi gani wangeliweza kuibadili timu kutoka kwenye 'uombaomba' mpaka kwenye kugawana dividends za shares. Ni chini ya 5% ya waliomuelewa alichokuwa anawaeleza kabla na yeye kuamua 'kujitoa'. Kumbuka Mengi huyu huyu (forget about his negative side of life maana ni binadamu) alipoleta wazo la SKUVI miaka ya 90 mwanzoni, wengi wetu hatukuelewa alichokuwa akiaddress lakini nasikia kuna baadhi ya waliomsikiliza na sasa hivi ni matajiri wakubwa katika miradi ile ile aliyowaelekeza.
Samahani kutumia mfano wa mtu mmoja lakini nia yangu sio kumsifu bali kukuonyesha jinsi watu wanaojiita 'wanachama' wa Simba/Yanga walivyo wagumu kubadilika ili nawe ujue kitu unachokiongea cha kuleta mabadiliko kilivyo kigumu huko!
Kipindi cha uongozi wa Rage ni mara ngapi alikuwa anazikimbia mechi za Simba 2napotaka kucheza na Yanga? Tena wakati mwingine anaenda nje ya nchi kabisa na kuiacha timu ikikabiliwa na khali ngumu ya kifedha madeni kwa wachezaji na ikikabiliwa na mchezo muhimu dhidiya Yanga. Ni hawa hawa kina HP ndo walikuwa wanasimamia kambi ya timu, kulipa madeni ya wachezaji na hatimae 2nafurahia ushindi wote pamoja dhidi ya mtani wetu au anafurukuta anapata sare.
Kama kuna mtu alikuwepo Taifa siku ile game ya 3-3 na Yanga, kabla ya game Manji alisimama alikuwa na Sanga akawanyanyua wana Yanga akawa anaonyesha vidole vi3 na Yanga wakalipuka sana sie tukanywea kabisa hadi alipoibuka HP nae akatuinua wanasimba akaonyesha vidole vi5 tukalipuka mara mbili yao, mnakumbuka? Rage alikuwa wapi siku ile?
Watu wanaweza kuwa wanafanya vitu kwa good faith but changamoto ni nyingi mno katika soka la sasa, kila timu inawezeshwa hivyo zinajiandaa kikamilifu.
Kaburu nasikia hana mawe siku hizi, hivyo hatoi hela pale SSC.
Tayari kocha kamtaja Kaburu kuwa ndiye anayempigiaga simu kumwambia wachezaji wa kuwapanga, kocha alitishia kuacha kazi au kumtukana kiongozi yeyote atakayefanya hivyo. Source: Bin Zubeiry(naiamini souce)