MwanaDiwani
JF-Expert Member
- Mar 22, 2013
- 5,536
- 2,266
Wakati wakisusia Bunge Maalum la Katiba, Mwenyekiti wa CUF, Profesa Ibrahim Lipumba alikaririwa akisema, Ukawa hatuwezi kuendelea kushiriki dhuluma dhidi ya wananchi kwa kupitisha Katiba ambayo ni kinyume cha matakwa yao.
Madai hayo hayakuishia kwa Prof. Lipumba pekee. Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe naye pia alikaririwa akisema,Hoja ya msingi ni kwamba, vikao vinavyoendela Dodoma ni batili. Viko kinyume cha mchakato ulioasisiwa kwa misingi ya shirikishi na vinaakisi ubabe, dharau na kejeli za viongozi kwa Watanzania,.
Aliendelea kusema, Vikao hivyo ni kama michezo ya kitoto ya kujitekenya na kucheka wenyewe, Mbowe alisema ikifanikiwa kupata Rasimu ya Katiba itakayopendekezwa kuwa Katiba na hata ikipitishwa kwa kura ya maoni kuwa katiba mpya, wao wataendelea kudai katiba bora.
Habari zaidi inapatikana hapa,
Kama hiyo haitoshi, Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe (pichani), alitangaza maandamano na migomo isiyokoma nchi nzima kushinikiza kuvunjwa Bunge Maalumu la Katiba, kwa madai kwamba limekuwa likitafuna fedha za umma huku wakijua kwamba Katiba haiwezi kupatikana.
Habari zaidi iko hapa,
Mantiki ya hoja inatueleza kuwa, viongozi wakuu wa vyama vya CUF na CHADEMA au UKAWA kwa ujumla wao walishafuta yale yote yaliyokuwa au yanayoendelea kufanywa ndani ya Bunge Maalum na matokeo yake yote. Kwa lugha rahisi, UKAWA hawalitambui Bunge Maalum na maamuzi yake pamoja na kwamba sheria ya nchi inalitambua, hii ni pamoja na maamuzi yake linayofanya bila uwepo wa kikundi kinachojiita UKAWA.
Kinachoshangaza ni kuanza kuwasikia viongozi wa UKAWA wakilalamikia upigaji wa kura na matokeo ya kura za kupitisha Rasimu ya Katiba ndani ya bunge ambalo wao wameishasema hawalitambui. Kwa lugha nyingine, UKAWA wanalalamikia matokeo wakati hata chanzo cha matokeo hawakitambui.
Kwa habari zaidi unaweza kusoma hapa,
Kama UKAWA walidhani kuna umuhimu wa kupiga kura na kusimamia zoezi la upigaji kura, kwa nini walisusa na wakaondoka bungeni?.
Ni hawa hawa UKAWA walikuwa kila siku wanasema wabunge wote waliobaki bungeni ni wanaCCM wanaotaka kuendeleza muundo wa Serikali mbili lakini cha kushangaza ni hawa hawa UKAWA kwa sasa eti wanalalamika matokeo ya kura za wajumbe waliokuwa wanawaita wanaCCM na pia wasaliti. Are they serious?
Hoja za UKAWA nazifananisha na mwanamme anayepinga hamtambui mwanamke fulani halafu huyo mwanamke anapojifungua mtoto, anaanza kuomba wafanye DNA ili afahamu kama mtoto ni wake. Hiki ni kichekesho!
Kuhoji matokeo ya kura wakati hawawatambui hata wapiga kura(wabunge) achilia mbali taratibu zilizotumika kupiga kura nakupatikana matokeo ni kichekesho kwa watu wenye fikra pevu.
Kama wao wameishajitoa kwenye Mchakato wa kupatikana kwa katiba mpya chini ya Sheria ya Mabadiliko ya Katiba, Sura ya 83, basi inabidi wakae kimya au waanze kudai Mchakato mwingine nje ya huu wa sasa kwa sababu wamedai wajumbe walioko bungeni wanachofanya kwa sasa ni kama wanajitekenya na kucheka wenyewe.
Tuliposema UKAWA hawafahamu wanachokisimamia baada ya kususia Bunge Maalum, kuna baadhi ya watu hawakutuelewa.
Huhitaji kuwa political analyst kuelewa kuwa UKAWA is all over the place. Kwa sasa hata ukiwauliza suala la maandamano na migomo limefikia wapi, huwezi hata kupata jibu.
Tumeanza kuona hata jina la UKAWA limeanza kufutika!.