Baada ya matokeo ya kura bungeni, UKAWA waendelea kuhaha

Baada ya matokeo ya kura bungeni, UKAWA waendelea kuhaha

Bado tuna safari ndefu, na ipo siku tutafika hata 2090 poa tu. Ila UKAWA and the likes sio wa kutuongoza kufika hapo. We are better than that. Kuna watu wana imani kabisa kuwa UKAWA ndo mkombozi wa hili taifa! Inafurahisha sana. Tusichanganye vitu. Naona hamu ya wengi ni bora mabadiliko tu, badala ya kutaka mabadiliko bora.
 
Ndugu,
Mimi sikuwa msimamizi wa kura na kwa maana hiyo, sifahamu lolote zaidi ya official results kama zilivyotolewa bungeni.

Ingefaa uwaulize zaidi hao wanaotoa hayo madai labda wana majibu yatakayo waondoa wasiwasi.

Kwa sababu uko CCM huwezi kujiuliza maswali magumu kama hayo...wewe unapokea tu unachoambiwa.....eti official results...My foot
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Muafaka upi unaozungumzia hapa? Wa kuongeza kinyemela idadi ya wajumbe toka Zanzibar toka 212 hadi 219!? Hao wajumbe 7 zaidi mmewatoa wapi? Ukiondoa kura za ndiyo za hao wajumbe 7 hewa hiyo 2/3 ili kupata akidi haijatimia.

Hivi definition NZURI ya kuwa na MUAFAKA ni nini zaidi ya kupata 2/3 ya wawakilishi wa kitaifa?
 
Unajua sana kuandika,ila hujui kama hujui,wewe ndiyo hufahamu unachokiandika,na kama wewe ni kada wa ccm,nakuambia hivi siku zote Uhuru haupatikani ghafla,taratibu tutakuja kuwa huru,ni ukweli usiopingika hii Katiba imepitishwa kwa nguvu tu,polisi,pesa na vitisho vimetumika sana,kama unaakili timamu hili unalijua,ni ushabiki tu unasababishwa na njaa ndiyo unaokusumbua.watanzania wote wameona nakusikia,na wanalaani kabisa vitendo hivi vya ccm et al.
Freedom is coming soon.
Freedom for what? Are you among the few Tz who has been completely brainwashed by Mr. Zero a.k.a Mbowe? Don't be stupid, if they had good intention, they would have remained in the Bunge so that we (wananchi) could hear, listen and support their stand on the issues that are touching. Otherwise the Intarahamwe guy (delusional professor a.k.a Li-Pumba) contended that we move out of the bunge and fight for wananchi right while outside. This country is full of idiot politicians who only mind about their own stomach. CCM will always be there!
 
unnamed-8-564x272.jpg

Wakati wakisusia Bunge Maalum la Katiba, Mwenyekiti wa CUF, Profesa Ibrahim Lipumba alikaririwa akisema, “Ukawa hatuwezi kuendelea kushiriki dhuluma dhidi ya wananchi kwa kupitisha Katiba ambayo ni kinyume cha matakwa yao.”

Madai hayo hayakuishia kwa Prof. Lipumba pekee. Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe naye pia alikaririwa akisema,“Hoja ya msingi ni kwamba, vikao vinavyoendela Dodoma ni batili. Viko kinyume cha mchakato ulioasisiwa kwa misingi ya shirikishi na vinaakisi ubabe, dharau na kejeli za viongozi kwa Watanzania,”.

Aliendelea kusema, Vikao hivyo ni kama michezo ya kitoto ya kujitekenya na kucheka wenyewe, Mbowe alisema ikifanikiwa kupata Rasimu ya Katiba itakayopendekezwa kuwa Katiba na hata ikipitishwa kwa kura ya maoni kuwa katiba mpya, wao wataendelea kudai katiba bora.

Habari zaidi inapatikana hapa,

Kama hiyo haitoshi, Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe (pichani), alitangaza maandamano na migomo isiyokoma nchi nzima kushinikiza kuvunjwa Bunge Maalumu la Katiba, kwa madai kwamba limekuwa likitafuna fedha za umma huku wakijua kwamba Katiba haiwezi kupatikana.

Habari zaidi iko hapa,

Mantiki ya hoja inatueleza kuwa, viongozi wakuu wa vyama vya CUF na CHADEMA au UKAWA kwa ujumla wao walishafuta yale yote yaliyokuwa au yanayoendelea kufanywa ndani ya Bunge Maalum na matokeo yake yote. Kwa lugha rahisi, UKAWA hawalitambui Bunge Maalum na maamuzi yake pamoja na kwamba sheria ya nchi inalitambua, hii ni pamoja na maamuzi yake linayofanya bila uwepo wa kikundi kinachojiita UKAWA.

Kinachoshangaza ni kuanza kuwasikia viongozi wa UKAWA wakilalamikia upigaji wa kura na matokeo ya kura za kupitisha Rasimu ya Katiba ndani ya bunge ambalo wao wameishasema hawalitambui. Kwa lugha nyingine, UKAWA wanalalamikia matokeo wakati hata chanzo cha matokeo hawakitambui.

Kwa habari zaidi unaweza kusoma hapa,

Kama UKAWA walidhani kuna umuhimu wa kupiga kura na kusimamia zoezi la upigaji kura, kwa nini walisusa na wakaondoka bungeni?.

Ni hawa hawa UKAWA walikuwa kila siku wanasema wabunge wote waliobaki bungeni ni wanaCCM wanaotaka kuendeleza muundo wa Serikali mbili lakini cha kushangaza ni hawa hawa UKAWA kwa sasa eti wanalalamika matokeo ya kura za wajumbe waliokuwa wanawaita wanaCCM na pia wasaliti. Are they serious?

Hoja za UKAWA nazifananisha na mwanamme anayepinga hamtambui mwanamke fulani halafu huyo mwanamke anapojifungua mtoto, anaanza kuomba wafanye DNA ili afahamu kama mtoto ni wake. Hiki ni kichekesho!

Kuhoji matokeo ya kura wakati hawawatambui hata wapiga kura(wabunge) achilia mbali taratibu zilizotumika kupiga kura nakupatikana matokeo ni kichekesho kwa watu wenye fikra pevu.

Kama wao wameishajitoa kwenye Mchakato wa kupatikana kwa katiba mpya chini ya Sheria ya Mabadiliko ya Katiba, Sura ya 83, basi inabidi wakae kimya au waanze kudai Mchakato mwingine nje ya huu wa sasa kwa sababu wamedai wajumbe walioko bungeni wanachofanya kwa sasa ni kama wanajitekenya na kucheka wenyewe.

Tuliposema UKAWA hawafahamu wanachokisimamia baada ya kususia Bunge Maalum, kuna baadhi ya watu hawakutuelewa.

Huhitaji kuwa political analyst kuelewa kuwa UKAWA is all over the place. Kwa sasa hata ukiwauliza suala la maandamano na migomo limefikia wapi, huwezi hata kupata jibu.

Tumeanza kuona hata jina la UKAWA limeanza kufutika!.

Unajua jana niliona bandiko la professor Kitila alinifurahisha sana. Wanasiasa nadhani hawajitambui. Ila mi ninayemshangaa tu ni limpumba hivi alitumia makalio au kichwa? kuwaita wenzake intarahamwe then na kutoka bungeni kwa kitu ambacho mpaka sasa watanzania tunayo katiba na imepita.
 
Ndugu, Tundu Lissu amewaingiza ''mjini''. Wamejikuta wananunua ''matango pori'' ya kisiasa.

Tundu Lissu anadhani kila suala la kisiasa linapata majibu kwa njia ya uanaharakati.

Kwa sasa wamegonga kisiki kwenye Mchakato wa Katiba.

Maandamano na migomo waliyoitisha imedharauliwa na wananchi wapenda taifa endelevu.

Eti wanashangaa kwa nini 2/3 imepatikana kwa upande wa Zanzibar .

Watanzania wengi hawaendeshwi kwa fikra za kibinafsi. Wajumbe wameamua kupiga kura za ndiyo kutokana na msukumo wa kitaifa katika msingi wa maridhiano kati ya Tanzania bara na Zanzibar.

Tunaomba pia hata kwenye kura za maoni waendelee kususa na kugoma kupiga kura.

Chura wa kisiasa hawezi kumzuia tembo wa kisiasa kunywa maji.
 
Ndugu,
Nadhani wewe hauishi Tanzania.

Kwa sasa Katibu Mkuu na timu yake yuko vijijini akikagua uhai wa chama na itekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi.

Jaribu kufuatilia mikutano yake ili upate jibu mbadala achilia mbali chaguzi zilizofanyika hivi karibuni za madiwani, na wabunge wa Kalenga na Chalinze.

Karibu Tanga kwenye ziara ya Katibu Mkuu ili ujionee mwenyewe.
Nimehudhuria asilimia zaidi ya 75 ya mikutano ya hadhara aliyoifanya Kinana alipokuwa mkoa wa Pwani ndugu yangu, nimeshuhudia jinsi wanachama wenu wanavyosafirishwa kwa malori na DCM ili akidi ya uwanjani itimie.
 
Ningekuelewa kama ungesema wanalazimishwa kwenda kwenye mikutano.

Kama kuna watu wana uwezo wa kutoa usafiri, tatizo hapa ni nini?.

Ulitaka watembee kwa miguu wakati wana usafiri.

Hata kwenye chaguzi ndogo za Kalenga na Chalinze walikuwa wanasafirishwa kwenye magari kwenda kwenye mikutano na kupiga kura ili kutimiza akidi!. Nadhani matokeo unayafahamu.

Hata kwenye chaguzi za madiwani walikuwa wanasafirishwa ili
Kutimiza akidi ya uwanjani!. Nadhani matokeo ya chopa 3 madiwani 3 unayafahamu.

Endeleeni kuishi katika nchi ya kufikirika wakati CCM inaishi katika uhalisia kama matokeo ya chaguzi mbali mbali yanavyobainisha.
 
Only in Tanzania fisadi aliyesababishia hasara nchi ndiye anayeandika rasimu ya katiba!
 
Wakati wakisusia Bunge Maalum la Katiba, Mwenyekiti wa CUF, Profesa Ibrahim Lipumba alikaririwa akisema, “Ukawa hatuwezi kuendelea kushiriki dhuluma dhidi ya wananchi kwa kupitisha Katiba ambayo ni kinyume cha matakwa yao.”

Madai hayo hayakuishia kwa Prof. Lipumba pekee. Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe naye pia alikaririwa akisema,“Hoja ya msingi ni kwamba, vikao vinavyoendela Dodoma ni batili. Viko kinyume cha mchakato ulioasisiwa kwa misingi ya shirikishi na vinaakisi ubabe, dharau na kejeli za viongozi kwa Watanzania,”.

Aliendelea kusema, Vikao hivyo ni kama michezo ya kitoto ya kujitekenya na kucheka wenyewe, Mbowe alisema ikifanikiwa kupata Rasimu ya Katiba itakayopendekezwa kuwa Katiba na hata ikipitishwa kwa kura ya maoni kuwa katiba mpya, wao wataendelea kudai katiba bora.

Habari zaidi inapatikana hapa,

Kama hiyo haitoshi, Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe (pichani), alitangaza maandamano na migomo isiyokoma nchi nzima kushinikiza kuvunjwa Bunge Maalumu la Katiba, kwa madai kwamba limekuwa likitafuna fedha za umma huku wakijua kwamba Katiba haiwezi kupatikana.

Tuliposema UKAWA hawafahamu wanachokisimamia baada ya kususia Bunge Maalum, kuna baadhi ya watu hawakutuelewa.

Huhitaji kuwa political analyst kuelewa kuwa UKAWA is all over the place. Kwa sasa hata ukiwauliza suala la maandamano na migomo limefikia wapi, huwezi hata kupata jibu.

Tumeanza kuona hata jina la UKAWA limeanza kufutika!.
3rd October 2014 07:37

Kesho kutwa itakuwa mwaka umeisha na shauri UKAWA waweke sherehe /shughuli ya kuadhimisha Mwaka Mmoja toka waamue kutoka Bunge Maalumu la KATIBA kwa kutetea KATIBA YA WANANCHI kwa kufanya tathimini- na shughuli maalumu ya kuhamasisha wananchi.

Back
Top Bottom