Baada ya matokeo ya kura bungeni, UKAWA waendelea kuhaha

poleni sana ukawa waswahili wanasema heri ya mchawi kuliko mnafiki mmeshindwa hoja kwenye kamati mnaanza kusumbua watu
 
Ndugu,
Mimi ni MwanaDiwani.

By the way, nani alikudanganya kuwa kada wa CCM ndiyo wasimamizi wa zoezi la upigaji wa kura ndani ya Bunge Maalum?.

Soma Sheria ya Mabadiliko ya Katiba, Sura ya 83 katika Ibara ya 22(1a-c) kuhusu muundo wa Bunge Maalum ili upate jibu lako.
 
Mbowe,slaa,lipumba,mbatia wote wametoka nduki na kutokomea.
Wamewaachia mnyika na mtatiro ambao wanapelekwa kama tiara katika tufani(tornado)............namnukuu MIZENGO PINDA"""muda wa kuwachekea wahaini na wavunja amani umepita, tutatumia nguvu zetu zooote kupambana nao na kuwaangamiza""""""
 
Kwa jinsi hali ilivyo huku mitaani kwasasa, kuitetea CCM inakubidi uwe na roho kama ya kichaa. Mtaishia kuandika makala tu huku jf, uswahilini watu hawawaelewi. Hata mtoto mdogo anajua mmechakachua katiba.
 
Kura kwa Fax & Email ? CCM sasa mnataka kulibinafisha taifa letu liwe mali ya Lumumba!!
 
MwanaDiwani mnahangaika nini na UKAWA nyinyi mmefanikiwa mlichokuwa mnataka, kelele za nini? Achaneni na UKAWA songeni mbele katika kuliangamiza taifa la Tanganyika na Zanzibar. Kazi ya ghiriba, Ubabe, Kubadili kanuni ili ziendane na mnachotaka ni hatua kubwa mno na mmefanikiwa, hatua inayofuata ni rahisi sana kwenu maana Watanzania ni wapole sana, hawajui siasa na hata wanaojua hujifanya hawajui mkiwapa elfu mbilimbili na T-shirt watapiga tu kura za ndiyo. Nawatakieni sherehe njema muendelee kula Keki ya Tanganyika na Zanzibar kiulaiiiiiiini.
 
No easy walk to freedom .
Freedom fighters never give up.
Struggling man never come down.
The freedom is not too far.
 
poleni sana ukawa waswahili wanasema heri ya mchawi kuliko mnafiki mmeshindwa hoja kwenye kamati mnaanza kusumbua watu

Ndugu,
Hawa UKAWA walilikimbia bunge na kuwaita waliobaki bungeni ni wasaliti, eti kwa sasa wanalalamika kura zimechakachuliwa. Sijui walidhani nani atazisimamia wakati wao wamesusa.

Watu wenye hekima na busara waliwashauri warudi bungeni lakini wakadhani wao ndiyo alfa na omega kwenye Mchakato wa Katiba.

Matokeo yametoka, wanaanza kutoa matamko kama ilivyo jadi yao.

Waliitisha migomo na maandamano, wananchi wakawapuuza.
 
Kwa jinsi hali ilivyo huku mitaani kwasasa, kuitetea CCM inakubidi uwe na roho kama ya kichaa. Mtaishia kuandika makala tu huku jf, uswahilini watu hawawaelewi. Hata mtoto mdogo anajua mmechakachua katiba.

Ndugu,
Nadhani wewe hauishi Tanzania.

Kwa sasa Katibu Mkuu na timu yake yuko vijijini akikagua uhai wa chama na itekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi.

Jaribu kufuatilia mikutano yake ili upate jibu mbadala achilia mbali chaguzi zilizofanyika hivi karibuni za madiwani, na wabunge wa Kalenga na Chalinze.

Karibu Tanga kwenye ziara ya Katibu Mkuu ili ujionee mwenyewe.
 

Unajua sana kuandika,ila hujui kama hujui,wewe ndiyo hufahamu unachokiandika,na kama wewe ni kada wa ccm,nakuambia hivi siku zote Uhuru haupatikani ghafla,taratibu tutakuja kuwa huru,ni ukweli usiopingika hii Katiba imepitishwa kwa nguvu tu,polisi,pesa na vitisho vimetumika sana,kama unaakili timamu hili unalijua,ni ushabiki tu unasababishwa na njaa ndiyo unaokusumbua.watanzania wote wameona nakusikia,na wanalaani kabisa vitendo hivi vya ccm et al.
Freedom is coming soon.
 

Ndugu Bujigile
Hakuna mwananchi makini anayehangaika na UKAWA bali UKAWA ndiyo wanahangaika na yale yanayofanywa na watanzania wapenda taifa endelevu.

Inashangaza wanasusa Bunge Maalum halafu wanabakisha macho na masikio kwa yanayoendelea bungeni.

Wao kama wamesusa, basi waachame na mambo yote ya Bunge Maalum.
 
Wajinga hawa jamaa. Hivi nani aliwaambia watoke?

Ndugu,
Hizo zilikuwa ni mbinu zilizoundwa na Tundu Lissu.

Tundu Lissu alishasema yeye ni Mwanaharakati, na kama inavyofahamika, Tundu Lissu ndiyo think tank ya CHADEMA. Ndiyo maana sera ya CHADEMA kwa sasa ni Matamko, Maandamano na migomo/kususa.
 
Hivi definition NZURI ya kuwa na MUAFAKA ni nini zaidi ya kupata 2/3 ya wawakilishi wa kitaifa?
 
Insanity: doing the same thing over and over again and expecting different results.
Albert Einstein

UKAWA please wake up!

Ndugu,
Please, We just don't want them to wake up!.

Let the one who does right continue to do right; and let UKAWA continue to be holy!.
 
Hivi definition NZURI ya kuwa na MUAFAKA ni nini zaidi ya kupata 2/3 ya wawakilishi wa kitaifa?

Ndugu Kasheshe,
Muafaka katika muktadha wa Bunge Maalum ni kukubali matakwa ya UKAWA.

Ukiyakataa unaitwa MSALITI!.
 
mtu mjinga tu ama mchumia tumbo ndiye anaweza kusapoti rasimu ya CHENGE na SITTA basi ule mle ni ujinga mtupu
hata hili la UWAZI
UZALENDO
UWAJIBIKAJI kwako wewe si chochote?
Ndugu,
Masuala unayoyagusia yako kwenye Sura ya Kwanza, Ibara ya 6 ya Katiba inayopendekezwa.

Ibara hiyo inasema hivi,

 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…