Idugunde
JF-Expert Member
- May 21, 2020
- 6,404
- 6,969
Nauliza hili swali kama raia wa kawaida ambae nimepigwa butwaa na nini kimetokea kwenye matokeo ya kura za maoni za chama tawala nchini Tanzania.
Kila mtu haamimi nini kilitokea Kawe, Kigamboni na Kyela. Yaani jimbo la Kawe Gwajima, Paschal Mayalla, kipi na vigogo kibao waligaragazwa na Kijana asiyekuwa na jina. Kigamboni kila mtu amejionea kwa macho.
Huko Kyela, Dkt. Harrison na uwezo wake wote wa kuongea kwa kujiamini nae amekula mzinga! Na hawa ambao walitoka upinzani na kujiunga na CCM nao wamelamba mchanga!
Lakini tuachane na hayo kuna hii minog'ono inayoibuka kuwa huenda CCM ikagawanyika kama mwaka 2010. Maana kuwakata walioshika namba moja bila sababu za msingi kutaleta mpasuko mkubwa. Mfano ni mwaka 2010 David Mwakalebela alishinda kura za maoni Iringa mjini,jina likakatwa na Monica akapewa nafasi,kilichofuata Chadema ikachukua jimbo.
Sasa hata mwaka huu huenda yakajirudia yaleyale ya 2010. Maana kuwakata walioshinda kutaleta mpasuko na hasira kwa waliompitisha aliyekatwa. Labda tu advantage kwa CCM ni kuwa kwa sasa tofauti na 2010 upinzani upo hoi maututi.