Uchaguzi 2020 Baada ya matokeo ya kura za maoni, Je kuna uwezekano wa CCM kupata mpasuko?

Uchaguzi 2020 Baada ya matokeo ya kura za maoni, Je kuna uwezekano wa CCM kupata mpasuko?

Jana hili swala nililizungumzia nilileta uzi hapa hap unaosema kama wako mods wakaunganisha uzi na mwingine
Walifanya sio fair, huku uraiani ndio story za mjini. Wakikata waliochaguliwa watu wanalipa kisasi.
 
Idugunde,

Hata Sugu alishinda Mbeya sababu ya ccm kuwachagulia wamtakae na sio wagombea watakiwao na wananchi.
Wakirudia tena kosa imekula kwao.
Safari hii bungeni tupeleke vichwa sio ma ndio masifu mtu ili yashibe
 
Mwakyembe sio anaongea kwa kujiamini Bali kwa Majivuno.... Sasa anawaletea Majivuno wanyaki wamemnyoosha
 
Huko Kyela Dk Harrison na uwezo wake wote wa kuongea kwa kujiamini nae amekula mzinga! Na hawa ambao walitoka upinzani na kujiunga na CCM nao wamelamba mchanga!
Ukishakuwa na Jina, chunga Sana unachokitoa /unachokitamka Kwa watu, Mimi ni mfuasi wa Magufuli Ila sio CCM, nimefurahishwa Sana kwa Mwakyembe kupigwa Chini, ukiondoa uzuri wake wa mambo Fulani Kwa Taifa, Ila alifika mahali akawa anaongea vitu vya kuwadharau Sana wananchi hasa wanyonge

Haiwezekani, uwe msomi halafu ambao unawaongoza bila kujali elimu zao, wakikuuliza swali ni Hadi ujue kwamba aliyekuuliza anakiwango gani cha elimu?? Upuuzi
 
Kama upo hai utaonekana tu wala usiwe na hasira. Polisi wanaudhibiti vipi? CCM inapasuka mnashinda maana watalazisha kupitisha walioshindwa.
Rais kuzuia mikutano ya upinzani na kuacha ya ccm iendelee alitumia Sheria Gani? Mkutano ya ccm mpk maandamano ruksa, Ila upinzani hata ya ndani inaingiliwa na policcm, Unaona sawa? Unapambana na mwenzio ulingoni kafungwa kamba then unaruka ruka umempiga.

Je wewe tukuite mshindi katika mizani ya haki?au unaposema upinzani uko hoi unamaanisha nini? M/kiti wenu ni muoga wa ushindani. Historia yake iko hivyo. BISHA.
 
Upinzani hauko hoi subiri tarehe 26 mwezi wa 8 hadi otoba 27 utapata majibu
 
Back
Top Bottom