Baada ya Maximo sasa atafuata huyu!!!!!!!!

mkolaj

JF-Expert Member
Joined
Mar 24, 2014
Posts
3,023
Reaction score
1,089
Wakati pazia la ligi linafunguliwa kila kocha alijawa na matumaini ya timu yake kufanya vizuri katika harakati za kuchukua kombe, lakini wakati timu zimecheza mechi chache tu za ligi kuu hali ikawa mbaya kwa kocha wa timu ya NDANDA FC ya Mtwara ndugu Denis Kitambi kwa kufunguwa virago.

Mambo hayakuishia hapo tu yakamkuta kocha wa timu ya YANGA SC ya DAR ES SALAAM Marcio Maximo kwa kutupiwa virago baada ya timu hiyo kufungwa katika mechi ya bonanza maarufu kama "NANI MTANI JEMBE".

Naamin hali hii ya timua timua haitaishia hapo tu! na sasa itakuwa zamu ya Patrick Phiri wa timu ya SIMBA SC ya DAR ES SALAAM na hii ni kutokana na mwenendo wa timu hiyo wa kusua sua katika harakati za kupigania kombe la ligi kuu Tanzania bara (vpl).

Huo ni mtazamo wangu na wewe unaweza kutuambia wa kwako kuhusiana na hii timua timua ya makocha katika ligi ya Tanzania, baada ya Maximo huyu atafuata.
 
Kumfunga Yanga ndiyo mpango mzima. Hayo matokeo mengine sio issue!
 
Phiri yuko katika probation, ole wake afungwe au hata atoe sare katika mechii ijayo. Mashabiki na wanachama wa mikia wamekasirishwa na kitendo cha Ivo Mapunda kufungwa bao rahisi vile, wamemtaka kocha amtumie Manyika Jr maana wanaamini Mapunda ni Yanga, kama si uzembe wake wangeambulia sare kama kawaida yao. Phiri ajiandae kurejea Lusaka muda wowote ndani ya wiki 2 zijazo.
 
Mkuki kwa nguruwe kwa binadamu mchungu, hawakumbuki alichokuwa amefanya JUMA KASEJA kwenye mpambano wa nani mtani jembe ya mwaka jana alipotoa goal ya boko kwa yule mtoto wa mzee pazi!!!!
Ama kweli mtenda akitendewa hujihisi ameonewa...
 
weka sawasawa kumbukumbu zako
 
Mkolaj umekuja na kiswahili kipya hapa
 
Mkuki kwa nguruwe kwa binadamu mchungu, hawakumbuki alichokuwa amefanya JUMA KASEJA kwenye mpambano wa nani mtani jembe ya mwaka jana alipotoa goal ya boko kwa yule mtoto wa mzee pazi!!!!
Ama kweli mtenda akitendewa hujihisi ameonewa...
Awadh Juma sio mtoto wa Idd Pazi, au unamchanganya Zahoro?
 
Awadh Juma sio mtoto wa Idd Pazi, au unamchanganya Zahoro?

Haya mkuu Masuke kwa kuweka sawa kumbukumbu...,....Amavubi nadhani kila kitu kimewekwa sawa na masuke ni Awadh Juma na sio Zahoro pazi, asanten wote
 
Mkolaj umekuja na kiswahili kipya hapa
Hakika hujakosea ndio kwanza nakuleteeni misamiati mipya kama vile escrow, epa, richmond n.k....au wewe unajua maana ya maneno hayo ili uwasaidie watanzania wengine wasiojua maana ya maneno hayo?????
 
Yanga ndo hawana subira ndo maana wanasajili watu waliokaribia kuchukua pension wengine wamejikatia tamaa pamoja na wacheza filamu za ngono.
 
Yanga ndo hawana subira ndo maana wanasajili watu waliokaribia kuchukua pension wengine wamejikatia tamaa pamoja na wacheza filamu za ngono.
Mbona torres ana miaka 30 na bado anawaniwa na vilabu vingi kule ulaya sembese tz mnakocheza kwa kuigiza????, kwani yule kiongozi wenu wa timu ameacha ile tabia ya kuvuliwa suruali na wanaume wenzake na wale wachezaji mashoga wanaolawitiwa wote mliwatimua???
 
Yametimia sasa, phiri na matola wafungashiwa virago simba,, kocha mserbia kuchukua nafasi yake na msaidizi wake atakuwa mnyarwanda..................Orodha ya makocha waliofukuzwa kaz katika vilabu vya ligi kuu tanzania bara kabla ya kumalizika raundi ya kwanza, DENIS KITAMBI-NDANDA FC MTWARA, MARCIO MAXIMO-YANGA DAR ES SALAAM NA PATRICK PHIRI-SIMBA DAR ES SALAAM.
 
Naona mkuu ulipitiwa kidogo, hapo kwenye wiki ilitakiwa iwe siku. Ila huyu jamaa aliyekuja ana CV kali sana, alafu sio babu ni kijana mwenye uwezo wa kuwakimbiza ipasavyo kina kisiga mazoezini.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…