mkolaj
JF-Expert Member
- Mar 24, 2014
- 3,023
- 1,089
Wakati pazia la ligi linafunguliwa kila kocha alijawa na matumaini ya timu yake kufanya vizuri katika harakati za kuchukua kombe, lakini wakati timu zimecheza mechi chache tu za ligi kuu hali ikawa mbaya kwa kocha wa timu ya NDANDA FC ya Mtwara ndugu Denis Kitambi kwa kufunguwa virago.
Mambo hayakuishia hapo tu yakamkuta kocha wa timu ya YANGA SC ya DAR ES SALAAM Marcio Maximo kwa kutupiwa virago baada ya timu hiyo kufungwa katika mechi ya bonanza maarufu kama "NANI MTANI JEMBE".
Naamin hali hii ya timua timua haitaishia hapo tu! na sasa itakuwa zamu ya Patrick Phiri wa timu ya SIMBA SC ya DAR ES SALAAM na hii ni kutokana na mwenendo wa timu hiyo wa kusua sua katika harakati za kupigania kombe la ligi kuu Tanzania bara (vpl).
Huo ni mtazamo wangu na wewe unaweza kutuambia wa kwako kuhusiana na hii timua timua ya makocha katika ligi ya Tanzania, baada ya Maximo huyu atafuata.