Pre GE2025 Baada ya Mbowe kutetea uenyekiti wake, masikini Tundu Lissu, kwishney! Je, atabaki ama atatimka? Lissu Cool down, usiitishe Press kumjibu Mbowe!

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Mbaya zaidi huyo ropo ropo Lisu anatafuta Uenyekiti Kwa kutukana wenzie.

Nadhani Mbowe afanye Kila linalowezekana ashinde harafu tuone kitakachojiri Kwa hiyo Lisu wa Mabeberu
 
mtaka yote kwa pupa hukosa yote,

nadhani athari za hilo zitamshape kidogo backbencher ili siku nyingine awe na hekima na busara katika kufanya uamuzi,

hata hivyo,
uwezekano wa Lisu kusalia chadema ni kidogo mno.

Namtakia kila lakheri in advance 🐒
 
Nimejifunza kwamba kumbe Demokrasia ni kitu cha hovyo hovyo hivi na si kila mtu anakitaka,Magufuli was very right.Tunataka Demokrasia lkn hatutaki the practice of Democracy.
 
Nakubaliana na wewe kuwa Lissu asimjibu Mbowe. Shida ni hata kama atamjibu, Mbowe hatamjibu. Ajipange vizuri kuhakikisha kuwa anapata kura za kutosha kumshinda katika sanduku la kura. Amjibu Mbowe katika mikutano yake ya kutafuta kura.

Amandla...
 
Hamna lolote baya,Me pia napenda Lisu awe Mwenyekiti lakini si kwa kuachiwa bure lazima ambambane.
 
Kwanini msimpe Lissu nguvu akashinde kwenye sanduku la kura?
Kwa nini chadema hawataki Tamisemi isimamie uchaguzi? Kwa nini chadema hawataki kushiriki uchaguzi mpaka kuwe na time huru?
Kwa Nini wasiwape nguvu watanzania wakawapigie kura sanduku la kura?

Naamini umeelewa mantiki ya maswali yangu. Ofisi inayosimamia uchaguzi ni ya kigaila, mrema. Ambao wanamuunga mkono mbowe aendelee, unategemea kutakua na uchaguzi fair?
 
Namuunga mkono Mbowe aendelee kutetea nafasi ya Uenyekiti Chadema, nimegeuza akili yangu baada tu ya kumsikiliza Wenje kwa makini sana.
 
Ma
Leo nimeamini CHADEMA ni mali ya Mbowe na Wachaga, sisi wengine heri tubaki Simba na Yanga huku tukifuatilia Trump anasema nini kuliko kuwa mfuasi wa siasa za Tanganyika
Mali ya ukoo tuwaachie wenyewe inawasaidia kuzidi asali ruzuku.
 
Eti kwa kweli !
 
Wapi kamvua nguo ❓
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…